Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?

Opuk Jater

Senior Member
Dec 25, 2018
145
130
Habari Wanandugu,

Katika kitu ambacho huwa kinanishangaza katika nyakati hizi ni maandishi na matamshi ya baadhi ya herufi na silabi. Huwa najiuliza kuwa Watanzania tunakwama wapi kwenye herufi "R" na "L" kuanzia kuyaandika mpaka kutamka?

Miaka ya nyuma kulikuwa na kichaka cha kujificha kuwa kuna Makabila ambayo hayana herufi "R" kwenye lugha zao za nyumbani, hasa mikoa ya kusini (Lindi & Mtwara).

Lakini siku hizi siyo kushindwa kutamka bali yanabadilishwa kabisa. Utakuta mtu na elimu yake anakuandikia "RAKINI" badala ya "LAKINI", Eti " KALILI" badala "KARIRI", kuna muda unamsikiliza mtu mpaka unashindwa kumwelewa kama anaongea kiswahili au anatumia lugha nyingine.

Tena kuna hawa Wachungaji na Manabii ukiwaskia wakiongea ndiyo wanazikazia " L" badala ya "R". Halafu hapo bado haujahamia kwenye vyombo vya habari.

Sasa cha ajabu siwani wakiwa wanabadili matumizi ya R na L wakiwa wanazungumza Kiingereza. Kwa hiyo huu ugonjwa ni ulimbukeni uliotujaa au ni wa makusudi?


MAONI KUTOKA KWA WADAU

Hizo ni athari za lugha ya nyumbani na sio rahisi kubadilisha kama unavyofikiri.Lugha yoyote inayokuja kwako kama lugha ya pili lazima itaathiriwa na lugha ya kwanza.Nailo ni swala la ulimi sio akili.Hata wazungu kwenye nchi wanazozungumza kingereza wanatofautiana lafudhi kati ya nchi na nchi wakati lugha ni ile ile.kwaiyo hiyo ni kawaida sana kwenye jamii yetu na kamwe hatuwezi kufanana ulimi.
------------
nuruyamnyonge, Haya si makosa ya kisarufi, useme kwa mfano, kusema anakujaga ni makosa, Kiswahili sahihi ni kusema anakuja.

Haya ni makosa ya kuchanganya herufi.

Kwa mfano, Magufuli mtu atamke "Magufuri" au "Mzee wa Kiraracha" mtu atamke "Mzee wa Kilalacha".

Hivyo basi, utaona ni vigumu kuweka kanuni katika makosa ambayo kimsingi si ya kisarufi (grammatical), bali ni ya kimatamshi (phonetical).
 
Hizo ni athari za lugha ya nyumbani na sio rahisi kubadilisha kama unavyofikiri.Lugha yoyote inayokuja kwako kama lugha ya pili lazima itaathiriwa na lugha ya kwanza.Nailo ni swala la ulimi sio akili.Hata wazungu kwenye nchi wanazozungumza kingereza wanatofautiana lafudhi kati ya nchi na nchi wakati lugha ni ile ile.kwaiyo hiyo ni kawaida sana kwenye jamii yetu na kamwe hatuwezi kufanana ulimi.
 
Naamini wana JF wote mpo sawa. JF imepata bahati kuwa na waandishi au wadadavuaji wazuri sana.

Lakini wapo ambao wanasumbuliwa na Maneno 'R' na 'L'. Baadhi hawajui R watumie wapi na L waweke wapi. Kuna mwana JF kaandika Lais Magufuli badala ya Rais Magufuli

Mwingine kaandika jambo lahisi badala ya jambo rahisi. Mwingine kaandika mahali 'namshukulu Mungu,' badala ya 'namshukuru Mungu'. Wapo pia wanaotatizwa na neno 'hawezi kufika' wakiandika 'awezi kufika'.

Nia yangu ya kuandika uzi huu ni kwamba, tusome vizuri uzi za wadadavuaji wa JF ambao tunawajua wako vizuri kwenye kiswahili maana Elimu haina mwisho.
 
racso kaunda, ]
Tatizo hili sio hapa jf tu. Yaani Waandishi na watangazaji karibu wote kwenye TV za mitandaoni wana tatizo hili R na L
 
Kiranga,

Kwenye kutamka ndio ana shida, sina hakika anapoandika. Hilo la kumtaka hana ujanja nalo kutokana na utumiaji mkubwa wa lugha ya mama utotoni, hilo halina mjanja ni kwa yoyote huweza kuathiriwa na mother tongue.
 
Yako makosa mengi sana, matumizi ya maneno " yeyote na yoyote " bado ni changamoto. Wekeni kanuni ya matumizi R na L hapa twende pamoja. Au nikukariri tu hakuna kanuni?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom