Radio Zetu na Vipindi Vya Mahaba/Mapenzi ifikapo Usiku

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,552
Hivi ni kukosa ubunifu?kukosa habari?au kitu gani?
Tena radio zote wanaigana mwisho Wa siku radio zinakosa maana
Tulizoea kusikiiza BBC radio nadhani ilikua mita band 103.1_lakini sasa inaelezwa frequency zao wamepewa radio mpya ya clouds FM
BBC tulikua tukipata world News 24Hrs,zikiwemo habari za michezo na matukio dunia nzima
Mwito kwa Radio zetu jifunzeni toka vyombo vya kimataifa muache kuigana pia tafuteni habari.Tanzania ni kubwa Matukio ni Mengi sana pia mwaweza fanya Vipindi mkafanya uchambuzi Wa kina kwa yanayotokea.

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Pole mkuu..! Mambo ya dunia ya sasa. Wenyewe wanakuambia "mapenzi yana run dunia". Ukiona hufurahii hayo matangazo badilisha tu station au zima ujilalie zako, ndio mwendo wa ulimwengu wa sasa. Huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono.
 
Aaah!! Me nlikua namskiliza
Tu Godfrey kusolwa wakat
Akiwa sahara midia RFA
aiseee zle songs za kihind
Alikua anajua kuzchambua
Bhana yan kipind kilikua bomba sana
 
Badala ya kutuletea habari za kichunguzi wao wanakalia kufunza watu mambo ya vyumbani...huvi kwanini wasitupe update za tukio LA uhalifu kibiti/mkuranga?maendeleo ujenzi Wa reli,Fly overseas,airports,Sakata LA Drugs_vita ya viroba,bei na hali ya vyakula nchini,Mvua nk mbona kuna Mengi tunataka kujulishwa watanzania?

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Badala ya kutuletea habari za kichunguzi wao wanakalia kufunza watu mambo ya vyumbani...huvi kwanini wasitupe update za tukio LA uhalifu kibiti/mkuranga?maendeleo ujenzi Wa reli,Fly overseas,airports,Sakata LA Drugs_vita ya viroba,bei na hali ya vyakula nchini,Mvua nk mbona kuna Mengi tunataka kujulishwa watanzania?

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
tukio la uhalifu linakusaidia nini.?
 
mi usiku nawekaga redio upendo au wapo redio nakula neno usiku kucha hadi sa kumi na mbili napata habari na baadae naenda clouds fm napata vichwa vya habari magazetin vya kubishania kwenye magroup huku content sijui ila ndiyo sinunui gazeti
 
kuna wa taarifa za habari na kuna muda wa burudani, acheni hizo habarii hakuna asiyependa kupata news lakini na burdani muhimu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom