RADIO WAPO na Madaktari Feki. Mnaudhi mno! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RADIO WAPO na Madaktari Feki. Mnaudhi mno!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyamahodzo, Mar 3, 2012.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Siku ya Jumatatu saa 4-6 mchana (muda wa kipindi cha Meza Busara) na usiku kuanzia saa 2 mpaka saa 3:30 kama si 4:00 wanakuwa na vipindi vya tiba vinavyoendeshwa na kijana (wakati wa mchana) na binti (wakati wa usiku.) Wageni wao ni wale jamaa wa tiba mbadala toka pande za Ukonga na Makumbusho.

  Hawa watangazaji wanawaita wateja wao madokta, ... maana ndivyo wanavyotaka kuitwa.

  Kwa mtu unayeifahamu biolojia ya mwili wa mwanadamu (just that of form I-IV) unapowasikia hao "madokta" utagundua ni waongo sana. Wanataja mada wanayokuja kuzungumzia siku husika mfano Magonjwa ya Mfumo wa Chakula. Sasa sikiliza wanapoingia kuelezea mada. Wee!! Wanawaingiza wasikilizaji wa radio kwenye "machaka yenye michongoma, miba-bamba na mbigili hali wasikilizaji wako peku."

  Kinachokera ni kuwa kwasababu tu hawajamaa wamelipia muda wa hewani, wanaachwa kuendelea kumwaga sumu kwa jamíi.

  Siku moja nikabahatika kuipata line wakati wa mchana nikatoa mchango wangu kuonyesha namna huyo Dr feki alivyomwongo na mtupu katika kuelezea mfumo wa mkojo na magonjwa yanayohusiana nayo kisayansi. Na tiba zake zinakuwaje. Nikawa natoa references, cha ajabu nilipomaliza yule dogo Mbise akasema "hayo ni maoni yake"(yaani maoni/mtazamo wangu tu) hakutaka Dr feki ajibu hoja.

  Siku nyingine nikakutana ana kwa ana na mtangazaji wa WAPO Radio, akiwa yupo ndani ya gari ya Radio hiyo, nikamwambia "kwa kuwaingiza hao jamaa wamepunguza sana heshima na mvuto wa kipindi cha Meza ya Busara na Radio WAPO ikiwa anamashaka akajifunze kwa wasikilizaji wa 98.0 FM" Sijui alinielewa kwa kiasi gani.
   
 2. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tanzania hatuna Redio na TV kwa bahati mbaya!!!!! Kuna ile ya Wafu, za mafisadi, watoto wa mafisadi na baada ya hapop za biashara ya kuzugia watu (za dini)
   
 3. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni gazeti mbili tu ambazo zimeweza kuwa huru, Mwanahalisi na Raia Mwema. Wengine wahuni tu! Waoga
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ama!!
  Magazeti yameingiaje tena? Mbona mada haihusiani na magazeti?
  OK, unaweza sema inahusiana lakini ni katika maudhui. Mbona hujazungumzia huo ulinganifu wa kimaudhui?

  Mmmh!!
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kwenye bold unahoja ya msingi iliyo nyuma ya pazia. Unaweza kutusaidia kutupa ufafanuzi japo kwa ufupi?

  Hapo kwenye red, ndiyo radio ipi hiyo?
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,433
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu wee... ukifuatilia songombingo zinazotokea Tanzania unaweza kushikwa vidonda vya tumbo kabisa. Unajua mtu akikunyima elimu amekunyima kila kitu.. hiki ndicho kilichopo Tz hivi sasa. Soma magazeti, angalia TV, sikiliza viongozi wa dini na wasiasa, etc... utagundua kweli tumepotea njia.
   
 7. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenena!!

  Nitakugongea like nikiwa kwenye pc.
   
 8. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mimi kwa kweli naipenda wapo radio kwa dhati hasa kwa ubunifu wa vipindi vya habari kama patapata, na kile cha usiku -yaliyotokea. Kinachonikera ni vile vipindi vya waganga wa kienyeji wanaojiita madokta na vipindi vya kutangaza ule uganga wa kienyeji wa mmiliki wao, askofu Gamanywa. Alianza kwa kusema hakuna lisilowezekana kwa Mungu, ghafla ameamua kumsaidia Mungu kwa kulipisha watu mahela mengi kupata ile ramli yake. Kwa kuwa nchi haina moral standards kila mtu anafanya yaliyomema machoni pake mwenyewe. Kuna siku wataua kila mtu hapa nchini isipokuwa mimi maana sidanganywi na ujinga. Mbona hawajatoa sumu za Mwakyembe mwilini? Nakereka sana na matangazo ya hawa waganga wa kienyeji ambayo makanisa mengi wanaaminishwa ni Mungu.
   
 9. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, uko sahihi.
  Waganga wa kienyeji a.k.a. wachawi wanaiteka WAPO taratibu. Kuhusu Gamanywa na clinic zake za Samaritan nataka niende huko halafu nikamilishe kile nilichoanza kuandika juu ya udanganyifu/madanganyo ya clinic hizo, uhatarishi wa afya za watz na ukwapuaji mkubwa wa fedha zao. Nimeanza kuandika kutokana na kusimuliwa na yule aliyekwenda huko. Naona huruma sijui Gamanywa atajiteteaje. Lakini kwa faida ya watz lazima niweke wazi uozo huo. I can't keep quite.

  Kuna yule mchawi mwingine anasema eti anadawa ya kutibu figo iliyothibitishwa na Wizara ya Afya sijui Muhimbili, halafu anatoa dalili za watu wenye matatizo ya figo na kuwaalika watu waende Magomeni.
   
 10. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  eti wanasema nyie mmesoma sana, sasa imekuwaje ? Au ni kosa la mafundi mitambo !
   
 11. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Pembeni muhusika yuko na Biblia ! Hivi Dr. Ndodi na yule JKBR wako wapi ? Wengind wamepanda daraja ni mitume !
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Hivi ubongo wako utakuwa lini? Ni lazima siku zote uone mambo kwa mtazamo wa "wao na sisi"?
   
 13. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Sisi na nyie, wao na sisi ? Aaaah ! Wapi na wapi ! Tofauti mbona iko wazi, nyie mmesoma, sie tupo tupo ! Nyie mnakufuru sie tunashukuru !
   
 14. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Oh, kwa hiyo tapeli Gamanywa kampata yesu mwingine wa mitishamba?
   
 15. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Wote wameongea na Yesu na akaonyeshwa dawa, kama Mchungaji wa Samunge, yeye aliongea na Bwana kabisa, na akawaponyesha watanzania na viongozi wao ! Sasa mbona inakuwa nongwa kwa Gamanywa ? Mwachieni ale vichwa !
   
 16. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Naomba usiwe mzushi.... ni AIBU ati!!
   
 17. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Theologically a BIG NO. Hakuna YESU wa mitishamba.

  Kiuhalisia, stop calling him tapeli. Anaweza akawa anafanya kwa kutokujua yaani kwa ujinga. Kwasababu masuala ya tiba si fani yake. Kwakuwa ni mjuzi wa kusoma mtu kama huyu inabidi kwenda naye kwa facts.
   
 18. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Ni Askofu na ni msomi, hivyo hawezi kuwa mjinga ila ni mjanja na oppotunist, yaani Tapeli !
   
 19. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nyie mnalaani, sisi tunabariki. Nyie mnahimiza chuki, sisi tunahubiri amani. Nyie mnaua (mkimpigania mola wenu as if yeye ni kiumbe dhaifu asieweza kujipigania mwenyewe), sisi tunaombea na Mungu anasikia maombi yetu kupitia kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo na wagonjwa wanapona.
   
 20. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Askof Gamanywa amekuwa anafundisha Somo la afya na matibabu .Kuna siku alisema hakuna lisilowezekana .Hivyo hata sumu ya Dkt Mwakyembe inaweza kutolewa.
   
Loading...