Radio One, tafuteni watu wanaoongea mambo ya Maana

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,182
7,642
Vipindi mbalimbali vya chombo cha habari vinaweza kuwa na wasikilizaji wengi au wachache kwa kutegemea pamoja na mambo mengine, aina ya watu wanaoshiriki, hoja wanazoongelea, na umakini wa uwasilishaji.

Leo nimesikiliza dakika chache sana Radio One nikiwa kwenye gari, ikabidi nitafute radio nyingine, maana mgeni aliyealikwa, bwana Katambi, hakuna kitu chochote cha maana alichokuwa anaongea zaidi ya siasa zile za kinafiki. Mara anasema vijana wanatumika, mara katiba mpya ni kwa sababu wapinzani hawakushinda kwenye Urais, mara wapinzani wanataka Tume huru kwa sababu wamekosa ubunge.

Ni dhahiri unaona wazi kuwa huyu mtu, kichwani hakujatulia. Hajajiandaa aongelee nini. Anaropoka chochote kilicho karibu na mdomo.

Haongelei kama Tume ni huru au siyo huru. Haongelei kama katiba ina mapungufu au haina.

Radio One tafuteni watu wenye utulivu wa akili, wajuzi wa mambo, wenye fikra pana na watu walio wakweli wa nafsi zao. Waalikwa kama huyu wa leo, watawapotezea wasikilizaji.
 
YAANI Mimi natangaza rasmi kutosikiliza redio one.huwezi kuwapa platform watu jamii ya pimbi Kama katambi!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom