Radar: Wabunge mkitoka london muelekee na uswisi pia

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Katika ripoti yao SFO walisema ukiachia pesa alizowekewa kwenye account zao CHENGE NA IDRISA RASHID kuna pesa zingine
zilitumwa USWISS kwenye account za watu ambao hawakuweza kuwatambua kulingana na sheria za kibenki za nchi hizo sasa
ombi letu kwa wabunge "wenye uchungu" mkimaliza kudai pesa zetu hapo London muelekee na USWISS pia mkadai pesa zetu
zilizotumwa huko. wadau naomba mnisaidie kwanini serikali yetu inaogopa kumdai pesa zetu vithlani pamoja na kuthibitika kutuibia ??
 
"Serikali" mnaipachika mzingo ambao haiuwezi na sina uhakika kama inajua kama hilo ni kosa!! Kwa taarifa yako Mhe CHENGE ni mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CCMgamba!! Tatizo tunafikiri kila kinachoitwa 'serikali' ni serikali. Na hapo ndipo Bongo ilipokwamia!!!!
 
Fuatilia kwa makini uone nani anaujanja wa kutoa hoja hii, wameshindwa kufuatilia hela za hapa ndani kama KAGODA, MEREMETA,TANGOLD na zinginezo sasa unawapa huo mzigo kuongea kigeni kila wanapo ulizwa wanaleta siasa hata kama mambo ni ya msingi hata utawala na uwajibikaji nchini LONDON walienda kutalii ndiyo maana kambi ya upinzani haikuwa na taarifa juu ya kwenda huko London ( soma MWANAHALISI WIKI HII) Hata hivyo maakubaliano ya huko na muafaka wake hauwekwi bayana kama wazo lao limekubalika la kuipa pesa serikali badala ya NGO
 
Hawa wabunge wameenda "kutalii" na Uswisi ni sehemu ni kivutio kizuri cha utalii. Hakuna dhamira wall utashi wa kushugulikia dials hili kwa sababu ambazo walio na dhamana ya kusimamia sheria na taratibu wanazijua. Hivi unamwacha mwizi wa vitu vyako ambavyo unaviona halafu unahangika na fidia kutoka kampuni ya ulinzi....hii haijaniingia akilini.
 
Kwani bado walioenda kuomba chenji hawajarudi? Siku ngapi?ivi si kama nusu mwezi? Kwa nini wasirud,au mpaka leo wako folen ya kuingia ofisi ya BAE Systems? Kwani LONDON ni mbali kiasi icho? Nani alisahau chenj?Mi kwa kweli nimezichoka safari za kitapeli za viongozi wetu. Tanzania ni nchi ya kisanii!
 
Wale wabunge walioenda kudai pesa ya rada nina wasi wasi na akili zao, kabisaa wanapanda ndege, wanapewea posho na kujaa ujasiri wa kudai pesa za wizi ambazo wezi waliyoiba bado wanadunda mtaani na wanakaa nao bungeni, lkn wao wanajifanya hawajui chochote eti wanadanganya wananchi na kuiita pesa iliyozidi dah ama kweli bongo mwizi ni yule anayeiba kuku, anayeiba ma bilioni si mwizi!!
 
Wakirudi watueleze wamepata kiasi gani na kama watakuwa wamefanikiwa tuwaombe wafuatilie za EPA,KAGODA,MEREMETA na MZEE CHENGE ili tujue kweli wanauchungu na nchi yetu na si posho tui zilizowasukuma kusafiri.
 
Back
Top Bottom