R.I.P Rais Magufuli; Ni nyakati mpya na kurasa mpya kwa watanzania

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Mwenyezi Mungu akurehemu katika Safari yako JPM, sisi ni wake na hakika kwake ni marejeo. Umetangulia hatujui inayo fuata ni zamu ya nani kati yangu Mimi na wewe unaye soma mada hii,ila inshallah Allah atufanyie wepesi katika Safari yetu tuondokane na ujasiri na kibri usio na tija kwa jamii yetu.

Pia nimpe pole Mama Rais Samia Suluhu Hassan kwa msiba mzito kwa Taifa kwa kuondokewa na Rais aliyekuwa madarakani. Bila kuisahau family ya JPM chini ya mkewe na watoto, Mungu wetu ni muaminifu na baba wa yatima na mume wa wajane kwa kuwa kila jambo lina sababu hakuna budi kumuomba atufanyie wepesi katika Safari yetu fupi ya Maisha ya hapa duniani.

Wahenga walisema kufa kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi,leo Taifa ndani ya majonzi limempata Rais Mama Samia Suluhu. Watanzania wampokea habari hizi kwa mshindo mkuu kwa kuwa wanaamini kupitia kwake kuwa nchi itasonga mbele.

Uhakisi wa hotuba yake fupi imerudisha imani iliyopotea kwa Watanzania kwa zaidi ya miaka mitano na ushehee,pambazuko jipya kwa nyakati MPYA na ukurasa mpya umefufua ari mpya ya matumaini kutokana na hotuba iliyobeba maudhui na muktadha wa mariadhiano ya kitaifa.

Hakuna wa kuwafuta machozi Watanzania zaidi ya kilongola wetu ikiwa ataishi yale aliyoyaamini. Rais mstaafu J K Kikwete aliwahi kusema "tusirithi uadui,Kama unataka uadui tengeneza madui wako mwenyewe Kama kuna ulazima"

Hakuna asiyejua hali ya kisiasa nchini ilivyokuwa,kwa kuwa Rais kasema tusifukue makaburi hatuna budi kunyamaza kimya kuganga yajayo.

Mama ni mama, muathirika mkuu wa machafuko ni mama,mama kaona machozi ya wengi ndo maana kasema hatuhitaji kunyoosheana kidole zaidi ya kufutana machozi. Tumpe muda afanye kazi,tumpe ushirikiano, ila namshauri kuwa samaki hukunjika ngali mbichi. Mahafidhina ndani ya chama watazame upya walipojikwaa kwa mustakabali wa amani yetu. Tuna vita ya kuisaka amani na kuachana na hali ya uvumilivu tuliyokuwa tumeibakiza.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom