Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Radi iliyoambatana na mvua katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imejeruhi wanafunzi 25 na mwalimu mmoja na kuharibu mfumo wa umeme katika shule ya sekondari ya Unberkant wilayani Nyasa ambapo kati yao wanafunzi watatu hali zao ni mbaya.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule hiyo mwalimu Stephano Mwela alipokuwa akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge aliyetembelea shule hiyo kujionea uharibifu uliojitokeza.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Bi. Isabela Chilumba anasema kuwa wilaya ya Nyasa imekuwa ikikumbwa na radi za mara kwa mara kutokana na wilaya hiyo kuwa katika bonde la ufa na kuwa na ziwa lakini kwa wananchi wamekuwa wakizihusisha radi hizo na imani za kishirikina.
Kutokana na uharibifu huo mkuu mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dkt Oscar Mbyuzi kufanya tathmini na kufanyia marekebisho uharibifu uliotokana na radi katika shule hiyo.
Chanzo: ITV