Binafsi sio mtumiaji wa Airtel Internet. Mara nyingi ukiona natumia bundle ya internet ya Airtel basi ni ile inayotokana na vifurushi vya kawaida vya Dakika + SMS + Internet ingawaje mara nyingi hii bundle huwa inapotea tu kwa sababu kwa muda mrefu nimekuwa nikitumia ama TTCL au Halotel.
Kwa watumiaji wa Internet bila shaka wanafahamu uhuni uliofanywa na mitandao ya simu ya kufuta ofa mbalimbali zilizokuwa zinatusaidia wanyonge. Hata TTCL waliokuwa wanatuimbia Rudi Nyumbani Kumenoga nao wamechukua mkondo huo huo.
Sasa katika kutafuta nafuu ndipo nikakutana na ofa ya Airtel Smartphone Double Data. Offer hii ni kwamba, kifurushi unachonunua, unaongewa tena kwa idadi hiyo hiyo, na hapa chini ndo vifurushi vyao-
Naomba ku-declare kwamba, hivi vifurushi sivifahamu ubora wake na kwahiyo imechukua hicho kifurushi cha Sh 3000 ambacho ni 2.5GB +2.5GB kwa majaribio na nikiona kinakidhi viwango vyangu, itabidi nihamie kwenye kifurushi cha Sh 20K.
Ili kujaribu ubora wa hivyo vifurushi, nimeamua ku-download Spy Game yenye ukubwa wa 1.7GB ili nione itachukua muda gani kumaliza downlaoding, na matokeo ya awali ni kama ifuatavyo
Hiyo download speed ya 1.7Mbs/s inapanda na kushuka ingawaje mara nyingi inakuwa chini ya 1MBs/s lakini haijawahi kushuka chini ya 500KB/s. Aidha, hapo natumia simu kama modem (hotspot to PC). Kwangu naona heri ya hii shari kuliko ile shari nyingine ingawaje nitaendelea kufuatilia speed yake katika vipindi vitatu vya siku; yaani asubuhi, mchana na jioni. Na kuweka kumbukumbu sawa, hiyo movie ya 1.7GB ilifika 60% downloaded baada ya dakika 25. Kama hali itaendelea kuwa hivi, nitamuona Airtel "Rafiki" aliyeamua kunifaa kipindi cha dhiki. Kama ndivyo, kwanini basi tusimuunge mkono ili kuwatia maumivu wale wengine?!
Jaribu na wewe uone kama itakufaa kulingana na mahitaji na eneo unaloishi (hakuna mipaka ya eneo lakini kama mjuavyo, signals strenghs za hii mitandao zinatofautiana kutoka eneo moja na lingine
NOTE: Bundle inapatikana kwa kupiga *149*99# kisha unachagua 5, hatimae unachagua 6. Hata hivyo, nadhani unatakiwa ku-activate kwanza lakini sikumbuki vizuri kama option ya ku-activate unaipata hapo hapo kwa sababu binafsi nili-activate juzi lakini nikapuuza hadi leo nilipofikwa maji shingoni na hawa muumiani!
UPDATE: Nimetumia Dakika 39 ku-download hilo faili la 1.7GB.