Radio Imaan, Shura ya Maimamu, Basuta na Bakwata Mnatudhoofisha Waislam kwa siasa za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Radio Imaan, Shura ya Maimamu, Basuta na Bakwata Mnatudhoofisha Waislam kwa siasa za Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Borakufa, Sep 30, 2011.

 1. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Islam ni dini iliyokamilia!

  Haiitajiki abadani nasema!! mfumo mwingine toka nje ya uislam ili utendeke au ufanye kazi sawia! Uislam ni mfumo pekee ambao hukuacha chochote! yani hata jinsi ya kunya (kujisaidia mtaniwia radhi) dini hii imefundisha.

  Ole wenu nyie shura ya maimamu, ole wenu ninye basuta, ole wenu ninyi bakwata ole wenu nyie radio imani kwa kuichukua dini yetu hii tukufu na kuifanya mseto na siasa chafu za Tanzania!!! na kutudhoofisha waislam wote ulimwenguni haki hamtakuwa na majibu ya kumpa ALLAH siku saa itakaposimama.

  Leo Kagame wa Rwanda anaupromoti uislamu Rwanda kwa kuwa katika maafa ya Rwanda ni waislam pekee ambao walisimama katika dini hawakujichanganya na mavyama au makabila ! hawakujiusisha kabisa na vita ile mbaya kwa sababu Uislam uliwakataza kutambuana kwa makabila.

  Leo nyie mnatugawa kwa sababu ya mavyama wakati dini haitaki haki mnafanya dhulma kubwa. Allah akuongozeni na mrejee katika mstari.
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  aibu tupu
   
 3. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umeandika maneno makubwa na ya hekma,najua watayasoma na kujisahihisha kama wataona inafaa.
   
 4. N

  NGEDENGE Senior Member

  #4
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HESHIMA SANA SANA MKUU UMEANANDIKA MAMBO MZITO
  MUNGU AKUJALIE WING WA REHEMA mambo ya kuzalau
  uislam kwa sababu ya watu wachache au kikundi cha watu furani sio vizuru
  na tulaani kwa pamoja si wakristo si waislamu watu wanao chafua dini fulan au wanaohusisha na siasa.
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Wakisoma hawatajibu kitu. Unafikiri kuhongwa ubwabwa mchezo.

  mkuu lakini umenifanya nicheke sana....Muhamad amefundisha hadi jinsi ya kunya? Kwani kunya mnahitaji kufundishwa?
  Na kula pia mmefundishwa? Yani mmefundishwa kupiga mpunga? Aseee!
   
 6. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yap...style ni ya ku squat....hata kama mtu anatumia choo cha kizungu ni lazima atapanda juu na ku squat....!ndiyo maana vyoo vingi vya maofisini huwa vinaharibika vile vinanihii vya kukalia!
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kipindi cha 2005 kurudi nyuma enzi hizo CUF ilipokuwa inanguvu na masheikh karibu misikiti yote walipokuwa wanaipigia kampeni misikitini tuliona jinsi ambavyo viongozi wa CCM mapovu yalivyokuwa yakiwatoka kukemea kuchanganya dini na siasa. Kwa kuwa sasa kuna chama ambacho kina nguvu zaidi ya CUF (CDM) ambacho ni tishio kwa CCM, tunashuhudia viongozi wakikaa kimyaa na kueleza kuwa uhuru wa maoni. Baada ya uchaguzi wa Igunga ndiyo watajitokeza kukemea udini, ila kwa sasa kwa kuwa unawanufaisha wanaangalia tu kama nchi haina authorities.

  Tanzania ni nchi yenye watu watulivu sana, lakini vitendo vya CCM ama kwa makusudi au kwa kutojua wanaiyeyusha hulka ya utulivu na kupanda hulka ya shari kwa kutotenda haki. Ni wakati sasa wa viongozi wa dini kuhubiri umoja badala ya mfalakano. BAKWATA leo hii imepoteza imani ya waislam wengi kwa kukubali kuwa vuvuzela la watawala badala ya kuendeleza uislam. Tatizo kubwa la dini hii ya mwenyezi mungu inaongozwa na watu wenye uelewewa finyu wa mambo yote, yaani ya kidunia na kiroho. Leo hii unamkuta sheikh mzima anafanya mambo ya kumshushia heshima na credibility lakini bado anang'ang'ania kuswalisha tu ili ale sadaka za msikiti.

  Nina hakika wanayoyafanya Radio Imaan na masheikh leo hii kama yangekuwa yanaiangamiza CCM basi tungeisha sikia kituo kimefungiwa na masheikh kukamatwa. Dini ya mwenyezimungu imekamilika kweli kwenye kila idara ya maisha. Ila isitumike vibaya kuangamiza chama fulani. Nina imani kuwa kwa mtazamo wa sasa ni kuwa matendo haya si tu yanawazuia waislam wenye uelewa mdogo kuiunga mkono CDM, bali pia yanaifanya CCM kuonekana kuwa ni chama cha kiislam na kuwakimbiza wakristo wenye uelewa mdogo kuiunga mkono CCM. Yaani kwa CCM hii strategy ni ZERO SUM GAME, tena inaweza kula kwao zaidi. Tukemee huu ubaguzi pale tu unapotoa kichwa si kusubiri umuume adui yetu na baadae ndiyo tuukemee.
   
 8. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Ninasikia haja..natoka naja..sijui sura inafundisha je jinsi ya kujisaidia..mimi leo gogo lianguke au kojo litoke..mengine baadae...
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Haya, nyie endeleeni tu.
   
 10. makwimoge

  makwimoge JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mie sichangii kitu nawaachia wahusika waendelee na mjadala
   
 11. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mzaha kama huu ndiyo umetufikisha hapa leo kila kitu tunaingiza mzaha, kama tungekuwa makini tusingeruhusu kugawanya kwa itikadi za kidini leo! acha mzaha katika mambo muhimu.
   
 12. 123yrz

  123yrz Member

  #12
  Sep 30, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Radio imani, bakwata na wapuuzi wengine ulio orozesha hapo ,vyote ni vyombo vyenye mchango kutoka MAGAMBA
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hili nalo neno..lakini si cdm wangeomba msamaha tu. was it too much to ask?

  Au na wao ni kweli wana element za udini -ukristo?
   
 14. t

  tininti Member

  #14
  Sep 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umeongea kama mzawa wa kweli, uislamu unafundisha kupendana wala si kuleta uzushi kwa wengine na kuiaminisha jamii kuwa uzushi huo ni wa kweli. Kwa nini tunatumiwa na CCM (i am sorry) kama con...m ?. Ole wenu bakwata et al mnaochochea moto kutaka kufarakanisha sisi ndugu zute wakristo, kwa kusimamia issues ambazo Magamba wanaziandaa . Kwa nini tusiweke nguvu kuangalia mustakabali wa maisha yetu na vizazi vyetu vijavyo kwa kuanza kuweka mikakati thabiti ya kupata viongozi na taifa ambalo litajali watu na maendeleo yao.Nani asiyejua maisha magumu tuliyonayo yamesababishwa na Magamba, jamani waislamu tuwe makini sana na Magamba.
   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Kama nitakose naomba mnikosoe.
  Mimi ni muislamu ili maamuzi ya viongozi wetu yananipa shida.
  Nashauri mfumo wa kupata viongozi wa kiislamu uangalie pia kiwango cha Elimu dunia, sio kujua tu qurani.
  Kwakuwa tunaishi dunia hakuna budi kutilia mkazo Elimu dunia.
  Viongozi wengi elimu zao ndogo.
   
 16. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ukishachanganya dini na siasa lazima kuchanganyikiwa ni kawaida..
  na hapa inaonekana dhairi kuwa sasa hivi kila kitu wanasiasa wanachofanya wanatumia kigezo cha udini kuficha maovu yao.
  pia tena hiyo radio si bakwata waliipigia kelele kwa kutoa tamko la idd kabla ya bakwata kutangaza..
   
 17. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yap mkuu,
  Unajua dini yetu ilivyo yani ilipo haki ikubali hata kama inatoka kwa shetani ili mradi tu iwe ni haki ichukue na umwache shetani na ushetani wake! lakini pia dini yetu imeharamisha kukata undugu. Hivi leo kama ndugu yangu atakuwa ni mwanachama wa cdm eti naambiwa nimtenge khaa! matamko gani haya ya ajabu ajabu!
  Sisi wenyewe waislam wa inchi hii hatuko sawa kutwa kucha tunapingana leo hawa idd kesho wengine halafu tunajifanya na matamko ya pamoja kwa mambo ya kipuuzi ambayo Allah ameyaharamisha!!
  Hivi kweli sisi waislamu wa nchi hii hatuwezi kushikamana kwa mambo ya muhimu tukashikamane kwa siasa hizi za kizandiki! hatuna mashule, hatuna mahospital hatuna mavyuo tumebaki kutumika tu! jamani hivi mpaka lini??
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  huu waraka angeutoa mufti ungenoga zaidi
   
 19. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ajabu ndiyo hiyo kaka, yani kwenye mambo muhimu tunachinjiana baharini lakini kwenye mambo hovyo kama haya eti tumeungana!
   
 20. t

  thinka JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  tukio la kuvuliwa hijab unaliona dogo lakin saydina omar aliitisha jesh kwa ajili ya kuwatilisha adabu waisrael waliomvua mwanamke wa kiislam.wao wameambiwa waombe radhi ugumu uko wap kama hawakukusudia si waombe radhi yaishe
   
Loading...