Radi huuzwa SUMBAWANGA TSh 4000 tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Radi huuzwa SUMBAWANGA TSh 4000 tu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mkurabitambo, Oct 5, 2012.

 1. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  KWA wakazi wa Dar es Salaam, mawingu yanapotanda angani na kutengeneza giza ambalo huashiria mvua, kwao huwa ni jambo la kawaida na pengine ni ahueni kwa karaha za joto kali. Lakini kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa, ikiwemo hasa Sumbawanga, dalili ya mvua inayoambatana na radi ni tishio la umauti, kwani mara nyingi radi hizi si za kawaida au za asili bali ni za kichawi na hutengenezwa na wanadamu kwa madhumuni ya kuua.
  Mkoa wa Rukwa hususani wilaya ya Sumbawanga, ni eneo linalosifika kwa imani za kishirikina nchini. Lakini katika masuala ya utaalamu wa radi, yapo maeneo na watu maalum ambao wana uwezo wa kutengeneza radi.
  Ukiwa unatokea wilaya ya Sumbawanga kuelekea wilaya ya Nkasi, ndipo vilipo vijiji maarufu kwa kutengeneza radi hizo.
  Baadhi ya vijiji hivyo ni Sintale na Chipu, ambako ndiko walipo wataalamu wenye uwezo na nguvu za ziada za kutengeneza radi.
  Kwa nini radi zinatengenezwa?
  Radi hizi zinatengenezwa kwa ajili ya kuua au kuwajeruhi maadui. Kwa mfano, kama yupo aliyekudhulumu, aliyekuibia mke au mume, aliyekugonga na gari bila kukulipia gharama za matibabu au anayekutusi na kukukebehi.

  Vijiji vya Sintale, Chipu na Kalundi, vimepakana, kinaanza kijiji cha Kalundi kisha Sintale na cha mwisho ni Chipu. Vijiji hivyo viko duni kimaendeleo na ukubwa. Hata hivyo huku ndipo walipo watalaamu na mafundi wa kuunda radi.
  Nilipokuwa mkoani humo hivi karibuni na mwenyeji wangu, tulielekezwa na wenyeji wa Kalundi kwa mganga wa kwanza nayeitwa Mashaka ambaye anaaminiwa kwa kuunda radi.
  Baada ya kufika kwa Mashaka, tunamkuta akiwa na wateja kadhaa. Ninamweleza shida yangu na kumtonya kuwa ni shida ya kipekee kidogo.
  Namweleza kuwa nahitaji kununua radi kwani nina adui yangu aliyenidhulumu fedha nyingi. Mashaka anajibu kuwa yeye si mtaalamu wa radi bali anatibu maradhi tu.
  Anasema: “Lakini yupo mtaalamu wa radi, anaitwa mzee Chimwaga, anaishi kijiji cha Sintale. Ngoja nimpigie simu sasa hivi,”
  Mganga huyu anazungumza kwenye simu kwa lugha ya kifipa, na baada ya dakika chache anakata simu na kutugeukia na kusema: “Yupo- nendeni- kutoka hapa kwenda Sintale kwa Honda ni dakika 20, mkimuuliza yeyote, atawapeleka kwa mzee huyo,”
  Kwa kuhofia muda, hatukwenda kwa mganga Mzee Chimwaga, na badala yake tunakwenda eneo jingine na kuuliza iwapo kuna mganga mwingine mwenye utaalamu wa radi.
  Mzee mmoja anatuelekeza kuwa yupo mganga anayeitwa Ntoro, mwenyeji wa hapo hapo Kalundi ambaye naye ni mtaalamu wa radi.
  Tunaelekezwa kwa mganga Ntoro, tunapofika tunamkuta akiwa na wake zake wawili na watoto wasiopungua wanane. Anatukaribisha na tunamweleza shida yetu.
  Mganga Ntoro anasema, yeye hutengeneza radi lakini kwa wakati ule alikuwa kaishiwa vifaa, hivyo aliamua kumpigia simu mganga mwenzake mwenyeji wa kijiji cha Sintale ambaye ana ujuzi huo pia.
  Anashika simu, na kumpigia mganga huyo tuliyebaini kuwa anaitwa Maisha, huku akimsisitizia afike haraka azungumze na wateja.
  Wakati tukimsubiri Mganga Maisha afike, tulianza kumdodosa Mganga Ntoro kuhusu utaalamu huo wa kuunda radi.
  Ntoro anasema, kwa kawaida huduma ya radi huuzwa, au hutozwa gharama kwa bei ya kuanzia Sh40,000 hadi 30,000 tu na hiyo ni kulingana na umbali wa eneo alipo mtu anayetakiwa kuuwawa na aina ya radi.

  “Kwa mfano watu wanaotoka Zambia au Kongo tunawachaji fedha nyingi zaidi kwa sababu ya umbali, lakini kwa maeneo ya karibu bei ni nafuu kidogo,” anasema Ntoro.
  Radi hutengenezwaje?
  Ntoro anasema, kwa kabila la kifipa, utaalam wa kuunda radi huitwa ‘Namasata’.
  Radi hutengenezwa kichawi, lakini mtu yeyote anaweza kufundishwa na kuweza kuitengeneza, ili mradi afuate masharti.

  Anasema zipo radi za aina tatu, ya kwanza ni ya maji, ya pili ni ya pembe, na ya tatu ni ya gome la mti. Zote hizo hutengenezwa kulingana na umbali na ubora wake.
  “Radi ya pembe ni ya hatari zaidi, huchoma na kuweza kutekeza watu na mali, na huenda umbali mrefu tofauti na radi ya gome la miti,” anasema
  Huku tukiendelea kumdadisi, mganga Ntoro anasema, radi ya maji hutengenezwa kwa kuchukua sahani mpya, bakuli mpya au chupa ya udongo. Kisha mtaalamu huweka dawa ndani ya chupa au bakuli na kuisemea maneno fulani.
  “Ukishanuiza, unaviweka vifaa hivyo ndani, kesho asubuhi utakuta maji ndani ya chupa au kama uliweka bakuli basi utaona maji ndani ya bakuli,” anasema na kuongeza,
  “Baada ya hapo unachukua vifaa vile na kuanza kunuiza adhabu unayotaka impate mbaya wako, kwa kumtaja jina. Kama huna jina basi uwe na nyayo zake, nguo au kitu chake chochote kile.”
  Anasema baada ya kunuiza, unachukua bakuli au chupa ikiwa juu ya sahani na kuyarusha maji yale juu, kwa nguvu za kichawi, maji yale hupotea lakini kama kutakuwa na kasoro yeyote, maji yale humrudia aliyeyarusha.
  Endapo mtaalamu atairusha radi ile kwa mtu asiye na makosa, basi maji yatarudi chini na kama kweli mtu yule amefanya kosa, basi maji hayatarudi na yatakwenda angani na kuanza kutengeneza wingu jeusi linaloambatana na ngurumo.
  “Maji yakisharushwa juu, baada ya saa moja tu, utaanza kuona angani kiwingu cheusi na kizito sana, mvua inaweza kunyesha kidogo na kisha ngurumo za kutisha … basi hapo ujue kazi tayari na mbaya wako kashamalizwa,” anasema na kuongeza:

  “Kama unairusha radi kwa mtu asiye na makosa kabisa, au ukakosea masharti radi inaweza kukurudia na kukuunguza wewe. Mtu akiniudhi mimi huwa nazirusha tu,”

  Radi ya pembe hutengenezwaje?
  Wakati tukiendelea kumsubiri mganga Maisha, kutoka Chipu, Mganga Ntoro anaendelea kutupa utaalamu huo bila kujua kuwa alikuwa akichunguzwa.

  Sasa anasimulia namna ya kutengeneza radi ya pembe. Anasema, radi hii hutengenezwa kwa pembe ya mbuzi au kondoo, ambayo kwa kawaida huwa na uwazi katikati.
  ‘Tunachukua pembe, tunaweka dawa ndani yake, (yaani kwenye uwazi) tunafunga hirizi kuizunguka pembe, pamoja na shanga, kisha tunanuiza maneno kadhaa ya kichawi, na kisha tunairusha kuelekea alipo mlengwa,” anasema
  Radi hii ni kama kimondo, inaporushwa, hupaa angani na hufuka moshi katika upande wa mbele wa pembe wenye uwazi kama zifanyavyo ndege za kushambulia(rocket).

  Mganga Ntoro anasema, radi hii huweza kupaa umbali mrefu na huweza kuharibu mali, mifugo na binadamu ambaye anawindwa.
  Kuhusu namna ya kutengenez radi ya gome la mti, Ntoro anasema hiyo ina masharti makali ambayo si rahisi kuzitoa siri zake kwa kila mtu.
  Hata hivyo, baada ya muda mfupi, mganga Maisha anapiga simu na kusema kuwa ameshindwa kufika kwa sababu ametingwa na shughuli za mazishi na kutaka twende siku inayofuata asubuhi na mapema.
  Mkazi mwingine wa kijiji hicho, David Ntare anasema mauaji ya radi ni jambo la muda mrefu mahali hapo kwani wanaotumia uchawi wa radi wamekuwa wakijigamba mitaani kwa uweza wao huo.
  “Tangu nazaliwa nasikia vifo vya radi na nina uhakika si radi za kawaida kwa sababu, wanaokufa mara nyingi huwa na uhasama na mtu, kama kumuibia mke,mume, kuiba au kutukana,” anasema Ntare.
  Ntare analihusisha tukio la kuungua kwa benki ya NMB, wilayani Nkasi, tarafa ya Namanyere lililotokea miaka ya nyuma na uchawi wa radi.
  “Ile benki iliunguzwa na radi na mzee mmoja mkulima wa kijiji cha Kizi baada ya aliibiwa hela nyingi katika akaunti yake, akaona alipe kisasi kwa njia ile. Ile benki iliungua wa radi, hakuna asiyejua,” anasema
  Inadaiwa kuwa wenyeji wa hapa aghalabu huviona vitu hivi na hujua madhumuni yake na mara nyingi vifo vya aina hii hutokea wilayani Sumbawanga.
  Anasema, kwa kawaida mtu aliyeungua kwa radi huwa kama aliyeungua kwa umeme.
  “Huungua na kuwa weusi kama mkaa, na wakati mwingine radi hukataa kumuua mtu akiwa ndani, bali humrusha nje na kumchoma huko ili isiwadhuru watu wengine,” anasema.

  Mwalimu wa shule ya msingi Chalantala, Abeid Kisanga, anasema siku moja akiwafundisha wanafunzi wa darasa la tatu somo la sayansi kuhusu radi , mwanafunzi wa kiume alinyoosha kidole na kusema ‘mimi najua kutengeneza radi, baba kanifundisha,”
  Anjelo Singo, Afisa wa Polisi tarafa ya Namanyere anasema suala la ushirikina wilaya ya Sumbawanga na Nkasi ni kubwa na yamekuwapo matukio kadhaa ya vifo vinavyodaiwa kusababishwa na imani hizo.
  “Ingawa serikali haiamini uchawi, lakini matukio ya radi yanayotokea hapa mengi ni ya kishirikina, au matukio ya watu kuuwawa na kukatwa sehemu za siri vilevile ni ya kishirikina,” anasema
  Anasema ni ukweli usiopingika kuwa uchawi umesheheni katika maeneo haya na wakazi wake wameshaathirika kisaiolojia kuhusu hilo.
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya anasema ameshawahi kusikia taarifa za kuwepo kwa wataalamu wa kuunda radi lakini akasema hata hivyo hana uhakika nazo.
  “Unajua jiografia ya mkoa wa Rukwa imekaa katika nyanda za juu, ni rahisi radi kulipuka maeneo haya. Hata hivyo hili suala ni la kiimani zaidi,” anasema
  Anasema pamoja na mambo mengi yanayosemwa kuhusu mkoa huo, kwa sasa maendeleo yanakwenda kwa kasi na anaamini miaka michache ijayo, imani za ushirikina zitapungua kama sio kwisha kabisa.

  SOURCE: MWANANCHI
   
 2. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkurabitambo, naona tuwatafutie Safari viongozi wote wahuni wahuni waende Rukwa, tuwachape na hizi radi..hii tu ndiyo iliyobaki!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli nawashauri hawa jamaa wainunue wakamlipue dr Ndalichako
   
 4. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  myths tupu!
   
 5. awp

  awp JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hao wataalamu wangepatikana Dar ningemaliza watu 3 ambao wananisumbua, ningeomba wanitengenezee radi ya pembe. kwi kwi
   
 6. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  watengeze radi za maendeleo pia si kuua tuu!
   
 7. thesym

  thesym JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 2,439
  Likes Received: 2,170
  Trophy Points: 280
  wakina nani hao
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  Muulize yoyo au Masanilo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. A

  ADK JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,152
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kwani hujui ndalichako aliwafelisha kina nani?
   
 10. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Ikianza vita na malawi tutumie hiyo ya pembe.
   
 11. w

  white wizard JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  hii kitu ni kweli kabisa!mimi mwezi wa 8,nilikuwa mpanda mkoa mpya wa katavi sehemu moja inaitwa maji moto ni karibu na kijiji kiitwacho KIBAONI,Nyumbani kwa waziri mkuu,kuna jamaa alimdhurumu mtu pikipiki,jamaa akaenda kutoa taarifa polisi mtuhumiwa akakamatwa,sijui kilichoendelea huko kesi ikaisha juu kwa juu,mlalamikaji hakuridhika,wakamtia ndani mlalamikaji huyo!kisa amewatukana polisi,baada ya siku 3,wakamtoa,alichowaambia kama ile pikipiki ilikuwa mali yangu sitakubali,akawaaga ndugu zake kuwa anakwenda NAMANYERE,huwezi amini baada ya siku 4,yule kijana aliyetoroka na pikipiki na kuiuza akiwa na jamaa zake kijiweni,lilitokea wingu zito, watu tukabaki tunaulizana kulikoni hili wingu wakati kwa sasa huku mpanda jua ni kali mno!!!mwenyeji wangu akaniambia ukiona hali hiyo jua kuna mtu anatafutwa hapo,bwana bwana baada kama ya dk15,ilipiga radi hiyo sijawahi isikia!!!!kumbe ilimpiga yule kijana kule kijiweni, cha ajabu walikuwa wengi ila ilimvuta yeye pekee yake na kumvutia pembeni na kumuunguza vibaya sana hata kumtambua ni kazi!!!!ndio tuukasikia kelele tukaenda pale hali inatisha!!!!!!Sasa kasheshe ipo kwa wale maaskari polisi kwani nao nasikia aliwaambia kuwa hatakubali,NASIKIA WALIKUWA WANAMTAFUTA WAMLIPE PIKIPIKI YAKE ILI IWE SALAMA YAO!!!!!!!!CHEZEA UFIPA WEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. amu

  amu JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Mimi hiyo ya radi niliisikia mwanza duh nikaogopa
  wacha niwaogope watu wa mwanza nikawaona kiboko
  jamani kuna watu wataalam
  mhhhh nimeogopaje na huu mdomo wangu
  naufunga siongei tena wasije wakaniendea sumbawanga bure loo
   
 13. amu

  amu JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Edit kidogo kuna sehemu umekosea mkubwa tittle umesema 4000 kwenye maelezo umesema 40,000 hadi 30,000
   
 14. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,360
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli basi waifanyie promosheni hiyo biznez yao na watafute mawakala mikoa yote na masharti ni kupewa moja bure uitumie, kama inafanya kazi unanunua zingine.
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Gaidi Sheikh Ponda Issa Ponda et al
   
 16. h

  hargeisa JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  acheni dharau na kejeli kwa waisilamu
   
Loading...