R Robert Kisena: Dar Rapid Trans kuanza January 10

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,790
141,684
Mwenyekiti wa Uda Transit amesema mradi wa Dart unakaribia kukamilika na wao wanatarajia kuanza kutoa huduma january 10, 2016. Amesema mabasi yao mapya ya kisasa capacited to carry 80 and 150 psgs yapo tayari kulihudumia jiji la Dar.

Chanzo: Startv habari

Wito wangu wahakikishe kabisa taratibu za kikodi kwa hayo mabasi zinazingatiwa ipasavyo kutuepusha na usumbufu wowote sisi abiria endapo HAPA KAZI TU itayafikia.

Ahsante!
 
Yaani mradi uliojengwa kwa fedha zetu tulizokopa huyo muhuni Robert Kisena ndio anakuwa msemaji wa Watanzania!!! Akiwa kama nani hasa? Walimchezea Kikwete ngosha atawanyoosha tu
 
Huo mradi wa DART nao ni miongoni ya majipu makubwa yanayopaswa kutumbuliwa.
Hivi ni mradi wa aina gani huu usiofika mwisho wake, huku tukishuhudia bomoabomoa ya kila siku kwenye barabara hiyo hiyo iliyokwisha kukamilika?!
Au pengine hao makandarasi walishapiga dili ya kula cha juu kama walivyozoea na wakajenga chini ya kiwango na baada ya kuona Tingatinga ametinga Ikulu, makandarasi hao wanalazimika kujenga 'upya' barabara hiyo ili wasije kumbwa na kimbunga cha Double M, which means a combination of Magufuli + Majaliwa.
 
Huyu jamaa simwamini kabisa, amekaa ujanja ujanja tuu! Lazima kapiga ndefu za kiharam, mkulu amulike huku!
Alafu kumbe DART ndo UDA! Duh!
 
Back
Top Bottom