QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEASON 7: SEHEMU YA 2


Kwa zaidi ya dakika tatu sasa,
rais Ernest Mkasa alikuwa
ameegemea ukuta akionekana
kuchanganyikiwa kwa ile simu
aliyopigiwa na mke wake
Agatha.Alihisi shati likiloana kwa
kijasho kilichokuwa kinamtoka
“ Bado siamini hiki
nilichokisikia.” Akawaza
“ Imewezekanaje? Akajiuliza
“ Sauti ni ile ile ya
Agatha.Kama kweli ni yeye
imetokeaje hadi asiwepo ndani ya
ule ukumbi kama tulivyokuwa
tumekubaliana? Kama alikuwemo
ukumbini ameokoka vipi? Na kama
hakuwepo ukumbini ni kwa nini
hakuwepo? Je kuna kitu chochote
alikwisha kihisi? Akajiuliza na
kukuna kichwa.
“ Naona kichwa changu
kinazidi kulemewa kwa mzigo
mzito wa mawazo.Imewezekanaje
Agatha asiwepo ukumbini wakati
yeye ndiye aliyekuwa mstari wa
mbele kukusanya wenzake wafike
pale ukumbini? Isitoshe yeye ni
mmoja wa viongozi wa Alberto’s
hapa nchini alitakiwa kuwepo mle
ndani.Kuna kitu chochote
alikigundua kuhusiana na mpango
wangu?
“ I’m not dead mr President.I’m
still alive.”
Maneno haya ya Agatha
yakaendelea kuzunguka kichwani
kwake
“ kwa maneno haya mni wazi
ananiambia kwamba
nilichokikusudia kwake
hakijatimia na bado mzima.Kama
kweli ni yeye this is going to be a
big war.Lazima atakuwa
anafahamu kuhusu mpango
wangu.Kama tayari anafahamu
nani kamueleza? Mtu pekee
aliyekuwa anafahamu kuhusiana
na mpango wangu ni Jenerali
Lameck na wengine ni wale
makamanda na marubani
waliopewa amri ya kuyalipua
majengo yale mawili ambao nina
imani walikula kiapo cha
kutokusema chochote.Agatha
amefahamu vipi mpango huu?
Akajiuliza rais
“ Just wait for my call mr
president anytime soon”
Maneno haya ya mwisho
aliyoyaongea Agatha kabla ya
kukata simu yalizidi
kumchanganya zaidi Ernest
“ Alimaanisha nini aliposema
kwamba nitegemee simu yake
muda si mrefu? Anataka
kuniambia jambo gani?
Akaendelea kujiuliza
“ Tayari nilianza kushangilia
mpango wangu wa kuwaondoa
Alberto’s kufanikiwa lakini simu
hii ya Agatha imetibua kila
kitu.Amewezaje kukwepa janga
hili? Huyu mwanamke ni kikwazo
kikubwa sana kwangu kwa
sasa.Idadi ya watu ninaotakiwa
kuwashughulikia kwa haraka
inazidi kuongezeka.Kwanza
walikuwa ni Austin na wenzake na
sasa ameongezeka
Agatha.Ameichanganya akili yangu
na sijui nifanye nini” akawaza na
mara akakumbuka kuwa alikuwa
na Jeneral Lameck akamtaka
waelekee katika chumba cha
maongezi ya faragha.Rais akavua
koti na shati lake lililoa jasho
“Pole mheshimiwa
rais.Mambo yanazidi kuwa
magumu lakini usihofu
tutayamaliza moja baada ya
lingine.” Akasema Lameck
“ Ahsante Lameck.” Akasema
rais na kumtazama Lameck
“ Lameck kwa silimia tisini na
saba naweza kusema kwamba
mpango wetu umefanikiwa na kile
tulichokuwa tumekilenga
tumekipata .Idadi kubwa ya
Alberto’s kama si wote wamefariki
dunia,na hata wabunge wafuasi
wao karibu wote wamefariki
dunia.Tumechafuka kwa damu zao
lakini ni ushindi kwetu na kwa
nchi pia.Pamoja na ushindi huo
kumejitokeza baadhi ya matatizo
.Kwanza ni Yasmin ambaye tayari
tuna uhakika kwamba yuko ndani
ya jiji la Dar es salaam.Huyu ana
nyaraka ya muhimu sana ambayo
lazima tuipate kwa haraka.Yasmin
yuko na akina Austin na lazima
atawaeleza kila kitu na anaweza
akawapatia hati hiyo ili wampatie
mwanae.Kama hilo likitokea
tutakuwa katika matatizo
makubwa.Wale vijana wanaweza
wakaharibu mafanikio haya yote
tuliyoyapata.Ni vijana hatari sana
kwetu ambao kwa kila namna
itakayowezekana lazima kabla ya
jua kuzama siku ya kesho
tuwapate.” Akanyamaza na kuuma
meno kwa hasira.
“ Sikutegemea kabisa kama
nitaingia katika vita na hawa
vijana.Niliwaamini nikawapa kazi
wanifanyie na sasa wamegeuka
adui zangu.” akasema rais
“ Ukiachana na hao vijana
kuna jambo lingine limetokea
muda mfupi uliopita na ambalo
limenifanya mwili wote uloe jasho.
Lameck tuna tatizo kubwa”
akasema rais na kuvuta pumzi
ndefu
“ Tatizo gani limejitokeza
mzee? Akauliza Lameck.
“ Agatha is still alive” akasema
na kumshangaza Lameck
“ Agatha yupi mzee? Akauliza
Lameck
“ Agatha mke wangu”
“ What ? Lameck akapatwa na
mshangao mkubwa
“ Imewezekanaje?
Amenusurika vipi? Hakuwepo
katika ile hoteli? Akauliza Lameck
“ Hata mimi bado najiuliza
maswali kama hayo na sifahamu
nini kimetokea hadi akanusurika”
akasema rais
“ Mzee umeajuaje kama kweli
yuko hai?
“ Amenipigia simu muda si
mrefu nilipomaliza kuzungumza
na Habib.Tumeongea kwa muda
mfupi sana na alichokisema ni
kwamba amenipigia kunijulisha
kuwa yuko hai na mwisho akasema
kwamba nisubiri simu yake hivi
karibuni.Lameck
nimechanganyikiwa.Agatha ni mtu
ambaye nilihitaji sana awepo
katika orodha ya watakaofariki
lakini imeshindikana.Maneno yake
yanaonyesha wazi kwamba
anafahamu kuhusu ule mpango
wetu Kama ni kweli ameufahamu
mpango wetu sijui nini
kitatokea.Sifahamu atataka nini
akipiga hiyo simu aliyoahidi
kupiga”akasema rais
“Mzee una uhakika kuwa
uliyeongea naye ni Agatha?
Haiwezekani mtu mwingine
akajitokeza akaiga sauti akajifanya
kuwa yeye ni Agatha? Akauliza
Lameck
“ Lameck ninamfahamu mke
wangu vizuri.Nimeishi naye kwa
miaka mingi kwa hiyo naifahamu
vyema sauti yake hata nikiisikia
nikiwa usingizi.Niliyeongea naye ni
Agatha” akasema rais
“ Umejaribu tena kumpigia
kwa kutumia namba hizo za simu
alizokupigia?akauliza Lameck
“ Hapana sijajaribu” akasema
rais na kupiga zile namba za simu
alizotumia mke wake lakini
akapewa angalizo kwamba namba
zile hazikuwa sahihi .Akazidi
kuchanganyikiwa.
“ Lameck namfahamu huyu
mwanamke ni mjanja sana na
hawezi kutumia namba ya simu
ambayo itatuwezesha kumpata
kirahisi .Nina hakika lazima kuna
kitu anakiandaa kuja nacho.”
“ Mheshimiwa rais suala hili
linanichanganya sana.Unadai
lazima atakuwa anafahamu
kuhusu mipango yetu ,kama ni
kweli anafahamu,nani kampa
habari hizi? Mpango huu
umepangwa na watu wawili tu
mimi na wewe,umevuja vipi?
Akauliza Lameck
“ Hilo ni swali ambalo hata
mimi nimejiuliza sana.Nahisi
inawezekana mmoja wa wale
marubani au makamanda
uliowashirikisha amevujisha siri
hii” akasema rais
“ Hapana mzee.Nina wamini
sana vijana wangu na wamekula
kiapo cha kutokusema chochote
kuhusiana na jambo hili.Kama
Agatha amefahamu mpango wetu
lazima kuna tatizo kubwa mzee.”
Akasema lameck na ukimya mfupi
ukapita.
‘”Kwa hiyo tunafanya nini
mzee? Mambo yameanza
kutubadilikia na tunapaswa
kuanza kuyatafutia ufumbuzi wa
haraka kuanzia sasa na kabla jua
halijatoka tayari tuwe na
mwangaza wa tunakoelekea ili
mambo yasiharibike” akasema
Lameck
“ Nataka Silvanus arejee dar es
salaam haraka sana ili
alishughulikie hili.Nguvu kubwa
kwa usiku huu inatakiwa
kuelekezwa kuwatafuta Agatha na
akina Austin ambao najua kwa
msaada wa Monica tunaweza
kuwapata kirahisi.Tatizo liko kwa
Agatha namna ya kumpata .Silva
nataka atumie rasilimali zote
zilizopo katika idara yake kumpata
Agatha.” Akasema rais.Lameck
akawaza kitu halafu akasema
“ Mzee nina wazo moja”
“ Sema Lameck nakusikia
“ Mambo mapya yanazidi
kuibuka moja baada ya
lingine.Alikuwa ni
Yasmin,wakaongezeka akina
Austin na sasa ameongezeka
Agatha na mpaka sasa hatuna
fununu zozote watu hawa wako
wapi ingawa wako hapa hapa Dar
es salaam .Nina wasi wasi
tunaweza tusifanikiwe kuwapata
kwa muda tunaotaka na kadiri
tutakavyozidi kuchelewa tunaweza
kujikuta kila kitu tulichokifanya
kikaharibika na tukashindwa
kufikia malengo yetu.Wazo langu
kwa nini usitafute muafaka na
akina Austin?
“Muafaka?! Rais akastuka
“ Ndiyo mzee.Kwa nini
usiwaite wale jaama ukazungumza
nao ukawaeleza ukweli wote ?
Waeleze kila kitu kilichotokea na
kwa nini tumefanya vile.Mwisho
waombe mshirikiane katika
kuitafuta tena hati ile ya
muungano.Wewe na Austin
mliyaanzisha mapambano dhidi ya
Alberto’s nina uhakika nyote lengo
lenu lilikuwa moja kuwaondoa
kabisa Alberto’s hapa nchini na
nina uhakika lazima Austin
atakubaliana na hiki
tulichokifanya.Nakushauri mzee
ufanye hivi angali bado mapema
na lengo kubwa la kukushauri
ufanye hivi ni kupunguza idadi ya
maadui tunaotakiwa
kuwapata.Nina uhakika mkubwa
kama tukiwashirikisha hawa akina
Austin basi uwezekano wa kuipata
hati ya muungano ni mkubwa
sana.Tukimalizana na hawa jamaa
tutabakiwa na mtu mmoja tu
ambaye ni Agatha.Huyu tutatumia
nguvu kubwa kumtafuta na
tutampata kirahisi.” Akasema
Lameck.Rais akainamisha kichwa
akazama katika mawazo halafu
akamtazama Lameck na kusema
“Lameck wazo lako ni zuri
lakini halitaweza kufaa kwa
sasa.Tumechelewa tayari.Kama ni
kuwashirikisha tulitakiwa
kuwashirikisha kuanzia
mwanzo.Mimi na wao tulikuwa na
mipango ya kuwafagia Alberto’s
hapa nchini lakini niliwageuka na
kuja na mpango huu wa kulipua
hoteli na bunge mpango ambao
umefanikiwa kuwaondoa Alberto’s
wengi kwa mara moja.Tayari uadui
umeingia kati yetu.Wamekwisha
gundua kwamba siko upande wao
kwa hiyo haitawezekana
kushirikiana nao katika jambo
lolote.Kitu pekee cha kufanya hapa
ni kuwatafuta kokote waliko na
ninatoa amri ya kuwapiga risasi
wote baada ya kuwa tumeipata
hati ya muungano watakayokuwa
wamepewa na Yasmin,kwani lengo
la kwenda kumchukua Zanzibar ni
ili k uipata hati hiyo” Akasema rais
na kumpigia simu Silvanus
Kiwembe akamtaka arejee Dar es
salama haraka iwezekanavyo kuna
jambo la dharura limejitokeza
“ Lameck nenda kashughulikie
ule mpango wa kufanya
mashambulio katika kambi za
Alshabaab.Jukumu hili la
kuwatafuta Agatha na akina Austin
nitampa Silva ambaye atawasili
muda si mrefu kutoka
Zanzibar.Kwa sasa ngoja
nikapumzishe kichwa changu
nahisi kinaweza kupasuka kwa
mawazo mengi
niliyonayo.Utanijulisha kila kitu
kitakavyokwenda” akasema rais
na kuelekea chumbani kwake.
“ Mambo yamekwenda vizuri
sana ila hapa mwishoni kuna
mdudu ameingia na anataka
kuharibu kila kitu.Hata hivyo
nashukuru kwamba kwa asilimia
kubwa nililolitaka
limetokea.Alberto’s karibu wote
hapa nchini nimewafyeka.Natumai
kesho asubuhi nitapata orodha ya
watu wote walioteketea ili
nitathmini mafanikio .Ninaamini
tayari nimeuzika mtandao wa
Alberto’s hapa nchini.Kwa sasa
nguvu natakiwa kuielekeza katika
kukabiliana na yale yaliyojitokeza
na yanayoendelea kujitokeza
baada ya mashambulio haya na
kikubwa ni kuwapata kwanza
akina Austin ambao nina uhakika
Yasmin atakuwa amewaeleza kila
kitu kilichotokea.Austin ni kijana
mwenye akili sana kwani alitaka
kwanza nifahamu kama Monica ni
mwanangu na alipofanikiwa katika
hilo akamfuata Monica akamtaka
awasiliane nami akijua wazi
kwamba siwezi kumkatalia Monica
jambo lolote.How could I be such a
fool?Kwa nini nimekubali
kuchezewa akili na kijana mdogo
kama yule? Akajiuliza huku akivua
shati na kujilaza kitandani
“ Anyway yamekwisha tokea
na kilichobaki kwa sasa ni
kuhakikisha kwa gharama zozote
zile ninaipata hati ya muungano na
kuirejesha mahala pake na hii
itapatikana endapo nitampata
Yasmin na akina Austin.Wale ni
vijana wadogo siwezi kushindwa
kuwpata wakati majeshi yote yako
chini yangu.Nitatumia kila nguvu
niliyonayo ili kuwapata akina
Austin kabla ya jua kuzama hiyo
kesho.Jiji la Dar kesho lazima
lifungwe hakuna kuingia wala
kutoka mtu hadi Austin na kundi
lake wapatikane.Najuta kwa nini
nilimtumiahuyu kijana.Nilimuona
wa thamani kubwa kwangu lakini
sasa amegeuka mzigo na adui
mkubwa.Lazima nimmalize haraka
kwani nikichelewa
atanimaliza.Kuhusu Alshabaab
nitamalizana nao .Nitazungumza
nao ili niwapatie kitu kingine
badala ya ile hati” akawaza rais na
mara akainuka na kukaa
“ Ni vipi endapo sintafanikiwa
kuipata tena hati ya muungano?
Akawaza na kukumbuka kitu
“ Mzee Pantaleo amekutwa
amejinyonga.Vijana wamefanya
kazi nzuri.Huyu angekuwa
kikwazo kikubwa kwangu kwani ni
yeye pekee aliyefahamu kuwa hati
ile iko kwangu.Endapo
sintafanikiwakuipata hati ile tayari
ninacho kitu cha kusema kwamba
Pantaleo ameshirikiana na watu
wakaiba hati ile ikulu na kuipeleka
mahala kusikojulikana na baada ya
kuona kwamba atagundulika
akaamua kujinyonga.Ninaamini
wananchi wataelewa.Isitoshe bado
tutaendelea kuwa taifa kwani kuna
hati nyingine kama ile iko umoja
wa mataifa kwa hiyo bado
tutaendelea kutambulika kama
taifa la Tanzania.Pamoja na hayo
lazima nihakikishe kwamba hati
inapatikana kwa gharama zozote.”
Akawaza na kuinamisha kichwa
“ Agatha!! Akasema kwa sauti
ndogo
“ Huyu naye ameibuka na
kufanya mambo kuwa magumu
zaidi.Nashindwa kupata jibu
ameokoka vipi? Kwa nini
hakuwemo katika kikao kile? Je
tayari alifahamu kuhusu mpango
niliokuwa nimeupanga dhidi
yao?Huyu mwananke kuendelea
kuwa hai ni hatari kubwa kwangu.
Najuta kwa nini sikummaliza
wakati ninayo nafasi.Ukiacha huyu
kuna mwingine ambaye ni hatari
zaidi pia Mukasha.Huyu naye
anatakiwa atafutwe kwa udi na
uvumba hadi
apatikane.Nikifanikiwa
kuwamaliza hawa nitakuwa
nimefunga kazi na nchi itabaki
salama.Nina hakika ndani ya wiki
hii lazima niwe nimefanikiwa
kuwapata wote. Mukasha ,Agatha
na akina Austin.Kwa sasa ngoja
nipumzike walau kwa saa moja
.Imekuwa ni siku ndefu sana yenye
mambo mengi.Sijapata wasaa wa
kupumzika toka jana na siku ya leo
itakuwa ndefu na ngumu sana
kuzidi jana.” Akawaza rais na
kujilaza kitandani
 
SEASON 7: SEHEMU YA 3

Mlio wa saa ulimstua Monica
toka katika usingizi wa mang’amu
ng’amu alioupata .Akatazama saa
ilikuwa ni saa kumi na moja kamili
za alfajiri.
“ Tayari kumeanza
kupambazuka.” Akasema na
kuinuka akakaa kitandani na
kushika kichwa
“ Mwili wote bado
unanitetemeka nikikumbuka yale
mambo ya jana usiku.Ni moja kati
ya tukio la hatari sana kuwahi
kunitokea katika maisha
yangu.Nashukuru Mungu nilirejea
salama.Austin alifanya kitu kibaya
na cha hatari sana kuipeleka ndege
ikatue katika daraja.Najiuliza ni
vipi endapo wakati wa kutua
tungegongana na gari? Ni vipi
iwapo rubani angekosea uelekeo
na kugonga daraja? Ungekuwa
ndio mwisho wetu.” Mwili wote
ukamsisimka alipolikumbuka
tukio lile.
“Siamini kama Austin
niliyemshuhudia jana usiku ni yule
Austin niliyemfahamu siku chache
zilizopita.Austin ninayemfahamu
ni kijana mpole,mcheshi na
mwenye uso uliojaa tabasamu
wakati wote kiasi kwamba ilibaki
kidogo nijipeleke kwake kwa
namna alivyonivutia.Alikuwa ni
kijana mwenye sifa lukuki lakini
huyu niliyemuona jana usiku
hafanani kabisa na Austin yule
ninayemfahamu.Najaribu
kujilazimisha kuamini labda ile
ilikuwa ni ndoto lakini ukweli
utabaki pale pale kuwa ile si ndoto
bali ni kitu cha kweli kimetokea na
Austin yule aliyehatarisha maisha
yangu jana usiku ni Austin yule
yule ambaye siku kadhaa zilizopita
nilimuona ni kijana mzuri pengine
kuliko wote.Nilijidanganya sana
kwa kubabaika na umbo la nje bila
kufahamu undani wake.” Akawaza
na kuinuka akaenda dirishani
akachungulia nje halafu akarejea
tena kitandani akakaa
“Nashukuru rais
alinihakikishia kwamba suala lile
halitaendelea tena lakini kuna
swali moja ambalo bado sijalipatia
majibu ni je Austi ni nani hasa?
Kwa mambo niliyoyaona
akiyafanya jana nashawishika
kuamini kwamba kuna uwezekano
mkubwa akawa ni mpelelezi.Kama
ni mpelelezi alikuja kwangu
kutafuta kitu gani? Alikuwa
ananipeleleza? Akajiuliza
“ Ni vigumu sana kupata jibu
la swali hili.Kuna watu wawili tu
ambao wanaweza wakanipa
majibu ya swali hili ambao ni
Austin mwenyewe na rais.Hawa
wanafahamiana vizuri lakini
ingekuwa vyema endapo
ningeweza kumpata Austin ili
anieleze ukweli yeye ni nani na
alikuwa anatafuta nini kwangu?
Naamini kabisa kwamba kuna kitu
alikuwa anakitafuta kwangu na
ndiyo maana akaja kwa kisingizio
cha kutaka kushirikiana nami
katika miradi ya kijamii.Dah !
ninajiona mrahisi sana kwa
kumuamini Austin kwa haraka
namna ile.Sikuwa na shaka naye
hata kidogo kwani alikuwa na
vigezo vyote vya kumuamini”
Akawaza na kukumbuka mara ya
kwanza kukutana na Austin .
“ Rais na Austin ni watu wa
karibu sana lakini jana
alinishangaza pale aliponitaka
nimsaidie kumpata Austin.Kwa
nini anitumie mimi wakati yeye ni
mtu wake wa karibu na anaweza
akawasiliana naye akafahamu
mahala aliko? Ninatakiwa kuwa
makini sana hapa kwani ninaweza
kuingizwa tena katika matatizo
makubwa.Tayari Austin alikwisha
niingiza katika tatizo jana usiku
sitaki tena kuingia katika tatizo
lingine.Kama ni kutafutana basi
watafutane wao wenyewe bila
kunihusisha mimi.” Akashika
kichwa baada ya kukumbuka kitu
“ Lakini nilimuahidi rais
kwamba nitamsaidia kumpata
Austin.Tulipanga kwamba
nimpigie simu Austin halafu
nipange kuonana naye kisha
nimjulishe rais atume vijana wake
wakamchukue Austin.Jana usiku
wakati nikizungumza na rais pale
ikulu kichwa changu hakikuwa
kikifikiri sawa sawa.Tukio la usiku
ule lilinichanganya sana na sikujua
nilichokuwa nakiongea na ndiyo
maana nikamkubalia rais kwamba
nitamsaidia kumpata Austin.Usiku
nimetafakari sana na nimegundua
nilifanya kosa kubwa kumkubalia
rais kuwa nitamsaidia kumpata
Austin.Rais ana namna nyingi za
kufanya kumpata Austin,halafu
wawili hawa ni watu wa karibu
kwa nini wanihusishe katika
mambo nisiyoyafahamu? akawaza
na kwenda tena kusimama
dirishani akitazama nje namna
kunavyopambazuka
“ Hapana sintafanya kitu
anachokitaka rais.Nitajiingiza
katika hatari bila kujua.Austin
niliyemshuhudia jana ni mtu
hatari sana.Akigundua kwamba ni
mimi ndiye niliyemsaidia rais
anaweza akaniletea matatizo
makubwa.Yule si mtu wa kuingia
naye katika matatizo.Isitoshe jana
aliniambia kwamba kuna kitu
anataka kunieleza kinachonihusu
mimi lakini kwa hasira nilizokuwa
nazo sikutaka kumsikia na
kumtolea maneo makali.”akawaza
na kukumbuka namna Austin
alivyosisitiza kwamba ana jambo
la muhimu la kumueleza
“ Monica I promised to tell you
something very important about
you.Please Monica it’s important”
Maneo haya ya Ausytin
yakamjia kichwani
“ Kuna kitu Austin anacho
anataka kunieleza lakini sikumpa
nafasi kutokana na hasira
nilizokuwa nazo.Yawezekana ni
kitu muhimu ambacho sikifahamu
na kinachoweza
kunisaidia.Natakiwa kutafuta
namna ya kuonana naye bila ya
rais kufahamu .Niliapa kutooana
naye tena lakini sasa inanilazimu
kumtafuta ili nifahamu alichotaka
kunieleza ni kitu gani.I have to find
a way to meet him” akakaa
kitandani akawaza kwa muda
halafu akatoka na kuelekea katika
chumba cha wazazi wake akagonga
mlango.Aliyeufungua mlango ni
mzee Benedict
“Monica !! akasema Ben
“Shikamoo baba”
“ Marahaba Monica.Pole kwa
matatizo.Mama yako alinieleza
kwamba ulipata matatizo jana
usiku.”
“ Ndiyo baba kuna tatizo
nilipata jana lakini tayari
limekwisha”
“Karibu unieleze ni tatizo gani
limekupata jana kwani hatukupata
usingizi kwa wasi wasi tuliokuwa
nao juu yako” akasema Mzee Ben
na mara Janet mke wake akaamka
baada ya kusikia Ben
anazungumza na Monica
.Waliokwenda katika sebule ya
Ben na mke wake iliyo pembeni
mwa chumba chao.
“ Monica wewe ni mboni yetu
ya jicho.Taarifa kwamba umepata
matatizo hadi ukaitwa ikulu
zimetustua mno na hasa kwa
wakati huu ambao kuna mipango
mikubwa inaendelea juu yako
.Hebu tujuze nini kimetokea jana?
Akauliza mzee Ben.
“ Baba na mama kwanza
nawaombeni samahani sana kwa
kuwastueni hadi mkakosa
usingizi.Ni kweli jana kuna kitu
kilitokea lakini hata mimi sikuwa
nimetegemea kitu kama kile
kitokee .Naombeni mnipe muda
nitawaeleza kila kitu kilichotokea
ila naomba niwatoe wasiwasi
wazazi wangu kwamba tatizo lile
likimekwisha na msiwe na hofu
yoyote” akasema Monica
“ Monica japokuwa unajitahidi
kutuondoa hofu lakini hatuwezi
kuwa na amani mioyoni mwetu
kama hatutafahamu ni tatizo gani
lilikupata na lilikwisha vipi.Hata
hivyo bado tutaendelea kusubiri
hadi hapo utakapokuwa tayari
kutueleza ila nakuomba Monica
endapo kutatokea tatizo lolote
muda wowote sisi tuwe wa kwanza
kupata taarifa.Haipendezi malaika
wetu unapatwa na matatizo tena
usiku halafu sisi wazazi wako
hatujui chochote.”akasema Ben
“ Ahsante sana baba kwa
kunielewa .Nisameheni vile vile
kwa kuwastueni asubuhi hii”
akasema Monica
“ Bila samahani
Monica.Hujatusumbua kwani hii ni
faraja kwetu kukuona
.Tumeisubiri kwa hamu kubwa
asubuhi ifike haraka ili tukuone na
kuhakikisha kwamba uko salama .”
akasema Ben
“ Nashukuru baba.Ahsanteni
kwa upendo wenu wa hali ya juu
ambao hauna kipimo.Hata hivyo
nimekuja kwenu asubuhi hii
nahitaji msaada wenu.” Akasema
Monca
“ Sema Monica.Unahiaji
tukusaidie jambo gani? Akauliza
Ben
“ Kuna mtu mmoja nahitaji
kuonana naye.Nahitaji sana
kuonana naye asubuhi hii lakini
sitaki kutumia simu yangu
kuwasiliana naye na wala sitaki
mtu yeyote afahamu kama
nimeonana naye.Nataka baba
umpigie simu kwa kutumia simu
yako na kisha mimi nitazungumza
naye” akasema Monica.Ben na
Janet wakatazamana
“ Monica kuna tatizo gani hasa
linaloendelea?Japokuwa
umetuahdi kwamba utatueleza
pale utakapokuwa tayari lakini
tunaomba utueleze japo kwa ufupi
tu nini hasa kinachoendelea?
Akasema Ben
“ Baba nitawaeleza kila kitu
lakini naomba mnipe muda.Kwa
sasa naombeni mnisaidie hilo
nililowaomba .Ni muhimu sana”
akasema Monica na kumpa baba
yake namba za Austin akampigia
“ Namba hizi hazipatikani.”
Akasema Ben.Monica akakuna
kichwa na mara akakumbuka
kitu.Alikuwa na namba za simu za
Amarachi akampa baba yake
akampigia .Simu ya Amarachi
ikaita Ben akampa Monica simu
“ Hallow” akasema Amarachi
baada ya kupokea simu.
“ Amarachi.It’s me Monica”
akasema
“ Monica !! akasema Amarachi
kwa furaha.
“ Amarachi naomba msaada
wako tafadhali.Nahitaji
kuzungumza na Austin asubuhi
hii.Ni muhimu sana” akasema
Monica
“ Sawa Monica naomba unipe
dakika moja nimpelekee simu
chumbani kwake” akasema
Amarachi na kuelekea katika
chumba alicholala Austin na
Marcelo.Bila hata kugonga mlango
akakinyonga kitasa na kuingia
ndani.Tayari Austin alikwisha
amka kitambo na alikuwa amekaa
kitandani.Akashangaa kumuona
Amarachi alivyoingia mle
chumbani.Kwa kasi ya ajabu
akainyakua bastora iliyokuwa
pembeni
“Amarachi kuna tatizo lolote?
Akauliza Austin
“ Austin ongea na Monica.”
Akasema Amarachi na kumpa
Austin simu.
“ Hallow Monica” akasema
Austin
“ Austin habari za
asubuhi?Samahani kwa
kukusumbua asubuhi namna hii”
“ Hakuna tatizo Monica .Vipi
hali yako?
“ Naendelea vizuri .Austin
samahani kwa maneno
niliyokutamkia jana.Nilikuwa na
hasira sana na woga mwingi
kutokana na mambo yaliyotokea.”
“ Usijali Monica.Hata mimi
nilifahamu ni hasira tu” akasema
Austin
“ Ahsante Austin.Nahitaji
kuonana nawe asubuhi hii kama
utakuwa na nafasi .Ni muhimu
sana.Kuna mambo nataka
tuzungumze”akasema Monica na
sura ya Austin ikajenga tabasamu
“ Tuonane wapi Monica?
Nikufuate nyumbani kwako?
“ Hapana siko nyumbani
kwangu.Niko hapa kwa wazazi
wangu.Nitakuelekeza ili uje
unikute hapa” akasema Monica na
kumuelekeza Austin nyumbani
kwa wazazi wake kisha wakaagana
“ Monica anahitaji kuonana
nami asubuhi hii.Amarachi jiandae
tunakwenda wote.Job atabaki hapa
” Austin akamwambia Amarachi na
kuanza kujiandaa .
“ Job tafadhali kuwa makini
sana na huyu Yasmin.Ni mtu hatari
” Austin akamwambi Job wakati
yeye na Amarachi wakiingia garini
na kuondoka kuelekea nyumbani
kwa mzee Benedict Mwamsole
kuonana na Monica
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom