Radiator, Coolant na Cooling System

Styvo254

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
246
226
Habari za leo wanaJF
Joto, au kiasi cha joto ni muhimu sana kwa mashine na mifumo kama vile kwa viumbe hai. Kunatumika vifaa na sehemu maalum za kutekeleza kazi hii ya kudhibiti joto la mfumo.
Kwanzia na muundo; upitishaji wa hewa/upepo. Amini usiamini, yawezekana kua na engine hata ya diesel isiyotumia mfumo wa maji wa kuipoza joto! Gari la Volkswagen beetle ni maarufu kwa kuutumia muundo huu kwa mda, magari na ustadi mkubwa. Urahisi, kiasi na kasi ya upepo unaopita kando/karibu ya mfumo ni muhimu sana. Kwa muundo huu wa air cooled engine, kuna mabati maalum ya kuelekeza ule upepo panapofaa. Imedhihirishwa kua kuyatoa yale mabati uzuia ule upepo 'kukusanya' joto kwa kua umepungua kasi na kiasi, na hapo 'kuichemsha' ile engine.
Ilikua muhimu kuanzia na air cooled kwa kua hapo ndio engine zilipoanza. Kuongezwa kwa ukubwa na idadi ya piston kulizua matatizo ya 'hot-spots', hizi ni sehemu ambazo joto lilikua linaongezeka kupindikua na kuadhiri mfumo. Ilibidi muundo unaotumia maji 'kukusanya' joto utumike. Hii ilileta mabadiliko na maongezeko ya muundo wa engine na mifumo kwa kua ilihitaji 'water-jacket' yaani mwanya/kovu ambapo yale maji yatatembea na mfumo ya kuyapa mskumo yale maji - water pump.
Tangu pale mwanzo, swala la joto lilikua la msingi pia kwa kuamua aina ya chuma itakayo tumika kuunda mfumo. Cast iron hua inaadhirika na kutu ikiwekwa kwenye maji, madini ya chumvi yanayopatikana kwenye maji pia huadhiri chuma aina nyingine. Hapo basi ilibidi kuvumbuliwa kwa COOLANT ambazo zimeboreshwa kuzuia kutu, kulainisha seal na bearing ya ile water pump na pia 'kukusanya' joto vyema zaidi! Kwa gari zetu hapa waeza pata somo zuri sana la hili swala! Radiator ya gari iliotembea kwa mda hapa (yaani inayotumia maji tu kwenye radiator) utapata tope limeziba ile radiator! Hii ni ile kutu kutoka kwa engine na kuchujwa kwa radiator.
Radiator zilikua zikiundwa kwa kutumia brass hadi teknolojia ikawezesha aluminium kutumika. Aluminium huadhirika/hulika na zile chumvi zilizokwenye maji - sulphates na carbonates. Ukiangalia magari ya kisasa kama Mercedes, RangeRover, L/R Discovery, Freelander na zinginezo zinatatizo la kuzitoboa oil cooler na sehemu zingine zinazogusana na coolant maji yakitumika.
Ni muhimu kutofautisha COOLANT kutoka kwa ANTIFREEZE! Coolant ni kimimini/fluid inayotumika kupoza mfumo - hata maji ni coolant, ingawa yana madhara yake. Antifreeze ni coolant ILA imeboreshwa ili kuganda baridi kwa nyuzi za chini zaidi ya sufuri centigrade! Hii ni muhimu sehemu za Ulaya na kwingine ambako hua na barafu. Kumbuka maji yanapoganda hua yanafura, kwa hiyo yakiwa barafu mle ndani ya water-jacket, yaweza kuipasua engine au mfumo.
Kwa leo nitakomea hapo, Happy Driving!
 
Kama coolant kwenye gari haiishi/haijavuja kuna haja yoyote ya kubadilishwa baada ya muda?

Kama ipi haja ni baada ya muda gani?
 
Kama coolant kwenye gari haiishi/haijavuja kuna haja yoyote ya kubadilishwa baada ya muda?

Kama ipi haja ni baada ya muda gani?
Asante kw swali.
Ipo haja ya kuibadilisha coolant baada ya miaka miwili (miezi 24). Vile viungo vya kuiboresha kuzuia kutu na mengineo huwa vimeisha nguvu.
 
Hizi coolant za lita 1 zinazouzwa kwenye maduka ya spare parts ubora wake ukoje? Nyingine baada ya muda ukidrain utaona ni clear fluid kama maji yanatoka wakati mwanzo ilikuwa ya kijani.
 
Hizi coolant za lita 1 zinazouzwa kwenye maduka ya spare parts ubora wake ukoje? Nyingine baada ya muda ukidrain utaona ni clear fluid kama maji yanatoka wakati mwanzo ilikuwa ya kijani.
Vipi kaka,
Pole kw kmya, kazi zimebana.
Bidhaa zingine kama ujuavyo sio maalum au ni bidhaa gushi. Siwezi comment kwa ujumla au bila kuangazia moja na kuijaribu na kupima ili kujua ubora au udhaifu wake.
 
Habari. Naomba kujua, je kuna coolant za grade tofauti tofauti na kama zipo zipi ni bora kwa Brevis.
 
Wadau kwa hiyo magari ya kisasa yanatumia coolant tu badala ya maji? Maana niliendesha rumion ya mshkaji muda flani cjaona sehemu ya kuweka maji
 
Wadau kwa hiyo magari ya kisasa yanatumia coolant tu badala ya maji? Maana niliendesha rumion ya mshkaji muda flani cjaona sehemu ya kuweka maji

Mkuu, inashauriwa kutumia coolant kwenye chombo chako cha usafiri. Haijalishi ni la kisasa au kizamani, shida/kutokujua ndo kunafanya watu watumie maji badala ya coolant.

Kacheki coolant reservoir tank kwenye hiyo gari ya mshkaji wako, pale ndo watu huwekaga coolant/maji. Sasa sehem ya kuweka maji/coolant ipo ni wewe tu umeshindwa kuiona
 
Ya coolant niliiona mkuu, kuna gari yangu ilikuwa na sehemu ya coolant na maji separately, sasa hii nikashangaa naona moja tu
 
Hizi coolant za lita 1 zinazouzwa kwenye maduka ya spare parts ubora wake ukoje? Nyingine baada ya muda ukidrain utaona ni clear fluid kama maji yanatoka wakati mwanzo ilikuwa ya kijani.
Kuna ile ya ABRi inauzwa 25000 litre 4 je iko freshi ile? Nata niinunue niweke katika gari langu!
 
Mkuu ulishakutana na mfumo wa cooling system ambao una filter (kama oil filter ilivyo) ndani ya hizo filter kuna kuwa chemicals (kama unga hivi) ambazo hizo hubadili maji kuwa coolant?
 
Back
Top Bottom