Your doubletalk is self contradictory.
Sidhani kama kuna kanuni.Ngoja waje wajuvi tuskie.Yako makosa mengi sana, matumizi ya maneno " yeyote na yoyote " bado nichangamoto. Wekeni kanuni ya matumizi R na L hapa twende pamoja. Au nikukariri tu hakuna kanuni?
Tatizo hili sio hapa jf tuu.yaani Wahandishi na watangazaji karibu wote kwenye tv za mitandaoni .wana tatizo hili R na L
Hawa wa H ndo wanakera zaidi bora hata R na L unaeza sema mbwembweTatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.
aibu umesema haibuHuu ni ugonjwa wa taifa, ni 'haibu' sana miandiko mibovu kweli mpaka watu maarufu wenye nyadhifa kubwa tu serikalini ama mashirika binafsi hawajui kutofautisha r na l, a na ha, inafikia hatua msomaji unaona hata aibu kwa niaba ya mwandishi
Makabila yote ya kanda ya nyanda za juu kusini hayana herufi 'R' kwenye misamiati yao. Kwa mfano wanyakyusa hawana herufi 'V' na 'R' badala yake sehemu yenye v kuna 'f' na r kuna 'l'. Kwa sasa V wanaweza kuitamka vizuri ila R imeshindikana kabisa.Lazima tufike sehemu sasa tukubaliane na hali, kanda ya ziwa, mbeya kote, kanda ya kati na sehemu mbalimbali hizi herufi zimeshaashindikana. Tukubali tu kama vile mjerumani hawezi kusema roho anasema hoho au mtu wa india kusema wewe hawezi hata umshikie bunduki atasema veve. Au kama kiingereza cha kimarekani kilivyo tofauti kimatamshi na kiingereza cha uingereza. Kuna sehemu mpaka bbadhi ya majina yameathirika KAROLI...KALOLI,nk
Wazenji huwa wanasema 'tumefiriwa'. Sasa sijui upande upi upo sahihi kati ya sisi wabara tunaosema TUMEFIWA na wazenji wanaosema TUMEFIRIWA. Wanakiswahili nisaidieni hapoWakurya wakisema tumefiwa utacheka au uji mtamu sana
Huu uzi unamhusu Faiza Foxy mwenyewe.Naamini wana JF wote mpo sawa. JF imepata bahati kuwa na waandishi au wadadavuaji wazuri sana.
Lkn wapo ambao wanasumbuliwa na Maneno 'R' na 'L'. Baadhi hawajui R watumie wapi na L waweke wapi. Kuna mwana JF kaandika lais JPM badala ya rais JPM.
Mwingine kaandika jambo lahisi...badala ya jambo rahisi.Mwingine kaandika mahali 'namshukulu Mungu,' badala ya 'namshukuru Mungu'.
Wapo pia wanaotatizwa na neno 'hawezi kufika' wakiandika 'awezi kufika'.
Nia yangu ya kuandika uzi huu ni kwamba, tusome vizuri uzi za wadadavuaji wa JF ambao tunawajua wako vizuri kwenye kiswahili maana Elimu haina mwisho.
Tunaweza kupinga na kubeza kila kitu, na kutukana mitandaoni kutwa kuchwa bila kusahau vigodoroZinawasumbua sana sana wanachama wa CCM na mada zao!
Na pia wengi wasiopenda wenzao waongee Kiingereza!
Sisi Watanzania hadi Kiswahili ni shida,sijui tutaweza nini dunia hii!
Shame on us!