Race for Ballali’s seat hots up

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Before you appoint any one as a new BOT Governor, Tanzanians would like to know the fate of that report that was handed to you more than 6 weeks ago and what action(s) would be taken against those who are guilty of wrong doing.

Race for Ballali's seat hots up

By MIKE MANDE
Special Correspondent
THE EAST AFRICAN

The sudden resignation of Bank of Tanzania Governor Daudi Ballali on health grounds has thrown the door wide open in the race for his replacement.

Though the government and the Bank are tight lipped over the issue, sources told The EastAfrican Mr Ballali handed his letter of resignation to President Jakaya Kikwete on December 19.

"We have no official communication at all. We don't know whether he has resigned or not. We are reading this in the newspapers," said Director of Communications at the State House Salva Rweyemamu.

Permanent Secretary to the Treasury Gray Mgonja gave the same answer, insisting he had no information on Ballali's reported resignation.

Mr Ballali had travelled to the US to receive medical attention. But efforts to reach Mr Ballali and Deputy Governor Juma Reli proved fruitless as their phones went unanswered.

Academicians and top bankers are being mentioned as the likely successors.

Among them are Deputy Governor Juma Reli, Dr Natu Mwamba, a director at the Bank, Peter Noni, Director of Economic Policy at BoT and Mr Mgonja, Treasury PS.

Also mentioned is Dr Charles Kimei - who had been at the Bank and is credited with turning round CRDB Bank, now the strongest bank in the country - and Dr Ramadhani Dau, the managing director of National Social Security Fund.

The sudden resignation of Mr Ballali comes at a time when investigations into alleged impropriety in the Central Bank's external payment arrears account, are ongoing and a report is expected to be presented to the government early next year.

In September, Ernst&Young auditing firm was appointed to investigate the alleged financial scam at the Central Bank.

Mr Ballali has in the recent past come under heavy criticism from the public and Members of Parliament who called for his resignation, for allegedly mismanaging public funds at the Central Bank.

The investigations at the central bank are significant because it is the first time the country will be conducting a thorough and independent investigation into the sensitive area of the commercial external debt account that is prone to abuse by corrupt regimes in developing countries.
 
Hiyo ni nafasi ya Prof. Benno Ndulu. Hao wengine wanaotajwa wanaweza kupewa nafasi aliyonayo Ndullu sasa hivi.
 
Hiyo ni nafasi ya Prof. Benno Ndulu. Hao wengine wanaotajwa wanaweza kupewa nafasi aliyonayo Ndullu sasa hivi.

Hii wasiwape maprofesa bana! Sasa huko yunivasiti atafundisha nani? Profesa akafundishe watu watakaopewa nafasi kama hizi baadae. Maana mnatumalizia maprofesa wetu kwa kuwapa kazi ambazo watu wengine wanaziweza kuliko hao mapofesa, ilhali hao wengine hawawezi kufundisha vyuo vikuu. This amounts to sheer misuse or misallocation of scarce resources.
 
Prof. Ndullu ni mmoja wa manaibu Gavana 2 walioteuliwa mwezi August mwaka huu. Huyu bwana aliondoka Mlimani mwaka 1989 akaenda Nairobi kuwa Executive Director wa African Economic Research Consortium. Baada ya hapo alichukuliwa na World Bank akakaa Bongo for some yrs kabla hajapelekwa DC. Appointment yake ya kuwa Naibu Gavana amepewa akiwa World Bank.

Kuna wanao sema kwamba na yeye ilikuwa aje Tanzania kama alivyoingia Ballali. JK alitaka awe mshauri wa Rais wa maswala ya uchumi, but for reasons best known to himself jamaa ali-punch hiyo post. Watu walioteuliwa kuwa washauri wa Rais wa maswala ya uchumi ni mapendekezo ya Ndullu kwamba anawafahamu na wangefanya kazi nzuri. Watu hao ni Dr. Mpango na Dr. Mwinyimvua. Dr Mpango alikuwa akifanya kazi World Bank Dar, na Dr Mwinyimvua alikuwa akifanya kazi za muda hapo World Bank Dar lakini sehemu yake ya kudumu ilikuwa ni Mlimani.

Wadadisi wa mambo bado wanajiuliza, ilikuwaje akakubali post ya u-Naibu Gavana ilhali alikataa nafasi ya ushauri wa Rais? Wapo wanaosema kwamba alipelekwa hapo ili akasome mazingira kabla ya kuikwaa post ya u-Gavana.

Pamoja na hayo baadhi ya watu wanaotajwa hapo juu hawana sifa za kuwa Gavana. Sheria ya BoT ya mwaka 2006 inasema kwamba mtu kuteuliwa kuwa Gavana lazima awe na uzoefu wa kuwa kwenye senior position kwa muda wa miaka 15 kama sikosei, au awe amefanya kazi kwenye mashirika makubwa ya kimataifa kwa muda wa miaka 8. Kwa hiyo mtu kama Dr. Natu Mwamba sijui kama ana-fit, labda kama watapindisha sheria. Hao wengine waliotajwa wana sifa hizo. Lakini nadhani inabidi tusubiri tuone mwisho wa siku mambo yatakwendaje!
 
Damn it, hizi kazi watangaze na sisi tusiokuwa na ma-god father tuombe mbona tumesoma vile vile bana. Kila kazi kubwa rais ateue tu ndio nini ati?
 
Kama sio muislamu au rafiki wa JK hata kama ana CV nzuri kiasi gani asahau! This is stupid but it is what will count. Wait and see!
 
Damn it, hizi kazi watangaze na sisi tusiokuwa na ma-god father tuombe mbona tumesoma vile vile bana. Kila kazi kubwa rais ateue tu ndio nini ati?

Ndiyo maana nilishasema kwamba ili kupunguza makali ya Rais nafasi za uteule inabidi kuwe na kamati itakayokuwa inaangalia mteule kama ana sifa au la. Lakini pamoja na kuwepo sifa za Gavana kwenye sheria, bado Rais anaweza kuipindisha na hakuna mtu anaweza kum-question. Tunahitaji kupunguza madaraka ya Rais kwenye uteuzi wa viongozi.
 
Prof. Ndullu ni mmoja wa manaibu Gavana 2 walioteuliwa mwezi August mwaka huu. Huyu bwana aliondoka Mlimani mwaka 1989 akaenda Nairobi kuwa Executive Director wa African Economic Research Consortium. Baada ya hapo alichukuliwa na World Bank akakaa Bongo for some yrs kabla hajapelekwa DC. Appointment yake ya kuwa Naibu Gavana amepewa akiwa World Bank.

Kuna wanao sema kwamba na yeye ilikuwa aje Tanzania kama alivyoingia Ballali. JK alitaka awe mshauri wa Rais wa maswala ya uchumi, but for reasons best known to himself jamaa ali-punch hiyo post. Watu walioteuliwa kuwa washauri wa Rais wa maswala ya uchumi ni mapendekezo ya Ndullu kwamba anawafahamu na wangefanya kazi nzuri. Watu hao ni Dr. Mpango na Dr. Mwinyimvua. Dr Mpango alikuwa akifanya kazi World Bank Dar, na Dr Mwinyimvua alikuwa akifanya kazi za muda hapo World Bank Dar lakini sehemu yake ya kudumu ilikuwa ni Mlimani.

Wadadisi wa mambo bado wanajiuliza, ilikuwaje akakubali post ya u-Naibu Gavana ilhali alikataa nafasi ya ushauri wa Rais? Wapo wanaosema kwamba alipelekwa hapo ili akasome mazingira kabla ya kuikwaa post ya u-Gavana.

Pamoja na hayo baadhi ya watu wanaotajwa hapo juu hawana sifa za kuwa Gavana. Sheria ya BoT ya mwaka 2006 inasema kwamba mtu kuteuliwa kuwa Gavana lazima awe na uzoefu wa kuwa kwenye senior position kwa muda wa miaka 15 kama sikosei, au awe amefanya kazi kwenye mashirika makubwa ya kimataifa kwa muda wa miaka 8. Kwa hiyo mtu kama Dr. Natu Mwamba sijui kama ana-fit, labda kama watapindisha sheria. Hao wengine waliotajwa wana sifa hizo. Lakini nadhani inabidi tusubiri tuone mwisho wa siku mambo yatakwendaje!

Mbona kama naanza kuwaogopa hao watu wanaotoka World Bank! wasije kuwa kama Balali kwa wizi na ulafi.

-Wembe
 
Mbona kama naanza kuwaogopa hao watu wanaotoka World Bank! wasije kuwa kama Balali kwa wizi na ulafi.

-Wembe

usiogope sana, nadhani shida ni moja ukichaguliwa kwenda kulinda kihenge lazima ujue namna ya kukaa na hao watu. ukweli unabaki hapo hapo, hata iweje come 2010 lazima JK atachota kwenye kihenge lakini ni kwa kutumia njia gani hapo ndiyo hatujui, na jamaa (Gavana) hawezi kusema NO kirahisi lazima awe na guts za kutosha. yeyote akiingia hapo lazima atawachotea wakubwa.
 
Kama sio muislamu au rafiki wa JK hata kama ana CV nzuri kiasi gani asahau! This is stupid but it is what will count. Wait and see!

Siamini sana katika swala la udini na wala si Bagamoyo connection. Ndulu ni mtu wa Morogoro (kwa hiyo Bagamoyo connection haipo), pia ni mkristo (kama kuna mtu alidhani kuna udini pia hakuna), swala la uswahiba sina uhakika nalo. Labda nizame kwenye data za shule hapo Mlimani, maana Ndulu alianza kufundisha Mlimani miaka ya 70s, labda alimfundisha JK ama walisoma wote, lakini siwezi kusema lolote kwenye hiyo area. Na ieleweke kwamba simpigii debe bali ninaangalia possibilities tu.
 
Mbona bado hajiuzulu? Bilai atatoka kikwete atakapoamua, na atamuweka yule anayemtaka mwenyewe.
Huyo atakayeteuliwa, sisi tummulike zaidi, na hata wakichota, si kwa kasi iliyowazi.
 
Ndullu naamini ni msomi mahiri, na kama tunavyopiga kelele humu JF kila siku, hawa wasomi jamani waje watukomboe! Sasa tutaendelea kuwa na vilaza kwenye nafasi nyeti kama hizi mpaka lini? As far as I know Ndulu ana PhD ya economics kutoka the prestigious NORTHWESTERN UNIVERSITY ya chicago, amepublish kwenye major journals kibao, na amefanya kazi Worldbank na kwenye academia, sasa sijui ni kipi kitamfanya na yeye atuibie, lakini kama ni credentials kweli ni unquestionable!

Tusubiri tuone kama muungwana atamchukua. Ila I think kama ana ethics za kazi na ana uchungu na Tanzania basi skills zake kwa kweli tunazihitaji maana ziko relevant kwa matatizo yetu.
 
Jamani nani anakumbuka kwamba Ndulu na marehemu Sanare walishiriki kuunda TRA wakati huo JK akiwa Waziri wa Fedha na walifanya kazi hiyo kwa karibu sana. Hebu tukumbushane kwa hilo
 
Kweli kabisa watangaze hizi kazi na independent pannel isimamie uteuzi wa gavana.

Haya mambo ya watu kubebwa, sijui kafanya Worl Bank, ni ujinga mtupu. WB kuna wakali lakini pia kuna vilaza. Ukiwa na bahati yako unaweza kupata kazi hapo hata kama sio mkali sana.

Ninaweza kumuunga mkono CEO wa CRDB maana mafanikio yake pale yanaonekana.

Lakini muhimu mtu anayetaka kuwa gavana awe na program yake juu ya anataka kufanya nini na sio kwenda kichwa kichwa bila mpangilio.

Kikubwa inatakiwa mtu ambaye ni independent na sio hawa wanaobabaishwa hata na mtu kama Makamba.
 
Kama sio muislamu au rafiki wa JK hata kama ana CV nzuri kiasi gani asahau! This is stupid but it is what will count. Wait and see!

Haswa! upo sahihi kabisa JK anawapendelea sana waislam na kawajaza ktk nafasi zote na hii naamini atapewa mvaa baraghashia tu..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom