'R' na 'L' zinatusumbua wengi JF

racso kaunda

Member
Joined
Aug 16, 2019
Messages
51
Points
125

racso kaunda

Member
Joined Aug 16, 2019
51 125
Naamini wana JF wote mpo sawa. JF imepata bahati kuwa na waandishi au wadadavuaji wazuri sana.

Lakini wapo ambao wanasumbuliwa na Maneno 'R' na 'L'. Baadhi hawajui R watumie wapi na L waweke wapi. Kuna mwana JF kaandika Lais Magufuli badala ya Rais Magufuli

Mwingine kaandika jambo lahisi badala ya jambo rahisi. Mwingine kaandika mahali 'namshukulu Mungu,' badala ya 'namshukuru Mungu'. Wapo pia wanaotatizwa na neno 'hawezi kufika' wakiandika 'awezi kufika'.

Nia yangu ya kuandika uzi huu ni kwamba, tusome vizuri uzi za wadadavuaji wa JF ambao tunawajua wako vizuri kwenye kiswahili maana Elimu haina mwisho.
 

nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Messages
4,114
Points
2,000

nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2014
4,114 2,000
Yako makosa mengi sana, matumizi ya maneno " yeyote na yoyote " bado ni changamoto. Wekeni kanuni ya matumizi R na L hapa twende pamoja. Au nikukariri tu hakuna kanuni?
 

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
47,306
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
47,306 2,000
Kwenye kutamka ndio ana shida, sina hakika anapoandika. Hilo la kumtaka hana ujanja nalo kutokana na utumiaji mkubwa wa lugha ya mama utotoni, hilo halina mjanja ni kwa yoyote kuathiriwa na mother tongue.
Watu wanajifunza na kunyoosha lugha. Hajataka tu.

Mbona kuna wazee wengi tu wamezaliwa huko na wanaongea vizuri tu.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
37,339
Points
2,000

RRONDO

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2010
37,339 2,000
Tatizo hili sio hapa jf tuu.yaani Wahandishi na watangazaji karibu wote kwenye tv za mitandaoni .wana tatizo hili R na L
Tatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
47,306
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
47,306 2,000
nuruyamnyonge, Haya si makosa ya kisarufi, useme kwa mfano, kusema anakujaga ni makosa, Kiswahili sahihi ni kusema anakuja.

Haya ni makosa ya kuchanganya herufi.

Kwa mfano, Magufuli mtu atamke "Magufuri" au "Mzee wa Kiraracha" mtu atamke "Mzee wa Kilalacha".

Hivyo basi, utaona ni vigumu kuweka kanuni katika makosa ambayo kimsingi si ya kisarufi (grammatical), bali ni ya kimatamshi (phonetical).
 

Noelia

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2017
Messages
12,368
Points
2,000

Noelia

JF-Expert Member
Joined May 26, 2017
12,368 2,000
Huu ni ugonjwa wa taifa, ni 'haibu' sana miandiko mibovu kweli mpaka watu maarufu wenye nyadhifa kubwa tu serikalini ama mashirika binafsi hawajui kutofautisha r na l, a na ha, inafikia hatua msomaji unaona hata aibu kwa niaba ya mwandishi
 

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
47,306
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
47,306 2,000
Tatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.
Hili ni tatizo la kimataifa, Wajamaica, hasa wa Kingston, katuka Kiingereza wengi hawajui kuweka h sehemu inapotakiwa na wanaiweka sehemu isipotakiwa.
 

morenja

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Messages
4,335
Points
2,000

morenja

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2012
4,335 2,000
Tatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.
Mimi ni typing error, ni kweli nimekosea na nilijaribu nirekebishe ikanigomea.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
24,119
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
24,119 2,000
Watu wanajifunza na kunyoosha lugha. Hajataka tu.

Mbona kuna wazee wengi tu wamezaliwa huko na wanaongea vizuri tu.
Sipingi hoja yako, lakini naona ni tatizo la kawaida kwa wengi. Na ni wachache sana wanafanya jitihada kuondokana na hilo kwani ni tatizo linalovumika na kueleweka dunia kote, na katika lugha zote.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
24,119
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
24,119 2,000
morenja,

Huku kwenye mitandao ni kosa la mtu kushindwa kuandika au kujua herufi sahihi. Tatizo lake Magufuli ni wakati wa kuongea, hayo ni matatizo ya kibinadamu kutoka lugha moja au nyingine. Sioni shida yoyote kwake kwenye hili.
 

Forum statistics

Threads 1,353,025
Members 518,223
Posts 33,070,085
Top