Tetesi: R. Kelly atishia kujiua nyumbani kwake, simu ya dharura yapigwa Polisi

Kwetu Masaki

Member
Mar 10, 2019
8
11
Msanii nguli wa muziki wa R’n’B nchini Marekani, R. Kelly ametishia kujiua, hii ni baada ya polisi Mjini Chicago kupokea simu ya dharura kutoka kwa mwanamke mmoja ambaye hakujitambulisha jina akiwataka kuwahi upesi nyumbani kwa gwiji huyo wa muziki.
r-kelly-death-hoax.jpg


Polisi mjini Chicago wameeleza kuwa, walivyokea simu hiyo ya dharura. Walikimbia upesi hadi nyumbani kwa R. Kelly ambapo walimkuta Mwanasheria wake na kudai kuwa hakuna chochote kilichotokea kwani R. Kelly ni mzima wa afya.
Simu hiyo pia, iliwataarifu polisi kwamba wanawake watano walionyanyaswa kingono na R. Kelly nao wapo kwenye hatari ya kujiua, jambo ambalo liliwafanya polisi wafike kwenye jengo la Trump Tower ambako wanawake hao wamekwaa kwa muda tangu waanze kusikiliza shauri lao mahakamani mjini Chicago.
Hata hivyo, mtandao wa TMZ umeeleza kuwa uliwasiliana na Mwanasheria wa R. Kelly na kuthibitisha kuwa taarifa hizo ni za uongo aliyepiga simu alikuwa na jambo lake binafsi, kwani masaa mawili kabla ya taarifa hizo alikuwa na mteja wake.
Kwa sasa, R. Kelly yupo nje kwa dhamana na anakabiliwa na kesi 10 ikiwemo tuhuma za unyanyasaji wanawake kingono, ambazo zote amekataa.
 
Sio hivyo bro, zengwe hilo kapewa. Wazungu sio watu. Kuna clip ya MJ nashindwa tu kuiweka hapa. Aliongea kweli wakamuua.
Lakini mbona alikuwa anamtafuna Aaliyah? Alikuwa anatembea na Aaliyah akiwa below 14....Kwahiyo Rkelly kupewa kaesi kama hizo inawezekana ikawa kweli na sio kusingiziwa na wazungu,mbona Lil wayne,Birdman,T.I etc hawajasngiziwa?
 
Nimeanza kuona ni namna gani sasa huyu jamaa anatengenezewa shimo la kufikiwa na watu weupe, na hawa ndiyo wapo nyuma ya hili sakata na dhumuni ni kumuonda r Kelly katika ramani ya dunia, hakuna anaejua ukweli ila siku ya mwisho ukweli utasimama na kujitenga na maovu

Super hero daddy
 
Kuna clip moja imesambaa ya hivi karibuni akiwa kwenye tv live show moja alikua akilia na kusema wanataka kumuua hajawahi kufanya hivyo alikua analia sio kidogo kama mtoto mdogo

Super hero daddy
 
Prince, Michael Jackson, bob Marley nk hawa walitengenezewa mfumo wa kuwaondoa kwa kweli rangi nyeusi tunanyanyaswa sana pasipo kupata haki

Super hero daddy
 
Kwa wasanii kufanya ngono na wasichana wadogo ipo duniani kote maana watoto wanapagawa sana!! Tukisema haki itendeke kwa wote wasanii wengi wataishia jela. Hapo kwa R kelly ni mwendelezo wa agenda ya kufuta legacy ya mtu mweusi US
 
Back
Top Bottom