RA ajaribu kujisafisha kupitia Tanzania Daima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RA ajaribu kujisafisha kupitia Tanzania Daima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Feb 8, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wana-JF nauliza: Kwa nini Rostam anatumia gazeti la T. Daima kama jukwaa ili hali ana magazeti yake. Nazungumza kutokana na stori kuu ya leo katika gazeti hilo, stori ambayo Roistam alikuwa anajaribu kuelezea uhusiano wake na Dowans. Hivi Mbowe, ambaye ndiyo mmiliki wa gazeti hilo analiona hilo na anakubaliana nalo?

  Kuna vitu havijakaa sawa hapa. Kwa nini Mbowe hamtimui huyo mhariri Kibanda ambaye inasemekana ni swahiba wa both RA na EL?
   
 2. n

  nyantella JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Si kalipia kama mteja mwingine? tatizo liko wapi? ni yale yale ya marando na manji! au unashauri wana CCM wasiingie Bills kucheza rhumba? mwachie afanye maamuzi yake katika biashara zake huwezi jua ana maana yake!
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Pandikizi hilo, ni lishushu la ccm
   
 4. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Rostam amekuwa akilitumia sana hilo gazeti kwa sababu amemnunua mhariri wake siku nyingi sana.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mwanzoni hata mimi nilitatizika lakini baada ya kuelezwa kwa kina uhusiano wa Rostam na Kibanda nikabaki kinywa wazi.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Uhusiano huo si Kibanda na Rostam bali ni uhusiano wa

  Mbowe (owner) na EL & RA

  Hawa ni wafanya bishara watu wamesahau wanamuonea mtumwa wao (mfanyakazi) kibanda
   
 7. n

  nndondo JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wale wote wanoona kwamba hili la Kibanda na Rostam lina shida. Haiwezekani RA akatolea breaking news kwenye gazeti hilo inamaana kibanda anashiriki kumtengenezea njia RA na hivyo kumfanya asipate maumivu ya upumbavu wa magazeti yake maana anajua hayaaminiki wala kuheshimika, wala kusomwa na wananchi popote pale walipo. Shit na sielewi kwa nini Mbowe anamchekea hata sijui ni kitu gani.
   
 8. F

  Fareed JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge mara zote wamekuwa wanalitumia gazeti la Tanzania Daima kujaribu kujisafisha kwani wanajua kuwa Watanzania siku hizi hawasomi tena magazeti yao ya Rai na Mtanzania. Wanajua kuwa Tanzania Daima linaheshimika kama gazeti huru, hivyo wanalitumia ipasavyo kueneza propaganda zao.

  Mafisadi hawa wamekuwa wanalitumia Tanzania Daima kila wanavyotaka kwa kuwa mhariri mkuu wa magazeti haya, Absalom Kibanda, yuko kwenye payroll yao. Sambamba na hilo, wamelitumia gazeti hili kumshambulia sana Samuel Sitta na Harison Mwakyembe kwa msimamo wao wa kizalendo dhidi ya DOWANS na uporaji wao mwingine wa mali za umma.

  Kwenye moja ya makala zake, Kibanda anasema kwenye gazeti hilo: "Sitta ni mtu wa visasi, hana uwezo wa kuongoza hata jumuiya ya watu wawili." Maneno kama hayo pia yalitumiwa na Rostam alipokuwa akijibu shutuma dhidi ya Richmond/Dowans.

  Kibanda ameajiriwa kwa muda mrefu na Lowassa kama mhariri wa magazine yake inaitwa UMOJA. Ofisi zake ziko Mikocheni na amekuwa yeye Kibanda muda mrefu yuko huko.

  Freeman Mbowe ni mmiliki wa Tanzania Daima lakini amekuwa akiachia gazeti lake litumiwe na hawa mafisadi. Au mtu huru naye kashanunuliwa? Maana mafisadi wanajaribu kumnunua kila mtu.
   
 9. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmhhhh!!!!!:coffee:
   
 10. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hiyo habari inasemaje?
   
 11. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huyo kibanda keshajengewa kajumba na rostam hivyo ni bora atuachie gazeti letu la t daima la sivyo tutalipiga chini tubaki na mwananchi na raia mwema
   
 12. k

  kohena Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawatakaa wasafishike. Hawa ni Mafisadi tuu
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,056
  Trophy Points: 280
  mimi ndie kaniachsha kusoma hilo gazeti kitambo sasa kwa ajenda zake za kuwabeba Lowassa na Rostam!!!!!!
  yaani kaamua kufa nao sijui aliwapa?/walimpa nini jamani?
   
 14. Kibanda

  Kibanda Verified User

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi ni lini Watanzania tutakuwa watu huru kifikra. Ni lini tutakuwa wakweli wa kile tunachokisema? Ni lini tutajifunza kukisema au kukiandika kile ambacho tumekitafiti na kupata majibu ya kweli juu yake? Miye ndiye Kibanda. Ni Mhariri wa Tanzania Daima. Mnazusha uongo ambao hata majibu hamna au hamjui maana ya gazeti huru.

  Rostam katuhumiwa, mwandishi kampigia simu kakubali kujibu shutuma. tuziache kwa kuwa tunaogopa kwamba eti watu watasema tunamsafisha? Mbona ni Tanzania Daima hili hili na mimi nikiwa Mhariri ndiyo tunaoandika habari na makala za akina Sitta, Mwakyembe, Mengi na wengine wengi ambao wanaonekana kuwa watu wenye mtazamo tifauti na Lowassa na Rostam? Watanzania wenzangu tukatae kulisha ujinga.

  Napenda kuwahakikishia Tanzania Daima ni gazeti huru na linaandika habari pasipo kuegemea upande wowote. Tunaandika habari huru na msimamo wetu huu japo unawakera baadhi ya watu ndiyo msingi wa nguvu zetu.


  Sioni ni kwa namna gani habari hii ya Rostam inavyomsafisha hebu labda niiweke hapa halafu Watanzania wenzangu muipitie halafu mtoe maoni yenu badala ya kusikia tu watu wazushi wakiwalisha uongo:

  "Rostam: Sijutii Dowans

  *Akiri kuteuliwa kuiwakilisha nchini, akana kuimiliki
  *Asema walileta mitambo na kuzalisha umeme nafuu
  *Lipumba amshangaa Kikwete kutowajua Dowans

  Na Mwandishi Wetu

  MFANYABIASHARA maarufu na Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz amesema haoni sababu ya kujutia uamuzi wake wa kumshawishi mwekezaji wa kampuni ya Dowans Holdings SA ya Costa Rica kuleta nchini mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura.

  Rostam, mwanasiasa na mfanyabiashara ambaye jina lake limekuwa likitajwa kwa namna tofauti katika sakata zima la Dowans alisema anaona fahari kwamba kampuni aliyoishawishi kuwekeza nchini iliweza kuleta mitambo hiyo kwa wakati na kuzalisha umeme kwa bei nafuu kuliko ilivyopata kufanywa na kampuni nyingine yoyote nchini.

  Mwanasiasa na mfanyabiashara huyo alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu na kutakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba aliyemhusisha na sakata la Dowans.

  Mbali ya kauli hiyo ya Profesa Lipumba, Tanzania Daima lilimtaka Rostam aeleze sababu ambazo zimesababisha jina lake kuhusishwa na kampuni ya Dowans ama akitajwa kuwa mmiliki na wakati mwingine mwakilishi wa kampuni hiyo ambayo hivi karibuni ilishinda kesi katika Mahakama ya Kimataifa Usuluhishi wa Mizozo ya Kibiashara (ICC) dhidi ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) na kutakiwa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 94.

  Mahojiano kati ya Tanzania Daima na Rostam Aziz yalikuwa ni kama ifuatavyo.

  Tanzania Daima: Leo hii Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amekutaja wewe kuwa mwakilishi wa Dowans uliyepewa nguvu ya uwakili (Power of Attorney) ya kuiwakilisha ambayo inakufanya uwe na nguvu kama ya mmiliki wa kampuni hiyo nje ya Costa Rica

  Rostam: Ni kweli nilipewa Power of Attorney na mwekezaji wa Dowans

  Tanzania Daima: Profesa Lipumba anasema wafanyakazi wa kampuni yako ya Caspian walisafiri hadi Texas, Houston nchini Marekani kuishawishi Richmond kuizuia mkataba Dowans pasipo Tanesco kuwa na taarifa kama mkataba ulivyokuwa ukisema

  Rostam: Nadhani tatizo hapa ni watu kutoelewa namna biashara zinavyofanyika…Kwanza kuna upotoshaji mkubwa katika jambo hili.

  Tanzania Daima: Je, hili la wafanyakazi wako wa Caspian kufanya kazi za Dowans ambalo kumbukumbu zinaonyesha kwamba liligusiwa pia hata katika ripoti ya Kamati Teule ya Mwakyembe unalielezaje?

  Rostam: Tangu mwanzo nilishasema kwamba nilimshawishi mwekezaji wa Dowans kuja kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme

  Tanzania Daima: Lakini Profesa Lipumba analizungumzia hili la wafanyakazi wako kufanya kazi Dowans unalielezaje?

  Rostam: Unapaswa kuelewa kuwa, mwekezaji wa Dowans, Brigedia Jenerali, Suleiman Al Adawi alinipa mimi Power of Attorney kwa kuwa yeye hakuwa akiishi hapa nchini na hakuwa na kampuni. Kwa hiyo halikuwa kosa kwangu kumtuma au kumuomba mtu yeyote kufanya kazi zake

  Tanzania Daima: Naamini unafuatilia kwa karibu mjadala mzima unaohusu hukumu ya ICC iliyoipa ushindi Dowans ambayo inalalamikiwa na wananchi mbalimbali akiwamo Profesa Lipumba alyetoa kauli akikuhusisha wewe binafsi katika suala hili zima.

  Rostam: Sikiliza ndugu yangu, kwanza alichokisema Profesa Lipumba si kipya na ni mwendelezo wa upotoshaji ule ule wa siku zote.

  Tanzania Daima: Una maanisha nini unaposema upotoshaji

  Rostam: Kwanza si kweli kwamba mimi ni mmiliki lakini pili watu wengi wanaolalamika leo wanaonekana kusahau adha ya mgawo wa umeme tuliyokuwa nayo wakati ule Dowans wanakuja. Huyu ni mwekezaji ambaye alitumia kiasi cha shilingi bilioni 150 kuleta mitambo kuifunga na akazalisha umeme wa bei nafuu kuliko wawekezaji wengine wote wa kabla yake na waliopo. Ni jambo la kusikitisha sana kwamba kuna watu hawalioni hilo

  Tanzania Daima: Lakini Rostam kumbuka kwamba kilio cha akina Lipumba na Watanzania wengine ni hili la fidia ya shilingi bilioni 94.

  Rostam: Ni kweli, lakini nilitarajia Profesa Lipumba angefanya utafiti na kuja na majibu ya swali muhimu tunalopaswa kujiuliza, tumefikaje hapa leo hata tulipe kiasi hicho kikubwa cha fedha, badala ya kuanza kutafuta mchawi kwa kupokea upotoshwaji wa wazi kuhusu jambo hilo.

  Awali akizungumzia sakata hilo la Dowans mara baada ya kupokea maandamano ya wanachama wachache wa CUF, Profesa Lipumba alieleza kusikitishwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kudai hawajui wamiliki wa kampuni ya Dowans akiifananisha na kosa la kutojua mipaka ya nchi na watu wake kisheria.

  Profesa Lipumba, aliyekuwa akihutubia katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam wakati wa maandamano ya wafuasi wa CUF, kupinga Serikali kulipa fidia ya sh bilioni 94 kwa Dowans alisema Raiskukana kuwajua wamiliki wa Dowans ni kulihadaha taifa.

  Aidha alisema Dowans yenye makao yake nchini Costa Rica, haina rasilimali zozote na hapa nchini inawakilishwa na Mbunge wa Igunga Rostam Aziz, (CCM) ambaye Novemba 28 mwaka 2005, alipewa mamlaka kisheria

  Alisema mamlaka aliyopewa Rostam ni makubwa na yenye uwezo kuendesha na kusimamia kampuni ya Dowans kama mali yake.

  "Utafiti unaoyesha mawakili wa TANESCO wameeleza wazi mtaji wa Kampuni hii nchini Costa Rica, ni Dola za kimarekani 100, sawa na sh. 150,000 za Kitanzania. Hawana nyumba wala ofisi na wala Dowans hawajafanya biashara yoyote wala kulipa kodi yoyote nchini Costa Rica," alisema Profesa Lipumba

  Akizungumzia hatua ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), kubariki malipo ya sh bilioni 94 kwa Dowans, Profesa Lipumba alisema hatua hiyo ni kinyume cha sheria kwani chombo chenye uwezo wa kutoa dira na mwongozo kwa Rais ni Baraza la Mawaziri pekee.

  Profesa Lipumba, alisema ni muhimu kwa serikali kuzingatia maamuzi ya kamati teule ya Bunge ambapo ilisisitiza umuhimu wa kupitia upya mkataba wa Kampuni ya Richmond na baadaye kuzaliwa kwa Kampuni ya Dowans.

  Hata hivyo alisema kwa mujibu wa kamati teule ya Bunge, Kampuni ya Richmond Development Company LLC, haikuwepo kisheria wakati wa kutia saini mkataba.

  Alisema litendo cha serikali kusema watapinga hukumu hiyo mahakamani ni muhimu kwanza wafanye uchunguzi wa kina kuhusu hukumu hiyo kwani taarifa zinaonyesha kuwa badala ya shauri hilo kusikilizwa makao makuu ya mahakama hiyo nchini Ufaransa, lilisikilizwa jijini Dar e s Salaam.

  Profesa Lipumba, alisema ni wakati sasa kwa Tanesco kufanyiwa marekebisho kwa kujifunza toka nchi nyingine kwa kuwa na mgawanyo wa makampuni yatakayosimamia nishati ya umeme.

  Katika hatua nyingine Chama Cha Kijamii (CCK), kimesema Rais Kikwete hawawezi kujivua kutohusika na mzigo wa Dowans.
  Kimesema Rais Kikwete hawezi kujitofautisha kuwa hawajui wamiliki wa kampuni hiyo bali anaikana kwa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi.

  Mwenyekiti wa CCK, Costantine Akitanda, alisema CCM ina maslahi na kampuni ya Dowans, ndiyo maana imekuwa ikipiga siasa kila linapotajwa kwa lengo la kuwahadaa wananchi

  "Dowans ni suala ambalo CCM ina maslahi nalo, hatuoni ni wapi Rais Kikwete, anaweza kujitofautisha kuwa halijui na pia hawafahamu wamiliki wake," alisema

  Alibainisha uzembe uliofanywa na CCM ndiyo umewafanya walalahoi kuwa gizani wakati huo huo kubebeshwa mzigo wa kulipa kiasi cha sh bilioni 94 kwa Dowans

  Alisema CCM inatambua masilahi yake katika sakata la Richmond ambalo baadaye lilizaa Dowans ndiyo maana aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati teule iliyoundwa na Dk. Harisson Mwakyembe alisema alificha baadhi ya mambo.

  Taarifa hii imeandaliwa na Bakari Kimwanga, Abdallah Khamis na Efracia Massawe.
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ah,kibandaaaa,kwanini ulimchamba samwel sitta?hapo hujajibu mzee
   
 16. garikicah

  garikicah Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  kazi ipo kubwa sana
   
 17. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kibanda pole sana, nakusikitikia kwa sababu huelewi unavyoacha mianya nyuma ya kutiliwa mashaka. Ni bora ukawa muungwana ukakikiri udhaifu itakusaidia kuwa huru.

  Rostam alishakanusha siku nyingi kuhusika na Dowans, baada ya mambo kuwekwa wazi kaona mtu pekee wa kuitengeza hiyo habari ni wewe!!!!!!!

  Kibanda tunakufahamu, ulitumika hata kujaribu kupotosha ajali ya Dr Mwakyembe, usivyo na aibu wala utu, uliona fedha tamu kuliko ubinadamu, tunakufahamu saaana Kibanda.

  Hebu wasome wenzako wa East Africa walivyo iandika hiyo habari uwe kuyaona mapungufu yako. You are not smart enough kukwepa kueleweka uko wapii. Shame on you!
   
 18. a

  artist Member

  #18
  Feb 8, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii story imeandikwa na nani?Juu ni "Mwandishi Wetu"

  Chini kuna majina matatu ya waandishi ni nani kati yao alipiga hiyo cm au wote waliongea na Rostam kwa wakati mmoja na Je, huyo Mwandishi Wetu ni hao wa chini au ni mwingine?

  Ha ha ha da nchi hii tusali sana
   
 19. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,024
  Likes Received: 8,508
  Trophy Points: 280
  Hebu yasomeni majibu ya Rostam ningependa kuona wanajf jinsi mnavyoyapangua kwa hoja ili jamaa huyu asisafishike.
  Kuhusu kibanda bgup man you got gut .
  Kwani sita ninani bana.huyo si ndo amejenga ofisa ya spika kijijini kwao?hafai
   
Loading...