Quran na Biblia zinahimiza kuoga Janaba.

Status
Not open for further replies.
First time nasikia kwamba kuna janaba ya rohoni. Teh, teh,

janaba la rohoni ni dhambi.....hicho ndio kitu kikuu kabisa kinachopaswa kusafishwa,baada ya kifo,mwili huzikwa na kuoza lakini roho itahukumiwa kwa dhambi iliyotenda,hivyo basi tutoe janaba la rohoni.
 
Excuse me, mleta mada kakumbusha watu wote kukoga janaba, wakristo kwa mujibu wa kitabu chao na waislam kwa mujibu wa kitabu chetu.

Na kwa mujibu wa kitabu chetu Quran tukufu hatujaambiwa kuwa tuamini kuwa yesu ni mwana wa Mungu, tumeambiwa tuseme kuwa Mungu ni mmoja, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hakuna kinachofanana nae.

Na wala hatujaambiwa kwenye Quran kuwa yesu ndo mwokozi wetu tumfate yeye ndo tutaenda mbinguni bali tumeambiwa tutende mema na kuacha maovu kwa mujibu wa maamrisho ya Quran na Sunnah za Mtume wetu Muhammad (S. A. W.)

Na hilo la mleta mada kukumbushia iv ni kwa sababu wapo wasojua wajibu wao, kwa kila upande.

Na wapo wanojitoa mshipa wa faham wakafanya kwa makusudi.

mkuu nafikiri hata wewe unapaswa ufikiri zaidi ya hapo. Hivi ni kwa nini mtu anatokwa na manii? ni mazingira gani yanapelekea mwanamume kutokwa na manii? think abt it

Tukija kwenye swala la kifungu cha Walawi 15:16 nafikiri mhusika hakupaswa kunukuu portion ndogo kiasi hicho alipaswa atoke mazingira yalopelekea kifungu hicho. Ila nafikiri hayuko peke yake kwani hata wayahudi wa enzi za Yesu hawakuwaelewa wanafunzi wake walipokuwa wanakula bila kunawa wakinukuu vifungu vinavyosema watu wanawe mikono kabla ya kula.

Mara nyingine ukitumia hila kwenye maandiko ya vitabu vya dini utatengeneza mazingira chonganishi tu.

hebu nimalizie kwa kukupa mfano wa kutumia hila kwenye aya za vitabu vya dini. Quran sehemu moja imesema "Uislam ni pambo la mwenyezi Mungu" kisha mahala pengine imesema "Mapambo yote ni upuuzi mbele za mwenyezi mungu". Kwa kutumia logical implication means UISLAM NI UPUUZI
 
Waislamu kuna kitu kimoja siwaelewi mkuu, inakuwaje mnatumia kwa kuchagua maneno ya Mungu kwenye Biblia?
kwa mfano hapa unatumia andishi la biblia kutuosha Janaba, hii inaonyesha unaiamini, sasa ni vp imani hii inakosekana biblia inaposema Yesu ni mwana wa Mungu?
Imani inakosekanaje pia biblia hiihii inaposema kuwa mtu hatafika mbinguni bila kumkiri Yesu kuwa ni bwana na mwokozi wake?
msaada tafadhali!

Aya nyingi za Biblia zinasema Yesu katumwa na Mungu, Yesu ni Mtume wa Mungu.

Tadhali soma aya hizi kisha tafakari,

Biblia inasema ...wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli,nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma. (Yohana17:3)

Huyu ndio Mungu (Mungu Mmoja tu), soma aya hizi,;

Biblia inasema , Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina. (1 Timotheo 6:16)

Quran Inasema, Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari. (Quran 6:103)

Quran Inasema, Mwenyezi Mungu, hakuna mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa yote milele. (Quran 3:2)

Quran Inasema, Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo. Hapana mungu ila Yeye, Mwenye nguvu na Mwenye hikima. (Quran 3:6)

Quran Inasema, Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. (Quran 3:18)

Quran inasema, Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Mabwana badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu. (Quran 3:64)
 
mkuu nafikiri hata wewe unapaswa ufikiri zaidi ya hapo. Hivi ni kwa nini mtu anatokwa na manii? ni mazingira gani yanapelekea mwanamume kutokwa na manii? think abt it

Tukija kwenye swala la kifungu cha Walawi 15:16 nafikiri mhusika hakupaswa kunukuu portion ndogo kiasi hicho alipaswa atoke mazingira yalopelekea kifungu hicho. Ila nafikiri hayuko peke yake kwani hata wayahudi wa enzi za Yesu hawakuwaelewa wanafunzi wake walipokuwa wanakula bila kunawa wakinukuu vifungu vinavyosema watu wanawe mikono kabla ya kula.

Mara nyingine ukitumia hila kwenye maandiko ya vitabu vya dini utatengeneza mazingira chonganishi tu.

hebu nimalizie kwa kukupa mfano wa kutumia hila kwenye aya za vitabu vya dini. Quran sehemu moja imesema "Uislam ni pambo la mwenyezi Mungu" kisha mahala pengine imesema "Mapambo yote ni upuuzi mbele za mwenyezi mungu". Kwa kutumia logical implication means UISLAM NI UPUUZI

duh..hapo andaa helmet wasubiri wanakuja
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom