RAAWU yataka Dk Ndalichako awajibishwe kwa mitihani kuvuja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAAWU yataka Dk Ndalichako awajibishwe kwa mitihani kuvuja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jul 16, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,718
  Trophy Points: 280
  RAAWU yataka Dk Ndalichako awajibishwe kwa mitihani kuvuja

  Na Festo Polea


  CHAMA cha Wafanyakazi Taasisi za Utafiti, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU), kimesema Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani, Dk Joyce Ndalichako, ndiye anayepaswa kuwajibishwa kwa kusababisha mitihani kuvuja na si wafanyakazi wa baraza hilo.

  Chama hicho pia kimesema kasoro zilizoko katika baraza hilo, haziwezi kuondolewa na watendaji kwa sababu zinatengenezwa na mfumo wa baraza umbalo lina uwezo mdogo kiutendaji na uzembe.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya RAAWU katika Kanda ya Mashariki, Everest Mwalongo, alipokuwa akizungumza na waandishi kuhusu kuondolewa kwa wafanyakazi 79 wa Baraza hilo.

  Mwalongo alisema inashangaza kuona watendaji hao wanahamishwa kwenda kufundisha katika shule za sekondari wakati baadhi yao licha ya kuwa na taaluma ya ualimu, lakini hawakuwa katika kitengo cha mitihani kwa zaidi ya miaka 20.

  Alisema uhamisho waliofanyiwa haukufuata sheria kwa sababu watumishi hao walipewa barua kwa nguvu huku wakisimamiwa na polisi kana kwamba ni wahalifu.

  Mwenyekiti huyo wa RAAWU alisema mbaya zaidi uongozi wa baraza, haukuwasiliana na uongozi wa chama hicho tawi la baraza, kuhusu hatua hiyo, jambo ambalo alisema ni ukiukwaji wa sheria.

  “Cha ajabu hawajatushirikisha na katika uhamisho huo wameua mzizi mzima wa chama cha wafanyakazi ndani ya baraza hilo, wote wamehamishwa sasa hakuna chama cha wafanyakazi katika eneo hilo jambo ambalo si haki na ni kinyume cha sheria,” alisema Mwalongo
  Mwalongo alisema sheria namba 6 ya mwaka 2004
  kifungu cha 7 kinakataza ubaguzi sehemu za kazi na kutaka kushirikisha viongozi au chama cha wafanyakazi kwa kila jambo linalofanyika, ili kuleta ufanisi na kuinua tija.

  Pia alisema Serikali imekiuka sheria namba 6 ya mwaka 2004 na sheria namba 8 ya mwaka 2002 kwa kutoshirikisha chama cha wafanyakazi au viongozi wao, katika jambo hilo.
   
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  HUyu Jamaa Vipi...? wakiondolewa si wanakuja wapya?..Awasubiri wapya waunde chama Kipya cha wafanyakazi....!!!

  Hawa Watetezi walikuwa wapi wakati nchi kila siku inaingia ktk Sokomoko la Kuvuja kwa Paper.
   
Loading...