Radio Free Afrika watakiwa kujieleza kwanini wasiadhibiwe kwa kurusha kipindi cha 'Amka na BBC' bila mizania

lissu aende mahakamani kwan8ni haonyeshwi tbc wakati ni tunailipia kodi? hivi hamna namna tukawapekeka court..?
 
Hata Maisha ya JF yaliyobakia sio marefu sana kwa sheria hizi!!! Halafu Kuna watu wanaiunga mkono hii serikali na sheria zake dhalimu.

Acha tu, inabidi wanajf tuanze kuambiana ni mtandao gani tutahamia wakitupiga pini. Nakumbuka mara ya mwisho walivyoleta mizengwe tulihamia Kenya Talk.
 
Sawa mkuu, lakini nijuavyo, unaowaita ‘mabeberu’ (Mungu akupe rehema) wana uhuru mkubwa wa upashanaji Habari, na kuwalinganisha na Sisi si Sawa na kufananisha kifo na usingizi!
Unacheza wewe soma hizo kanuni na sheria zake ndio utaelewa. Unaweza kuona labda blogs zao watu wanaandika ovyo kama vile amna control.

Lakini huko kwao BBC1, BBC2, ITV, Channel4 na Channel5 hizo ndio main channel UK wajaribu kuvunja ata kanuni ndogo waone cha mtema kuni hao ata vipindi vyao kwa siku asimilimia kubwa lazima viwe UK made kulinda utamaduni wao.
 
Watanzania watakwambia media zinaonewa wapitie hizo kanuni za regulator wa mabeberu ☝sheria zetu zina afadhali. Upuuzi BBC unaofanya africa awawezi thubutu kuufanyia kwao.

We ukimsikiliza mzungu kwenye kila kitu utaingia chaka huko kwao UK kwenye muungano wao wame devolve mambo kibao isipokuwa vitu vitano tu vya msingi moja kati ya ivyo ni BBC kwanini wanajua ni namna gani media inaweza tumiwa vibaya kuaribu nchi yao kwa iyo kama chombo cha propaganda za serikali kiko kwenye control ya central government.

Huku kwetu wanataka kila aina ya ujinga na upuuzi wananchi wasomeshwe na wasikilizishwe bila ya kujali midhani ya habari, mtu akitaka kusema uongo sawa na upuuzi wowote; serikali yoyote makini duniani aiwezi acha huo upuuzi ata wanaojiita liberal democracies media ni sehemu moja wasiyochekea mambo hatari yanayoweza wagawanya au hata kuwa sehemu ya kuchochea ujinga ndani ya jamii.

Madictator wote huwa na watetezi wa aina yako. Hiyo BBC tumeanza kuisikiliza miaka na miaka, hakukuwa na tatizo, ila tatizo limeanza baada ya magu kuwa rais wa nchi hii!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom