R. Kelly angeazima hekima za Dully Sykes, asingenyanyasa watoto kingono..

I ain't gon stop mpaka huyu dogo wa kidato cha tatu akalie msumari. Jela kitu gani bwana!!?
 
WAZAZI WANABEBA LAWAMA

Docuseries ya Surviving R Kelly inatuma lawama nyingi kwa wazazi. Kwa kutoa uhuru mkubwa kwa watoto wao, kuwaamini bila kufuatilia, ni sababu ya watoto wao kuwa na watu ambao siyo wazuri. Mwisho, yote hayo yanawekwa kwenye neno moja; uzembe!

Mfano, Aaliyah alipelekwa kwa R Kelly na mjomba wake, Barry Henkerson ambaye alikuwa prodyuza mwenzake kwenye studio za Chicago Music Company. Barry alimfahamu vizuri R Kelly, lakini alimwacha awe jirani na Aaliyah na matokeo yake yakashuhudiwa makubwa ya R Kelly kumuoa Aaliyah aliyekuwa na umri wa miaka 15.

Sparkle alifanya kazi na R Kelly tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990. Alikuwa 'back vocalist' wake, vilevile Sparkle aliingiza sauti kwenye nyimbo ambazo R Kelly alizitengeneza akiwa prodyuza. Hata albamu ya Age Ain't Nothing but a Number, Sparkle amejaza sauti karibu nyimbo zote. Sparkle pia alishirikiana na R Kelly katika "Be Careful", ambayo ni bonge la hit. Hivyo, Sparkle anamjua vizuri R Kelly, lakini akakubali kumkabidhi Reshona.

Jerhonda stori yake ni jinsi wazazi wake walivyokuwa wanamwamini na kumpa uhuru kupita kiasi. Alipowaambia anakwenda kwa rafiki yake, wakamkubalia bila kufuatilia, matokeo yake aliangukia kwenye mikono ya R Kelly. Labda ndiyo mnaita malezi ya Kizungu, mimi naita malezi ya uzezeta. Mtoto lazima alindwe mpaka akue.

Katika documentary ya BBC yenye jina, "Sex, Girls, STDs: R Kelly Sex Scandal", wameguswa Lisa Van Allen, Faith Rogers, Kitti Jones, Asante McGee na Joycelyn Savage. Hapa pia nisimulie kuhusu Joycelyn alivyonasa kwa R Kelly, akanogewa na kugoma kurejea kwa wazazi wake.
Joycelyn anatamani kuwa mwanamuziki. Wazazi wa Joycelyn wapo vizuri kimaisha. Jumba la kifahari Atlanta, wanaendesha magari ya bei mbaya. Hawana njaa. Walipoona mtoto wao kipaji chake ni muziki, waliamua kumtafuta R Kelly ili amsaidie mtoto wao kumuingiza kwenye lebo.

Baba wa Joycelyn, Tim Savage na mama yake, Jonjelyn Savage, walipata namba ya R Kelly ambaye alikubali kumpokea binti yao. Faith Rogers alipofanikiwa kuchomoka kwenye jengo la R Kelly, aliwatafuta wazazi wa Joycelyn na kuwaeleza kinachoendelea mjengoni kuwa mtoto wao anashiriki mapenzi ya kikundi na R Kelly. Faith aliwaambia kuwa R Kelly ana maambukizi ya magonjwa ya ngono (STDs). Na alithibitisha hivyo kwa kuwa baada ya kutoroka, alipima na kukutwa na STDs.

Baada ya hapo, wazazi wa Joycelyn walitumia jitihada nyingi kumpata binti yao bila mafanikio. Mamlaka za usalama Marekani, wakiwemo FBI, ziliingilia kati lakini Joycelyn mwenyewe akawa hataki kurudi kwa wazazi wake.

Tunarudi kulekule, wazazi wa Joycelyn walijua kila stori iliyokuwa inaendelea kuhusu R Kelly, lakini waliona uzushi, wakampeleka kwake. Mpaka leo wanaendelea na mapambano ya kumpata bila mafanikio. Mtoto kaganda kwa R Kelly.

Inaendelea..
Huyo mtoto kaganda mpaka leo
 
Mi nachojua mtu mweupe haamini kama mtu mweusi anaweza kupata mafanikio kiuhalali na wakipata "nyufa dhaifu" ndo inakuwa kama hivi. Tutasikia mengi sana. rejea stori za kina Wako Jacko na Mike Tyson.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom