R. Kelly ahofia kupata Virusi vya Corona ndani ya gereza, aomba kuachiwa

marco polo jr

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
363
1,770
Msanii Robert Kelly maarufu Kama R. Kelly ameomba kuachiwa akihofia kupata maambukizi ya virusi vya korona katika Gereza la Metropolitan Correctional Center (MCC) Chicago. Hivi karibuni majaji wa Chicago walionesha nia ya kumuachia kwa dhamana lakini Jaji kutoka New York amesema abaki gerezani.

Katika barua iliyowasilishwa na wakili wake imesema kuna msongamano mkubwa selo pia hakuna sabuni na sanitizer za kutosha kwa wageni wanaokuja kuwaona.

Ikumbukwe, hivi karibuni R. Kelly alikamatwa na kushtakiwa kwa kufunguliwa mashitaka 13 ukiachilia mbali yale 11 ya zamani ambayo Kati ya hayo yapo Hadi miaka 30 jela.
 
Back
Top Bottom