Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Raia Mwema
Lula wa Ndali Mwananzela
Nilikaa pembeni nikisikiliza kwa makini maelezo ya Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz (CCM) akielezea na kufafanua msimamo wake kuhusu hatua ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania kukana mchango wake na kumruka kufuatia kushiriki kwake kwenye hafla ya uzizundi wa albamu ya kwaya ya Amkeni usharika wa Kinondoni. Bw. Rostam alishiriki katika siku kuu hiyo jumapili ile iliyopita ya tarehe sita ambapo yeye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.
Maelezo yake kwa waandishi wa habari yamenifanya niamini kuwa Bw. Rostam anapaswa kuchunguzwa na vyombo vyetu vya usalama ili kuondoa utata wowote wa mambo ambayo anayafanya ambayo kwa kuyaangalia (kama nitakavyoonesha) siyo tu yanaweza kusababisha vurugu isiyo ya lazima, lakini kwa hakika yanachezea utawala wetu wa demokrasia, misingi ya haki, na michakato ya kidemokrasia nchini.
Sitopenda kurudia kile alichosema kwani aliyoyasema siku ile Jumapili na aliyoyarudia jumapili hii kwa waandishi wa habari yote yanaweza kusikika vizuri kwenye tovuti ya http://www.klhnews.com. Hata hivyo yatosha kusema kuwa majibu ya Rostam baada ya KKKT na Mch. Mtikila na wenzake kuanzisha kelele za kutaka arudishe fedha alizotoa pale Kinondoni kumenifanya niamini pasipo shaka kabisa kuwa Bw. Rostam ni mwanasiasa mjanja, mwenye dalili ya vitendo vya rangi ya majivu majivu, na ambaye endapo ataendelea kuonewa haya atakuwa anaweka mchakato wa kisiasa na demokrasia nchini kuwa matatani.
Kwa wale wanaokumbuka Aprili 16 (siku mbili tu baada ya Rostam kumpatia fedha Mtikila) niliandika makala kwenye gazeti hili iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho Sipendi Rostam Azizi atikise kiberiti Bungeni. Wiki ile inayofuata mwandishi mmoja alijitokeza na kumtetea Rostam na kujaribu kuchambua hoja zangu, jaribio ambalo wiki moja baadaye niliweza kulionesha udhaifu wake na mwandishi wetu yule kutokomea bila kujibu.
Katika makala hiyo ya kwanza niliandika hivi kuhusu Mhe. Rostam Aziz Kama wananchi wengine Rostam ana haki ya kujitetea na mahali ambapo anaweza kujitetea pasipo shaka sana ni hapo bungeni kwani huku uraiani haina kinga ya kusema awezacho. Kama kweli Rostam anaamini hakutendewa haki na ya kuwa amebebeshwa mzigo usio kuwa wa kwake kwa yeye kuchutuma na kuendelea kuubeba si tu anajidhihakisha lakini anafanya watu waamini kuwa yaliyosemwa juu yake ni kweli.
Nikaongeza na kusema hivi, Rostam ni mwana CCM, hajanyamazishwa wala kukatazwa kusema. Kama hatopewa nafasi bungeni anavyo vyombo vyake vya habari na anao waandishi wake wa kumpamba, awatumie ili siri itoke. Hata hivyo akumbuke kuwa wewe ukijua hili, wenzio wanajua lile
Na mwisho nikagongelea msumari kwa kuhitimisha kwa wito huu Ninampa changamoto asimame aseme, vinginevyo na anyamaze! Kama amezoea kutisha wana CCM wenzake, aendelee kufanya hivyo hivyo lakini asifanye kama walivyofanya mafisadi wa EPA ambao wameliteka Taifa huku sisi wenyewe tukiwa hatuna uwezo wa kufanya lolote. Sitaki Rostam kwa maneno yake na yeye aliteke Taifa, kwani hatuwezi kutekwa mara mbili!
Baada ya mwandishi yule kunijibu, niliandika makala ya pili ambayo ilikuwa na kichwa cha habari Rostam: Mtu mzima hatishiwi nyau na kimsingi niliendeleza nilichoandika kwenye makala ya kwanza. Mwishoni mwa makala hayo nilisema hili lifuatalo Kwa upande wangu narudia nililosema kama analo lake la kusema na anafikiri ameonewa asimame ajitetee; wenye kutikisika watatikisika na Tanzania haitotishika. Wale walio mabua ya mitete ambao wanatetemeka akikohoa na kukosa pumzi akipita waende kupanga foleni na kumlilia asiseme.
Mimi nasema Rostam anatikisia kiberiti ambacho akikiwasha vitakavyoungua ni yeye na nguo zake na za marafiki zake. Sisi wengine tutakaa pembeni kuwachora wanavyoumana na kutafunana kama mchwa. Kama haamini na asubiri.
Ndugu zangu Rostam siku ya Jumapili amejaribu kukiwasha kiberiti na walioshtuka kwa mlio wake wameruka pembeni kwa woga. Amejaribu kutikisa na kutuma ujumbe kwa wabaya wake, lakini kama nilivyosema akikiwasha vitakavyoungua ni yeye na nguo zake na za marafiki zake. Huu ni wakati wa kuonesha kuwa alichokifanya siku ya jumapili ni kuthibitisha kuwa anayo nguvu ya pekee katika Tanzania, nguvu ambayo inampa aina fulani ya kiburi na uwezo fulani wa kibabe. Kiburi kwamba anauwezo wa kuamuru mvua inyeshe ikanyesha na jua kuwaka likawaka. Tuanze pole pole kumchambua.
Kuitisha waandishi wa habari anaowataka.
Sijui ina ukweli gani habari kuwa Bw. Rostam alitoa mwaliko kwa waandishi anaowataka yeye ndio waende kumsikiliza. Kwamba, vyombo vya habari havikuwa huru kupeleka mwandishi wanayemtaka na badala yake majina yaliyopendekezwa ndiyo walitakiwa kwenda huko. Kwa kuangalia kwa haraka ni baadhi ya wahariri waandamizi ndio walialikwa kwenda kumsikiliza. Binafsi napinga kabisa mtindo wa viongozi kuchagua ni waandishi gani waende kumsikiliza au vyombo gani vya habari viende.
Mtindo huu umetumiwa hata na Rais mwenyewe wakati fulani ambapo anaamua ni waandishi wa vyeo gani waende kumsikiliza. Inasikitisha kuwa waandishi wetu na hasa wahariri wanakubaliana na upuuzi huu. Nimetumia neno upuuzi nikimaanisha hivyo. Jukumu mojawapo la vyombo vya habari na waandishi hasa linapokuja suala la utawala bora ni wao kuwa kiungo cha habari kati ya watawala na watawaliwa. Katika kufanya hivyo vyombo vya habari vinatakiwa kuwa huru kufanya kazi yake pasipo kuingiliwa na watawala.
Mtawala anapokuja na kusema nina jambo la kusema kwa wananchi, na ningependa x,y waje kunisikiliza na kuwaambia wananchi mara moja kengele za tahadhari hazina budi kulia. Jukumu la mtawala au kiongozi ni kusema lini, wapi na nani ana la kusema na ni jukumu la waandishi wa habari kuona umuhimu wa kuripoti jambo hilo na kuamua nani anafaa kwenda kusikiliza.
Hivyo, kitendo cha Rostam kuitisha waandishi anaowataka yeye (aidha moja kwa moja au kwa kuashiria chombo kingine) ni kumpa nguvu ambayo haistahili na kwa hakika ni kucompromise suala zima la kuripoti tukio lake. Yeye mwenyewe akiwa ni mmiliki wa vyombo vya habari, ni wazi kuwa ana ushawishi wa aina yake katika vyombo hivyo. Ni vizuri kuanzia sasa vyombo vyetu vya habari (kupitia Baraza la Wahariri au chombo kingine kinachowaunganisha) kuchukua msimamo wa pamoja wa kukataa kugawanywa na watawala na kuhakikisha kuwa wao wanabakia na uamuzi wa mwisho wa nani aende kuripoti kuhusu nini. Kiongozi asiyekubali hilo basi vyombo vyote vimgomee (ukiondoa vile vyake).
Ni kwa misingi gani Rostam alichagua waandishi waliokuja kuripoti habari zake? Je alitumia ushawishi wowote wa ahadi au vitisho kupata waandishi anaowataka yeye?
Rostam na Mtikila
Mojawapo ya mambo ambayo yalifunua sura ya Rostam ni urafiki wake na Mch. Christopher Mtikila. Wengi wetu tumekuwa tukiona mara nyingi jinsi Mch. Mtikila amekuwa akimshambulia Rostam katika mambo mbalimbali. Kumbe kwa mujibu wa Rostam hawa jamaa wawili wanafahamiana kwa ukaribu na urafiki wa kiasi cha kupeana/kukopeshana fedha! Unapofikia mahali unampa mtu fedha lazima kuna kiwango cha kuaminiana na ukaribu. Sidhani kama mtu yeyote ambaye anakutuhumu hadharani akija na kukuomba fedha utampa. Isipokuwa kama na wewe una kitu unakipata toka kwa mtu huyo.
Kwa watu ambao tumekuwa tukifuatilia suala la Rostam na Mtikila kuna baadhi ya matukio ambayo hayana budi kuonesha ni jinsi gani hawa jamaa wawili kama siyo ni wazugaji wa kimataifa basi wote wawili wamekula njama ya kuihadaa Tanzania kwa malengo ya kusaidiana. Nikumbushe matukio machache tu:
Kwanza, tarehe 16/9/2005 Mchg. Mtikila alitoa madai mazito sana kumhusu Rostam na Kikwete. Madai hayo ambayo yalinukuliwa na vyombo mbalimbali hasa wakati wa mchakato wa uchaguzi Mkuu. Katika madai hayo Mch. Mtikila alisema kwamba anazo taarifa kuwa Serikali ya Iran imekuwa ikimtumia Bw. Rostam fedha nyingi ambazo zilitumika katika kampeni ya mgombea wa CCM Bw. Jakaya Kikwete. Mch. Mtikila alisema kuwa Wairan wamekuwa wakimtumia Rostam kwa sababu ya nasaba yake na ya kuwa wana maslahi fulani kama Kikwete angechaguliwa. Madai haya ya Rostam pamoja na uzito wake hayakuchunguzwa na vyombo vyetu vya sheria na usalama.
Sasa kwa watu wengine hili wanaweza wasiwe wameliona. Wiki moja kabla ya mkutano huu na waandishi wa habari (yaani tarehe 9), Kampuni ya Kagoda Agriculture ilisajiliwa na siku iliyofuata (jumamosi) ikawa tayari imepata mikataba mikubwa kutoka Benki Kuu. Je, yawezekana fedha ambazo Mch. Mtikila alikuwa anazizungumzia wiki moja baadaye hazikutoka Irani bali Benki Kuu? Yawezekana kuwa sababu kina Rostam na Kikwete hawakumshtaki Mtikila ni kwa sababu ingejulikana hakuna cha fedha za Irani bali kukombwa kwa fedha toka Benki Kuu?
Pili, Kumbukumbu yangu ni nzuri kwani hayo hayakuwa madai ya pekee dhidi ya Rostam na Kikwete kupokea fedha kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kampeni zake. Mwezi wa Aprili mwaka huo huo gazeti la African Confidential liliandika taarifa kuwa Bw. Rostam alipokea shilingi Bilioni mbili (vijisenti mara mbili!) kutoka Oman kwa ajili ya kampeni zao. Licha ya vitisho vya mgombea wa CCM Bw. Kikwete kuwa atafungua mashtaka dhidi ya gazeti hilo, hakufanya hivyo kwani gazeti hilo lilimuambia atangulie kwenda mahakamani kwani ushahidi upo na ni mkubwa. Siyo Kikwete wala Rostam aliyefungua mashtaka. Kwa maneno mengine walikubali jambo hilo.
Kitendo cha vyombo vyetu vya usalama kutokufuatilia habari nyeti kama hizi au hata kuomba ushirikiano kutoka kwa Mtikila na gazeti la African Confidential kumethibitisha ni kwanini wengine wamekuwa wakipiga kelele juu ya kulega lega kwa usalama wetu wa Taifa.
Kama Kikwete alipokea mabilioni ya shilingi kutoka nje ya nchi ili afanikiwe kuwa Rais, alifanya hivyo kwa misingi gani? Hao waliomtaka aingia kwa udi na uvumba, kwa mbinde na kwa pinde walikuwa na maslahi gani?
Anaposema yeye msafi, Rostam anajilinganisha na nani, Kikwete?
Tarehe 17 Machi mwaka huu Mch. Mtikila tena akaja na madai mazito juu ya Rostam. Safari hii akagusa eneo nyeti sana nalo linahusu Uraia wa Rostam. Mchg. Mtikila akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake alisema hivi Licha ya kuwa Bw. Rostam ni rafiki yangu, siwezi kumtetea yeye kuliko nchi yangu? ushahidi wa kuwa yeye sio Mtanzania ninao, maana najua mpaka hospitali aliyozaliwa na mpaka sasa, wazazi wake wako Iran. Rostam alipoulizwa na mojawapo ya vyombo vya habari siku hiyo hiyo hakukanusha wala kusema lolote isipokuwa kusema Wanasema mimi siyo raia...asante sana...asante sana.
Sasa hilo linaweza lisiguse fikra zako ndugu msomaji hadi pale mwezi mmoja baadaye, yaani tarehe 14 Aprili mwaka huu ambapo kwa maelezo ya Rostam ndiyo siku ambayo yeye alimpatia Mch. Mtikila kiasi cha Shs. Milioni 3. Kwanini Rostam alimpatia fedha Mch. Mtikila mtu ambaye amemtuhumu kuwa si raia mwezi mmoja kabla yake? Katika mazungumzo yake juzi alimuelezea Mtikila kwa maneno makali akidai kuwa maneno yake (Mtikila) yamejaa kinyaa, chuki, ubaguzi, na yananuka ufisadi. Alipompa milioni 3 alikuwa hajui hayo yote? Au ni kitu gani kilikuwa kinawaunganisha?
Katika haya yote tuliyaona tunaweza kuona kitu kimoja ambacho kwa wale wenye kumbukumbu nzuri watakigundua. Sijui kama umewahi kuiona picha ya urafiki wenye mashaka. Katika picha hii wanyama mbalimbali wamechorwa wakiwa kwenye tafrija nyikani, na wanyama ambao ni mahasimu wakiwa karibu karibu, hivyo simba na swala wako pamoja, chui na mbuzi wako pamoja wanasherehekea. Katika hayo yote wote wanaangaliana kwa mashaka kwa maana huwezi kujua ni lini nani atamgeuka nani.
Rostam na Waandishi wa habari.
Mojawapo ya vitu ambavyo vimemfanya Rostam kuonekana ana malengo ambayo yanamfanya aonekana ni mmoja wa watu wenye urafiki wenye mashaka ni jinsi gani amekuwa akihusiana na waandishi wa habari. Kuna madai mengi ambayo ni yeye pekee anaweza kuyathibitisha ya jinsi gani anaweza kumlipa mtu kwa sababu fulani, hata kama mtu huyo ni adui au rafiki yake. Alipoamua kuingia kwenye biashara ya magazeti kuna madai mengi sana ya jinsi gani amekuwa akishawishi uandishi wa magazeti yenye hisa zake hususan kuhusu habari zake.
Kama nilivyoonesha hapo juu jinsi wito wake ulivyotolewa kwa vyombo vya habari kumekuwa kama mtu mwenye ubia wa aina ya pekee. Swali langu kwa Mhe. Aziz ni hili, kama kweli yeye ni mtu msafi kama alivyodai, na kwa vile inaonekana amekuwa akitoa misaada ya fedha kwa watu mbalimbali wakiwamo mahasimu wake; je yuko tayari kutaja majina ya waandishi wa habari ambao amewapa fedha ambazo si mikopo kama fadhila yake na watu hao wameendelea kumuandika vibaya? Kwa maneno mengine, waandishi wanafiki ambao wameandika habari za madai ya ufisadi dhidi yake licha ya kupewa fedha na Bw. Rostam? Je kuna waandishi ambao wamelipwa na Bw. Rostam na ambao hawajawahi kuandika habari zozote mbaya dhidi yake? Tukisema huo unaodaiwa kuwa ni mtindo wake ni ishara ya vitendo vya kifisadi atakataa?
Rostam naUshirika Usio Mtakatifu
Wakati anazungumza na waandishi wa habari aliowaita Bw. Rostam alisema yafuatayo baada ya kutangaza kuwa maneno ya Mtikila ni kinyaa, yananuka harufu ya chuki, wivu, ubaguzi, unafiki na ufisadi Bw. Rostam aliendelea na kusema hivi huu ni mwendelezo tu wa kampeni chafu unaoendeshwa na watu wachache ambao ni maarufu na ni wazito katika jamii yetu waliojiunga pamoja katika ushirika usio mtakatifu. Ambao kwa kutaka kutimiza malengo yao wameamua wanaoyajua wao wenyewe wameamua kuchafua majina, heshima, na hadhi za baadhi yetu.
Katika kikundi hicho wapo ambao hawaridhiki na nafasi za uongozi walizonazo, ambao wamejenga chuki kwa kudhani na kujiaminisha kuwa labda mimi nilihusika kuwazuilia kujichukulia fursa za ufahali na haki inayostahiki vyeo vyao...wapo ambao uwezo wa maarifa yao umewapeleka kutomudu ushindani wa kibiashara na badala yake wamejianimisha labda baadhi yetu ndio sababu ya kutofanikiwa kwao, na wapo ambao wamejiingiza katika kikundi hicho kwa sababu ya wivu. Mawazo yote hayo si sahihi, na yanaelekea kunipa uwezo ambao sina.
Swali ambalo mimi ninalo kwa Mhe. Rostam na ambalo wenye uwezo wakuchunguza wachunguze ni kuwa Bw. Rostam anawajua hawa watu kiasi kwamba ameweza kujua wako katika makundi gani. Je yuko tayari kuwataja watu hawa ambao yeye amewaita ni maarufu na wazito katika jamii yetu? Maana kama hawa watu wapo na wanaendeleza hizi kampeni za kuchafuana naamini Watanzania wangependa kuwajua ni kina nani? Vinginevyo kuna mtu amhoji Bw. Rostam ili tuweze kujua ni kina nani chanzo cha kuchafuana kunakoendelea. Vinginevyo, tutaweza vipi kumuamini Bw. Rostam kwa maneno yake hayo?
Umiliki wake wa Richmond
Kati ya majibu ya kijanja ambayo nimewahi kuyasikia ni pale alipoulizwa kuhusu kuhusishwa kwake na Richmond. Mhe. Aziz hakukana kumiliki au kuhusika katika kumiliki kampuni ya Richmond. Alichofanya Bw. Rostam ni kuelekeza utetezi wake kwenye ripoti ya Kamati Teule ya Mhe. Mwakyembe. Alichosema ni kuwa Kamati Teule haikusema yeye ni mmiliki na hivyo basi ina maana hamiliki au kuhusika katika umiliki wake. Huu ni mtitiririko mbovu wa ujengaji hoja (illogical flow of an argument). Kwa vile Kamati Teule haikusema anamiliki RDC, haina maana hamiliki. Binafsi ningependa kumsikia yeye Rostam akisema kuwa hakuhusika katika umiliki wake na hakuwa na maslahi yoyote yale. Hadi hivi sasa yeye hajakana.
Taifa linahitaji kujua ni nani aliyekuwa mmiliki wa RDC tangu mwanzoni?
Mwisho
Ndugu zangu, naweza kuendelea kusema mengi. Lakini kati ya mambo ambayo yamedhihirika katika jambo hili na ambalo inaonesha ipo haja ya Rostam kuchunguzwa na vyombo husika ni kuwa, kwanza, Uhusiano wake na Mtikila na habari ambazo Mtikila amekuwa akitoa zinaonesha kuwa chanzo kikubwa ni yeye mwenyewe Rostam. Kuna mambo ambayo yamekuwa yakifanywa na kusemwa na Mtikila ambayo kama siyo Rostam chanzo chake basi ni mtu wa karibu wa Rostam. Hilo la pili naliondolea uwezekano mkubwa kwani kama Rostam anataka kuwa mkweli angesema ni mara ngapi nyingine pasipo risiti ambapo amewahi kumpa Mtikila fedha kwa kiwango chochote kile kwa shughuli nyingine? Je amewahi kumlipa Mtikila kuhusiana na kesi zozote ambazo Mtikila amekuwa akifungua aidha dhidi ya serikali au dhidi ya mambo mbalimbali likiwamo mojawapo ya magazeti maarufu nchini?
Hivyo mtu mwenye ujasiri na chombo chenye ujasiri hakina budi kuanzisha uchunguzi kwanza kujua ushiriki wake katika kupata fedha kutoka nje ya nchi wakati wa kampeni za mgombea wa CCM Kikwete mwaka 2005, na vipi kuhusu fedha ambazo imedaiwa na gazeti mashuhuri la African Confidential, fedha za Shs. Bilioni mbili toka Omani kumsaidia Kikwete. Na zaidi ipo haja ya kufanya uchunguzi wa mahusiano ya watu hawa wawili isije kuwa wote wawili wanachotufanyia ni uzugaji wa daraja la kwanza kwani kama wana urafiki basi ni urafiki gani huo na kama ni uadui ni uadui wa aina gani huu.
Vinginevyo hawa wawili yawezekana kuwa ni watu ambao wanaweza kutuletea matatizo makubwa huko mbeleni kama hakuna mtu atakayewafunga breki. Binafsi, simuamini hata mmoja wao kwani nilichoona ni dalili ya unafiki wa mchungaji na mwanasiasa!