Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,080
8,219
Mkazi wa Kijiji cha Masweya Kata ya Mtunduru Wilaya ya Ikungi, Vaileth Hassan Mtipa (32) amefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa wanazini na mume wa mtu kwenye pagale la nyumba.

Tukio hilo ambalo linadaiwa kughubwikwa na usiri tangu lilipotokea mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu lakini baadaye limeanza kuzungumzwa huku ndugu wakikiri kutokea tukio hilo.

“Tukio lipo na tumeshamzika lakini uliza viongozi watakuambia, na hadi sasa mwanaume aiyekuwa na marehemu bado anaugulia maumivu kwani alijeruhiwa vibaya miguuni na radi hiyo,” alisema shuhuda wa tukio hilo.

Inadaiwa siku ya tukio hilo, Vaileth alikuwa na mpenzi wake Hassan Nzige na wakati wanafikwa na majanga hayo kwenye pagale walikuwa wakiendelea kufanya mapenzi.

Shuhuda anaeleza kuwa baada ya kupatwa na mkasa huo, Nzige alishindwa kusimama ndipo akaanza kupiga yowe kwa nguvu kwa ajili ya kuomba msaada ndipo watu wakamkuta akiwa hajiwezi wakati mwenzake akiwa amepoteza maisha tayari.

Baadhi ya wanakijiji wa Masweya walimchukua Nzige aliyejeruhiwa miguu yake na kumkimbizwa zahanati ya Ndulungu, kwa matibabu ambapo inadaiwa kuwa kwa sasa anaendelea vizuri.
Mwenyekiti wa Kijiji Masweya, Saidi Hongoa amekiri kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 23, 2021 jioni muda mfupi kabla mvua haijaanza kunyesha.

“Radi ilipiga kabla mvua kuanza kunyesha, wakati huo wapendanao hao wakiwa kazini (wakifanya mapenzi) na wote wawili walikimbizwa katika zahanati ya kijiji cha Ndurungu wakati mwanamke akiwa ameunguzwa vibaya shingoni na mgongoni na mwanaume alikuwa ameunguzwa miguuni, lakini walipofikishwa waliambiwa mwanamke alikuwa amepoteza maisha tayari”, amesema Hongoa.

Amesema baada ya kutokea kwa tukio hilo, juhudi zilifanyika katika kumjulisha mume wake marehemu Violeth, Manase Nkungu aliyekuwa mbali na eneo hilo lakini aliposikia alilipokea kwa masikitiko.

Diwani wa kata ya Ndurungu, Theresia Daudi amsema kuna kila dalili kwamba marehemu Vailenth alifariki papohapo kwa vile aliunguzwa sehemu nyeti za mwili wake japo ni vigumu kueleza.

Mume wa marehemu, Manase Nkungu akiwa na masikitiko amesema hakutegemea kuwa angepata pigo kubwa la ghafla namna hiyo katika kipindi ambacho alimwamini mkewe.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom