Radio Deutsche Welle kuna nini na Tanzania?

the truecaller

JF-Expert Member
May 8, 2019
809
940
Naomba kuuliza hili jambo kwa kina.

Hapa nchini tunasikiliza taarifa za habari kwa lugha Kiswahili toka mataifa kadhaa nje miongoni mwao ikiwemo radio Deutsche Welle ya Ujerumani pamoja na BBC Swahili miongoni mwa zilizojizolea umaarufu kwa muda mrefu.

Yako mengi tunayonufaika nayo kwa kina hususan yanayohusu siasa na matukio na habari mbalimbali za mataifa ya nje hususan Magharibi, Ulaya na Marekani.

Na hilo hasa ndio lengo la maudhui ya matangazo yao, kila mmoja akijaribu kueneza siasa, propaganda na tamaduni zaonkuelekea nchi hizi zetu za Kiafrika.

Sasa nijikite kwenye hoja yangu kuhusu hii idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani.

Wao wanatangaza sambamba kabisa na BBC Swahili, hasa jioni na pia asubuhi. Lakini ukiwasikiliza zile contents zao ni tofauti sana.

Wakati BBC Swahili ikijikita kwenye habari na matukio mbalimbali kote duniani, wenzao hawa wajerumani wanajikita zaidi kwenye siasa za Tanzania hususan upinzani, kila mara utawasikia aidha wako na Zitto Kabwe au Maalim Seif, (enzi za CUF).

Lakini pia ukiwasikiliza hawatowi habari chanya kwa serikali ni nadra sana kuwasikia hata siku moja wakimpigia waziri au msemaji wa serikali pale inapotokea tuhuma toka upande wa upinzani,

Tofauti na wenzao BBC Swahili ambao hujitahidi kufanya balanced stories kwa kuwahoji watu wa pande zote pale inapotokea mkanganyiko wa habari. Au jambo ambalo linahitaji ufafanuzi wa pande mbili husika ili mpewa habari au msikilizaji apewe content ambayo sio biased na uponde mmoja.

Lakini pia huwa najiuliza swali lingine bila kupata jibu nalo ni hili.

Hivi wanapokuwa na mahojiano na mtanzania yeyote kuhusu jambo fulani hususan siasa, wao hutumia vigezo gani kuwapata na kujiridhisha nao kwamba huyu aidha kweli ni mchambuzi wa mambo ya siasa za tanzania na sio mwanaharakati wa huo mlengo anaoupigia chapuo?

Na mara nyingi ukimchambua huyo mtu badae unaweza kuta anaitumikia taasisi flani hapa nchini yenye mlengo wa kijerumani. Ambayo inapokea ruzuku zake za kiuendeshaji toka kwao.

Je nauliza tena Detsch Welle Swahili huwa mna ajenda gani nyuma ya pazia.

Hivi kila siku Tanzania hakuna mazuri ya kutangaza au taasisi tofauti na hizi ambazo kila siku ndio ziko vinywani mwenu?

Huwa ukimsikia
Umur heir....basi anamhoji Maalim Seif halafu hakuna kumtafuta mtu wa upande wa pili..

Ukimsikia Hawa bihoga....anamhoji Zitto Ruyaga.
Naye hakuna kubalance tena.

Au utamsikia mtangazaji akimnasibu mtu fulani kama bingwa na mchambuzi wa siasa za Tanzania halafu upande wa pili tunategemea muwe na kiongozi mwingine lakini nyinyi ni nadra sana kufanya hivyo.

Tofauti na wenzenu wa BBC Swahili kulikoni?

Mimi niwasihi nyinyi waandishi wakazi mnaozitumikia hizi taasisi za nje,kutokea hapa nchini. Nina imani maslahi yenu ni mazuri, hivyo mnapaswa kutumia maadili yenu vizuri kwa kutuletea taarifa ambazo zimejitosheleza bila chembe ya ushawishi kutoka makundi fulani kwa maslahi mapana ya nchi yetu, na ustahimivu wa amani yetu.

Mkielewa kalamu huwa ndio silaha ya kwanza ambayo hutumika vibaya huishia kusaini amri za mapigano, kalamu ndio husaini mauziano ya silaha duniani kote hivyo zitumieni vizuri kwa kuleta utengamano popote mlipo duniani.
Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kanuni za kuandika habari, i.e nini kiende hewani na nini kisiende, zinaongozwa na mambo mawili makuu: 1. Sera za chombo hicho 2. Siasa za chombo hicho. Ikitokea waandishi wa DW waliopo hapa Tanzania wanatoa habari unazozisikia ni kwa sababu ndio sera na siasa za DW.
 
Uhuru wa wananchi kupata na kuchangia kusikiliza habari wanazozitaka..

Ukiwa unahisi kuwa ukiwa unafikiria kuwa habari za idhaa ya kiswahili ya radio ya Ujaeumani hazina ukweli au zinapendelea upande mmoja basi nakushauri acha kusikiliza vipindi vyao
Kuna baadhi wanaoweza kuzichukulia umakini kama za kweli kumbe zitto ruyaga amamtumia Hawa bihoga.
Watu wengi elimu duni na ufuasi nyumbu halafu inakuwa shida.

Mtu unavaa gwandana hujawahi kutumi jeshi tangu uzaliwe, mnaunda genge halafu mnaanza kujiita makamanda.

Tatizo hamlioni lengo la mada yangu. Mmezowea matusi na kujibu hoja kwa mistari mifupi badala ya hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuuliza hili jambo kwa kina.

Hapa nchini tunasikiliza taarifa za habari Kwa lugha Kiswahili toka mataifa kadhaa nje miongoni mwao ikiwemo radio Deutsh Welle ya Ujerumani pamoja na BBC Swahili miongoni mwa zilizojizolea umaarufu kwa muda mrefu.

Yako mengi tunayonufaika nayo kwa kina hususan yanayohusu siasa na matukio na habari mbalimbali za mataifa ya nje hususan magharibi, Ulaya na Marekani.

Na hilo hasa ndio lengo la maudhui ya matangazo yao, kila mmoja akijaribu kueneza siasa, propaganda na tamaduni zao.kuelekea nchi hizi zetu za kiafrika.

Sasa nijikite kwenye hoja yangu kuhusu hii idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani.

Wao wanatangaza sambamba kabisa na BBC Swahili, hasa jioni na pia asubuhi.
Lakini ukiwasikiliza zile contents zao ni tofauti sana.

Wakati BBC Swahili ikijikita kwenye habari na matukio mbalimbali kote duniani, wenzao hawa wajerumani wanajikita zaidi kwenye siasa za Tanzania hususan upinzani, kila mara utawasikia aidha wako na Zitto Kabwe au Maalim Seif, (enzi za CUF).

Lakini pia ukiwasikiliza hawatowi habari chanya kwa serikali ni nadra sana kuwasikia hata siku moja wakimpigia waziri au msemaji wa serikali pale inapotokea tuhuma toka upande wa upinzani,

Tofauti na wenzao BBC Swahili ambao hujitahidi kufanya balanced stories kwa kuwahoji watu wa pande zote pale inapotokea mkanganyiko wa habari. Au jambo ambalo linahitaji ufafanuzi wa pande mbili husika ili mpewa habari au msikilizaji apewe content ambayo sio biased na uponde mmoja.

Lakini pia huwa najiuliza swali lingine bila kupata jibu nalo ni hili.

Hivi wanapokuwa na mahojiano na mtanzania yeyote kuhusu jambo fulani hususan siasa, wao hutumia vigezo gani kuwapata na kujiridhisha nao kwamba huyu aidha kweli ni mchambuzi wa mambo ya siasa za tanzania na sio mwanaharakati wa huo mlengo anaoupigia chapuo?

Na mara nyingi ukimchambua huyo mtu badae unaweza kuta anaitumikia taasisi flani hapa nchini yenye mlengo wa kijerumani. Ambayo inapokea ruzuku zake za kiuendeshaji toka kwao.

Je nauliza tena Detsch Welle Swahili huwa mna ajenda gani nyuma ya pazia.

Hivi kila siku Tanzania hakuna mazuri ya kutangaza au taasisi tofauti na hizi ambazo kila siku ndio ziko vinywani mwenu?

Huwa ukimsikia
Umur heir....basi anamhoji Maalim Seif halafu hakuna kumtafuta mtu wa upande wa pili..

Ukimsikia Hawa bihoga....anamhoji Zitto Ruyaga.
Naye hakuna kubalance tena.

Au utamsikia mtangazaji akimnasibu mtu fulani kama bingwa na mchambuzi wa siasa za Tanzania halafu upande wa pili tunategemea muwe na kiongozi mwingine lakini nyinyi ni nadra sana kufanya hivyo.

Tofauti na wenzenu wa BBC Swahili kulikoni?

Mimi niwasihi nyinyi waandishi wakazi mnaozitumikia hizi taasisi za nje,kutokea hapa nchini. Nina imani maslahi yenu ni mazuri, hivyo mnapaswa kutumia maadili yenu vizuri kwa kutuletea taarifa ambazo zimejitosheleza bila chembe ya ushawishi kutoka makundi fulani kwa maslahi mapana ya nchi yetu, na ustahimivu wa amani yetu.

Mkielewa kalamu huwa ndio silaha ya kwanza ambayo hutumika vibaya huishia kusaini amri za mapigano, kalamu ndio husaini mauziano ya silaha duniani kote hivyo zitumieni vizuri kwa kuleta utengamano popote mlipo duniani.
Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda wameona upande wa pili awapati ushirikiano maana huwezi nena bila ruhusa ya mwenyekiti
 
Hoja yangu sio ya usikilizaji binafsi bali iko kwenye madhara ya content zao kwa nchi na sio kama unavyokimbilia kunijibu kama nyumbu

Sent using Jamii Forums mobile app
Umewahi kufikiria madhara ya taarifa za TBC au RFA kwa kizazi cha vijana wa Kitanzania? Huo ni kama wanalishwa hizo taarifa za kuabudu na kusifia wataishia kuwa mazumbukuku katika dunia hii?

Kuliko kuanza kuuliza kwa nini DW wanatoa taarifa zile, nenda kawashauri TBC waache hayo mavipindi ya #Tunatekeleza na kusifia Jiwe
 
Kuna baadhi wanaoweza kuzichukulia umakini kama za kweli kumbe zitto ruyaga amamtumia Hawa bihoga.
Watu wengi elimu duni na ufuasi nyumbu halafu inakuwa shida.

Mtu unavaa gwandana hujawahi kutumi jeshi tangu uzaliwe, mnaunda genge halafu mnaanza kujiita makamanda.

Tatizo hamlioni lengo la mada yangu. Mmezowea matusi na kujibu hoja kwa mistari mifupi badala ya hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo lako unashabikia upande wako, ona sasa unaanza kuleta porojo mara sijui magwanda mara makamanda, haya hao green guard wamepitia jeshi gani?
 
Hoja yangu sio ya usikilizaji binafsi bali iko kwenye madhara ya content zao kwa nchi na sio kama unavyokimbilia kunijibu kama nyumbu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama contents za TBC, TV ya Taifa, za kuisifu Serikali tu na viongozi wa Serikali na CCM, bila ya kubalance stories, hazijaleta madhara kwa Taifa, itakuwa DW ambayo ni idhaa ya kigeni?

Sisi siyo watu wa kuongolea masuala ya kubalance stories, maana hatujawahi kuwa Taifa la namna hiyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom