Radio wapo na mwaipopo.

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,897
4,620
Yule mwanaharakati maarufu kwa kunusa mkando wa ulaji, Said mwaipopo,alikuwepo radio wapo leo, katika kipindi cha meza ya busara, pamoja na wenzake wawili akinadi mazumuni ya kundi lao.
Kwamba ni watu wanaotaka kutetea amani ya nchi inayotaka kutoweka.
Kwamba maandamano yanayofanyika nchini sasa hivi hayana tija na ni uchochezi wa kuondoa amani.
Kwamba kongamano lililoandaliwa na UDASA j/mosi iliyopita lilikuwa na sura ya uchochezi.
Kwamba Kenya walililia katiba mpya lakini haikuwasaidia na hivyo tuko juu sana kuliko wao kwa kila hali.
Kwamba JK kajenga barabara alizozitaja, kutoka Dar mwanza, Lindi Dar na nyinginezo nyingi.
Kwamba uchaguzi ni kwa kura tu na akishatangazwa kiongozi hakuna uhalali wala haki ya kumwondoa aliyechaguliwa hata kama anashindwa kuilinda katiba. Maana wale watakaomwondoa nao ni walewale, akitolea mfano wa Mwai Kibaki. Nk wa kadha.
My take:
Mwaipopo huyu ndie aliyetangaza mda mfupi kabla ya kampeni za uchaguzi mkuu kuanza kwamba anguzunguka nchi nzima kuwashawishi waislamu wasiichague ccm, kwa sababu ya kushindwa kutekeleza ilani yao ya kuwapa mahakama ya kadhi.
Ghafla alitoweka na katika kipindi chote cha uchaguzi hata mda mfupi baada ya uchaguzi hakuwepo nchini.
Habiri zenye uthibitisho zilijuza kwamba alikuwa Somalia ndani ya kundi la Elisha- baab.
Sasa najiuliza kule alienda kujifunza namna ya kutengeneza amani au namna ya kuiondoa?
Ni nani walioifazili safari yake ya zaidi ya miezi mitano?
Najikuta nikijiuliza masuali haya, kwa kuzingatia kwamba kuna kiongozi mmoja mwandamizi (waziri) alilalamika kuundiwa njama za kuuawa na miongoni mwa wauaji wake kuna vijana wa elisha- baab.
Kuna uhakika gani kama huyu mwaipopo sii miongoni mwa hao elisha-baab tishio la viongozi wetu?
Nawakilisha tujadili!!
.
 
Back
Top Bottom