R.I.P Zacharia Hans Poppe: Historia fupi ya Jabari lilotaka Kumpindua Mwalimu Nyerere

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Kama anavyotambulishwa, jina lake ni Zacharia Hans Poppe, ambaye alizaliwa mwaka 1956 mjini Dar es Salaam na kukulia mkoani Iringa.
-
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Zacharia alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako alifikia cheo cha Kapteni
-
Kabla ya kuachishwa kazi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma za uhaini, dhidi ya serikali ya awamu ya kwanza, ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1983.
-
Zachariah Hans Pope wa JWTZ alieshiriki Ktk jaribio la mapinduzi ya kumpindua baba wa Taifa mwl JK Nyerere 1982 akishirikiana na kina kapteni Eugene Maganga, Luteni vitalis Mapunda, Luteni Kajaji Badru, Captain Hatibu Gandhi(Hatty McGee), Luteni Mbogolo, Captain Christopher Kadego, Luteni Pius Lugangila. Maafisa usalama wakiongozwa na comandoo Mabere Nyaucho Marando
-
waliwashambaratisha Kabla hawajawampindua Nyerere. inasemekana baada ya kukamatwa (isipokuwa Pius Lugangila alietoroka) walipelekwa ikulu na Nyerere alimkabidhi Hans Pope bunduki amuue ile awe rais yy Kama alivohitaji, Hans Pope alilia machoz na kugaragara chini huku akiomba msamaha,
-
Nyerere aliwasamehe lkn walifungwa jela maisha, Hans Pope akiwa Gereza kuu Butimba ndie alieanzisha ligi kuu Gerezani huku akiunda timu ya Simba ya Gerezani.
-
waliachiwa 1995 Wkt rais Ally Hassan Mwinyi akimaliza muda wake. Kumbuka Hans Pope babake ni Mgiriki na mamake ni Mhehe wa Ipogoro lringa na ndo maana amekuwa akiidhamini Lipuli FC.

Kama zinavyosema sheria za nchi, mtu aliyehukumiwa kifungo, hana haki ya kugombea wadhifa wowote au kuajiriwa tena, Zacharia naye hakuweza kurejea kazini, badala yake akaamua kujiajiri, kwa kuanzisha miradi yake mwenyewe, ambayo leo ikiwa ni miaka 17 baadaye, miradi hiyo imesimama imara.

HANS POPE NA SIMBA SC:

Alianza kuipenda Simba SC mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1970, akiwa kijana mdogo na zaidi mwenyewe anasema,

Mechi ambayo ilimfanya ajitamke rasmi yeye ni Simba damu ilikuwa dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga Juni 23, mwaka 1973, ambayo Wekundu wa Msimbazi, walishinda 1-0, bao pekee la Haidari Abeid ‘Muchacho’ dakika ya 68.

Mwaka 2012 alijaribu kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Club ya Simba lakini TFF wakalikata jina lake kutokana na historia ya kufungwa kwa kosa la jinai...

Kulingana na hiyo Title ya thread nilitarajia kusoma kwa wingi ishu ya attempted treason Ila bahati mbaya umeishia kusimulia juu juu.

Hapa ingependeza ukajazia nyama jinsi ilivyokuwa, ni lini, simulia mpango mzima ulivyosukwa sio kuishia kuwataja tu, elezea kila kitu mpaka siku anapelekwa Ikulu anapewa bunduki na Mchonga akamwambia haya niue sasa akaishia kulia tu na kuomba msamaha, elezea hata msamaha walipopata instead ya kifo akawapa kifungo Cha maisha na Hadi walipopata msamaha wa Rais 1997 then ndio utusimulie huyu Hans Poppe wa Simba.
 
Ni kosa gani walifanya mpaka kupelekea Zakaria Hans Pope na wenzake kufeli katika jaribio la kumpindua Mwl. JK Nyerere?
 
Kama anavyotambulishwa, jina lake ni Zacharia Hans Poppe, ambaye alizaliwa mwaka 1956 mjini Dar es Salaam na kukulia mkoani Iringa.
-
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Zacharia alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako alifikia cheo cha Kapteni
-
Kabla ya kuachishwa kazi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma za uhaini, dhidi ya serikali ya awamu ya kwanza, ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1983.
-
Zachariah Hans Pope wa JWTZ alieshiriki Ktk jaribio la mapinduzi ya kumpindua baba wa Taifa mwl JK Nyerere 1982 akishirikiana na kina kapteni Eugene Maganga, Luteni vitalis Mapunda, Luteni Kajaji Badru, Captain Hatibu Gandhi(Hatty McGee), Luteni Mbogolo, Captain Christopher Kadego, Luteni Pius Lugangila. Maafisa usalama wakiongozwa na comandoo Mabere Nyaucho Marando
-
waliwashambaratisha Kabla hawajawampindua Nyerere. inasemekana baada ya kukamatwa (isipokuwa Pius Lugangila alietoroka) walipelekwa ikulu na Nyerere alimkabidhi Hans Pope bunduki amuue ile awe rais yy Kama alivohitaji, Hans Pope alilia machoz na kugaragara chini huku akiomba msamaha,
-
Nyerere aliwasamehe lkn walifungwa jela maisha, Hans Pope akiwa Gereza kuu Butimba ndie alieanzisha ligi kuu Gerezani huku akiunda timu ya Simba ya Gerezani.
-
waliachiwa 1995 Wkt rais Ally Hassan Mwinyi akimaliza muda wake. Kumbuka Hans Pope babake ni Mgiriki na mamake ni Mhehe wa Ipogoro lringa na ndo maana amekuwa akiidhamini Lipuli FC.

Kama zinavyosema sheria za nchi, mtu aliyehukumiwa kifungo, hana haki ya kugombea wadhifa wowote au kuajiriwa tena, Zacharia naye hakuweza kurejea kazini, badala yake akaamua kujiajiri, kwa kuanzisha miradi yake mwenyewe, ambayo leo ikiwa ni miaka 17 baadaye, miradi hiyo imesimama imara.

HANS POPE NA SIMBA SC:

Alianza kuipenda Simba SC mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1970, akiwa kijana mdogo na zaidi mwenyewe anasema,

Mechi ambayo ilimfanya ajitamke rasmi yeye ni Simba damu ilikuwa dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga Juni 23, mwaka 1973, ambayo Wekundu wa Msimbazi, walishinda 1-0, bao pekee la Haidari Abeid ‘Muchacho’ dakika ya 68.

Mwaka 2012 alijaribu kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Club ya Simba lakini TFF wakalikata jina lake kutokana na historia ya kufungwa kwa kosa la jinai...

Pius Lugangira a k a Uncle Tom hakuwa mwanajeshi,alikuwa mfanya biashara ambaye mwanzoni alikuwa mwalimu wa Kemia.
 
Back
Top Bottom