Rafiki mwema ni yule akufaaye siku ya dhiki: Tuwaunge mkono Airtel na hii offer yao

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
721
1,000
Binafsi sio mtumiaji wa Airtel Internet. Mara nyingi ukiona natumia bundle ya internet ya Airtel basi ni ile inayotokana na vifurushi vya kawaida vya Dakika + SMS + Internet ingawaje mara nyingi hii bundle huwa inapotea tu kwa sababu kwa muda mrefu nimekuwa nikitumia ama TTCL au Halotel.

Kwa watumiaji wa Internet bila shaka wanafahamu uhuni uliofanywa na mitandao ya simu ya kufuta ofa mbalimbali zilizokuwa zinatusaidia wanyonge. Hata TTCL waliokuwa wanatuimbia Rudi Nyumbani Kumenoga nao wamechukua mkondo huo huo.

Sasa katika kutafuta nafuu ndipo nikakutana na ofa ya Airtel Smartphone Double Data. Offer hii ni kwamba, kifurushi unachonunua, unaongewa tena kwa idadi hiyo hiyo, na hapa chini ndo vifurushi vyao-

Bundles.png

Naomba ku-declare kwamba, hivi vifurushi sivifahamu ubora wake na kwahiyo imechukua hicho kifurushi cha Sh 3000 ambacho ni 2.5GB +2.5GB kwa majaribio na nikiona kinakidhi viwango vyangu, itabidi nihamie kwenye kifurushi cha Sh 20K.

Ili kujaribu ubora wa hivyo vifurushi, nimeamua ku-download Spy Game yenye ukubwa wa 1.7GB ili nione itachukua muda gani kumaliza downlaoding, na matokeo ya awali ni kama ifuatavyo

Airltel.png


Hiyo download speed ya 1.7Mbs/s inapanda na kushuka ingawaje mara nyingi inakuwa chini ya 1MBs/s lakini haijawahi kushuka chini ya 500KB/s. Aidha, hapo natumia simu kama modem (hotspot to PC). Kwangu naona heri ya hii shari kuliko ile shari nyingine ingawaje nitaendelea kufuatilia speed yake katika vipindi vitatu vya siku; yaani asubuhi, mchana na jioni. Na kuweka kumbukumbu sawa, hiyo movie ya 1.7GB ilifika 60% downloaded baada ya dakika 25. Kama hali itaendelea kuwa hivi, nitamuona Airtel "Rafiki" aliyeamua kunifaa kipindi cha dhiki. Kama ndivyo, kwanini basi tusimuunge mkono ili kuwatia maumivu wale wengine?!

Jaribu na wewe uone kama itakufaa kulingana na mahitaji na eneo unaloishi (hakuna mipaka ya eneo lakini kama mjuavyo, signals strenghs za hii mitandao zinatofautiana kutoka eneo moja na lingine

NOTE: Bundle inapatikana kwa kupiga *149*99# kisha unachagua 5, hatimae unachagua 6. Hata hivyo, nadhani unatakiwa ku-activate kwanza lakini sikumbuki vizuri kama option ya ku-activate unaipata hapo hapo kwa sababu binafsi nili-activate juzi lakini nikapuuza hadi leo nilipofikwa maji shingoni na hawa muumiani!

UPDATE: Nimetumia Dakika 39 ku-download hilo faili la 1.7GB.
 

holy holm

JF-Expert Member
May 6, 2017
3,260
2,000
Halotel na airtel wapo vizuri mijini lakin vijijin ni spidi ya konokono waliangalie sana hilo Voda tu ndo anatawala sana vijijini kwa spidi yake nzuri lakini vifurushi vyake sasa!
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,806
2,000
Airtel mara nyingi huwa na vifurushi vya bei nafuu sana kulinganisha na mitandao mingine ya simu Tanzania.

Changamoto yao kubwa huwa ni kasi ya internet yao kuwa ndogo. Ingawa hili ni kulingana na eneo ulilopo.

Mfano huwa natumia kifurushi cha mwezi 20,000 wao 22GB wakati kwa gharama hizo hizo napata 8GB Vodacom 🙌😭

Kwa hali hii, kuwa na laini zaidi ya mbili haziepukiki.

Vinginevyo Serikali ije na Ewura yao kwa ajili ya ku regulate gharama za mawasiliano.
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
721
1,000
Airtel mara nyingi huwa na vifurushi vya bei nafuu sana kulinganisha na mitandao mingine ya simu Tanzania.
Changamoto yao kubwa huwa ni kasi ya internet yao kuwa ndogo. Ingawa hili ni kulingana na eneo ulilopo.
Upo sahihi kabisa. Nahisi eneo langu hivi sasa wame-improve speed kwa sababu nilishawahi kununua Modem ya Airtel lakini nikaitupa ghalani kwa sababu speed ilikuwa mbovu sana. Tena umenikumbusha, itabidi niitafute ile modem nijaribu tena manake hotspot na yenyewe inaboa sana.
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
16,834
2,000
Airtel wana changamoto moja tu ya mtandao.

Juzi nimecheki TTCL lile bundle la usiku wamelipiga pin, tigo na voda ndio hawana kabisa. Airtel lipo ila ishu ya speed kwa eneo nilipo ndio linanikatisha stimu.
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
721
1,000
Mm kimekataa
Nadhani moja wapo kati ya haya litawezekana.

1. Je, uliona ile option ya ku-activate ofa?
2. Ikishindikana hapo jaribu kuweka laini mpya, book kwa ajili ya laini mpya sio issue. Nahisi ukiweka laini mpya inaweza kusoma kama "new user"
 

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,467
2,000
Hii si kwa wote. Wale ambao wamekuwa wakitumia Airtel kwa muda mrefu haiwahusu. Nlitaka kurudi kuanza kutumia line yangu ya airtel nliyoitupa last week. But nmejaribu mimi sijapata hizo options. Nimeitoa tena kuachana nayo. Ngoja tuendelee na mitandao ambayo itaturahisishia maisha.
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
721
1,000
airtel wana changamoto moja tu ya mtandao

juzi nimecheki TTCL lile bundle la usiku wamelipiga pin, tigo na voda ndio hawana kabisa. Airtel lipo ila ishu ya speed kwa eneo nilipo ndio linanikatisha stimu
Hilo tatizo hata mimi nilikuwa nalo kwa miaka hadi modem yao nikaitupa ghalani, ndo maana hata hii ya leo niliamua kama kujaribu kwanza kwa sababu sikuwa na uhakika wa speed. Nahisi huku kwetu wame-improve.
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,806
2,000
Upo sahihi kabisa. Nahisi eneo langu hivi sasa wame-improve speed kwa sababu nilishawahi kununua Modem ya Airtel lakini nikaitupa ghalani kwa sababu speed ilikuwa mbovu sana. Tena umenikumbusha, itabidi niitafute ile modem nijaribu tena manake hotspot na yenyewe inaboa sana.
Ukiwa Mtwara Mjini, Nanyamba, Tandahimba network ya Airtel inakuwa Juu Sana, ukiwa nyanda za Juu kusini hadi Dodoma Vodacom inakuwa na speed kubwa.

Hapo lazima umiliki laini zote kuanzia Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel na TTCL
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
35,378
2,000
airtel wana changamoto moja tu ya mtandao

juzi nimecheki TTCL lile bundle la usiku wamelipiga pin, tigo na voda ndio hawana kabisa. Airtel lipo ila ishu ya speed kwa eneo nilipo ndio linanikatisha stimu
Airtel si binamu wa TTCL
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
16,834
2,000
Hilo tatizo hata mimi nilikuwa nalo kwa miaka hadi modem yao nikaitupa ghalani, ndo maana hata hii ya leo niliamua kama kujaribu kwanza kwa sababu sikuwa na uhakika wa speed. Nahisi huku kwetu wame-improve.
ngoja leo nijitusu niweke night pack ni seed downloads zangu ambazo ziko pending tangu halotel wakate utepe ile unlimited bundle
 

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
14,710
2,000
Yes,airtel wanacheap bundles

Ila nikiwa na GB 1 siwezi kuangalia mpira dk 90,Voda natumia 300MB-450MB......kwangu airtel MB huwa zinaisha faster mechi haishi hata dk 30,GB inaisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom