Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,791
Tuko kwenye kipindi cha maombolezo ya kuondokewa na jabali la Afrika na Dunia kwaujumla, mzee Mandela ambaye amefanya mengi ya kutukuka na anastahili yote mwema anayostahili
Kila mahali sasaivi ni habari za mzee huyu, kila mtu anaongea analolifahamu yote mazuri sisikii baya lake hata moja, pengine watu wanaogopa kuwa watazodolewa
Mimi naomba niwe tofauti nao, Madiba alimnyanyasa Winnie Mandela mkewe wa ndoa kwa maneno ya kuambiwa na kusikia
Tukumbuke baada ya madiba kutupwa gerezani kifungo cha maisha, winnie alichukua usukani wa mapambano kwa miaka 27 mpaka Mandela alipoachiwa huru
Pamoja na ukatili mkubwa wa wazungu waliowafanyia watu weusi Mandela alitafuta suluhu na kuwasamehe wote waliomtendea mabaya yeye na waafrika kusini weusi, alitangaza msamaha hadharani
Kitendo dhiki kikapongezwa duniani kote, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua Mdomo wale na kumuuliza kama aliweza kuwasamehe wazungu walifanya kila aina ya ubaya iweje ashindwe kumsamehe mkewake? Hata kufikia kumtaliki?
Hakika Winnie ni binadamu kama wengine ana mapungufu yake na hakika asingeweza kukaa bila mzizi kwa miaka 27 mzee akiwa gerezani, lakini mazuri yake yote yakafunika na baya moja tu akalimwa talaka ya dharau
Winnie ni mwanamke wa shoka aliweza kuhimili na kusimama imara baada ya talaka ile na kashfa zote zilizofuata, ni role model wa wanawake wengi waishio kwenye unyanyapaa wa wanaume wengi
Tunapomkumbuka Madiba tusisahau kosa hili ambalo lilitia doa kubwa kwenye msamaha wake na wazungu