R.I.P Holice Kolimba, Bado nakukumbuka kwa kauli yako.

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,399
320
R.I.P Holice Kolimba,

Ile CCM uliyosema "Imepoteza dira" siku chache kabla ya kifo chako......... Hivi sasa haisomeki kabisa, hata imelipatia tifa viongozi wasio na sifa, wengine wanadaiwa kughushi mpaka vyeti,

Wala hawaji hata hadharani kukanusha kwa kuleta vyeti vyao halali ili kuuzika wauitao uzushi,

Leo CCM tuliyoitegemea inatuadhibu, hapana tena wasemao kwa staha si mkubwa si mdogo,

Taifa ndiyo hiloooo tena wala hatujui laelekea wapi, maana ile CCM uliyosema "imepoteza dira" hakika kwa sasa haina mvuto

Labda uwe katika kilevi, maana vijana "mcharuko" ndiyo wamepewa majukumu, hawajui hata waseme nini wakiwa wapi, na wawe wapi ili kuongea nini,

Ni vurugu mtindo mmoja.
 
Back
Top Bottom