Rafiki wa kwanza na wa kweli wa maisha yako ni wewe mwenyewe

MERCIFUL

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
2,589
2,000
Hakuna atakayekupenda kama wewe, hakuna atakayekuheshimu kama wewe, hakuna atakaye kutunzia siri zako kama wewe, hakuna atakayekuthamini kama wewe, hakuna atakayefurahia mafanikio yako kama wewe, hakuna atakayekuhurumia Kama wewe
HAKIKA....
Abadani, Asilani!!!
 

Tetramelyz

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
4,103
2,000
Hakuna atakayekupenda kama wewe, hakuna atakayekuheshimu kama wewe, hakuna atakaye kutunzia siri zako kama wewe, hakuna atakayekuthamini kama wewe, hakuna atakayefurahia mafanikio yako kama wewe, hakuna atakayekuhurumia Kama wewe.

Jifunze kujifurahia, kujipenda, kujisahihisha unapokosea, jifunze ku-enjoy company yako mwenyewe, Jifunze kumtafuta Mungu mwenyewe kwa bidii bila kulazimishwa maana yeye ni uzima na afya mifupani mwako. Jifunze kujiwekea mipaka itakayokufanya uheshimike, usiongee kila kitu( kuwa na mipaka kwenye kinywa chako)

Shibisha akili yako na vitabu vinavyojenga, kula chakula chenye afya, jitengenezee mazingira rafiki hasa kwenye nafsi yako, jisemee mambo mazuri, jishughulishe ili usiwe tegemezi.

Mara moja moja ukipata nafasi jipe likizo. Ukianguka amka, jikung'ute mavumbi, na songa mbele.

Ukihisi kuumizwa na kusalitiwa kwa namna yoyote ile; lia kidogo, futa machozi kisha songa mbele.

Usipoteze muda wako kukaa katika maumivu kwani siku zako za kuishi zimehesabiwa.

Usikubali maneno mabaya ya walimwengu yajenge kiota kwenye kichwa chako

Usikubali mtu akuumize bila ruhusa yako.Jifunze kuondokana mazingira au makundi unapoona yanakuondolea amani na kudhoofisha afya ya nafsi yako.

Jifunze kuridhika na ulichonacho huku ukipambana kuwa bora kuliko jana.

Usipende kujilinganisha na wengine hasa kwenye mafanikio labda ukiwa na lengo la kujifunza tu ili na wewe uongeze bidii na juhudi za kufanikiwa.

Mwisho kabla ya kujenga urafiki na wanadamu, jenga urafiki wa karibu na Mungu wako anayejua mwanzo na mwisho wa maisha yako.

Otherwise FURAHIA UHAI ULIOPEWA NA MUNGU NA UTENDEE HAKI UZIMA WAKO

Neema ya Mungu ikuatamie leo!

Niwatakie siku njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujumbe mzuri sana

Mungu akubariki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom