Radio Free Afrika watakiwa kujieleza kwanini wasiadhibiwe kwa kurusha kipindi cha 'Amka na BBC' bila mizania

ORCA ACE

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
746
1,000
Hizi habari za BBC na DW pia zinapatikana online ivyo from today onward tutakuwa tnawasilikiza online
TCRA imekituhumu kituo cha utangazaji cha RFA kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji kupitia kipindi cha 'amka na BBC' kwa kurusha maudhui bila kuzingatia mizania ya habari walipokuwa wanamuhoji Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu juu ya viongozi wa chama hicho kutoshiriki kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa hayati Benjamin Mkapa.

TCRA imesema mtangazaji wa kipindi aliruhusu kurushwa habari iliyoegemea upande mmoja kwa Lissu kutoa tuhuma na kulalamika kuwa serikali ilimnyima nafasi ya kutoa heshima za mwisho bila kumtafuta msemaji wa serikali ili aweze kutolea ufafanuzi tuhuma hizo.

RFA wanatuhumiwa kukiuka kanuni Na. 15(2)(b) na (c) na 16 za mawasiliano ya kielektroniki na Posta(Maudhui ya Utangazaji na Televisheni) 2018.
 

Miiku

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
3,842
2,000
Jf najua kabisa nayo haitakuwepo duniani itapigwa itafariki dunia kazi hiyo itaongozwa Na Mataga
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,490
2,000
Najua upo kazini. Lakini najua pia njaa haina chama. Kwa hiyo nina uhakika uchaguzi huwapi kura CCM. Ila usiwe na wasiwasi naogopa nisijekukuharibia kazi yako.

Nakutakia kazi njema ya kusifia.
Njaa haina chama.

Ukiwa naa akiri timamu jiulize toka 2015 pesa zote za ruzuku na zile mnazokata wabunge mmefanyia nini?
Je kuna kibanda mmejenga?
Kipi kipya kimeongezeka kutokana na hiyo ruzuku?
Je hiyo pesa ni ndogo sana kwenye hicho chama?
Je pesa za wabunge kwa ajili ya kampeni zipo?
Ukipata majibu hayo njoo tuzungumze.
 

santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
1,254
2,000
Watanzania watakwambia media zinaonewa wapitie hizo kanuni za regulator wa mabeberu ☝sheria zetu zina afadhali. Upuuzi BBC unaofanya africa awawezi thubutu kuufanyia kwao...
Unaamini ulichoandika mkuu? Ni mawazo yako au ni mawazo pole pole? Na kama ni mawazo yanayo weza aminika, hapa unatushauri tufanane na ‘mabeberu’?
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
13,349
2,000
Wameambiwa na TCRA ni marufuku kwa vituo vya Radio na Tv za ndani kujiunga na hayo mashirika ya nje bila kupata kibali. Kazi kweli kweli...yaani ni pini kwa kwenda mbele kuelekea uchaguzi.
Main stream media kwa sasa hazina impact kubwa kama social networks tuhamie huko
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
13,349
2,000
Mkumbuke tu, vyombo vya habari hasa vya nje ya nchi ndio huwa chanzo cha machafuko na kutoweka kwa amani katika mataifa mengi duniani hasa Africa, hii ni hatua nzuri kudhibiti mitafaruku inayotarajiwa kutokea...

Na tunaomba serikali ifungie na mitandao ya kijamii hasa Facebook na Twitter.
Miaka yote vimekuwa vikisikika Tanzania kwanini viwe chanzo cha mitafaruku leo.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,284
2,000
Unaamini ulichoandika mkuu? Ni mawazo yako au ni mawazo pole pole? Na kama ni mawazo yanayo weza aminika, hapa unatushauri tufanane na ‘mabeberu’?
Wewe ndio wakijiuliza hilo swali unaamini TCRA wamekosea kweli au unapenda kupinga tu.

Tatizo liko wapi vyombo vya habari kuitwa kutolea ufafanuzi maudhui ambayo TCRA yanaona sio balanced sheria iliyovunjwa wamekuwekea hapo kukwepa ‘misrepresentation’ lazima walau kuwe na jitihada za kupata upande wa pili.

Ndio maana saa zingine unasikia vyombo vya habari baada ya kuripoti malalamiko ya upande mmoja vinakueleza harakati za kupata upande wa pili azikufua dafu ukipiga simu mtu anaetakiwa kutolea ufafanuzi jambo analoshutumiwa apokei/apatikani au chochote kuonyesha ulijaribu you are off the hook.

Media za vijana wadogo tu wanajua hilo iweje taasisi kubwa ishindwe kuelewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom