Quattara aongoza ivory coast akiwa hotelini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Quattara aongoza ivory coast akiwa hotelini

Discussion in 'International Forum' started by The Finest, Dec 14, 2010.

 1. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Alassane Quttara, ambaye alitangazwa na tume ya uchaguzi ya Ivory Coast kuwa mshindi wa mbio za kiti cha rais, anaongoza taifa hilo akiwa kwenye chumba cha hoteli chenye uwezo wa kuhifadhi dawati moja kutokana na rais anayemaliza muda wake kung'ang'ania madaraka ikulu.

  Utawala wa Quttara umechukua ofisi ya meneja wa hoteli amabyo ina mashine na faksi inayotumika kuwasiliana na balozi za nje, viwanja vya mchezo wa gofu vilivyo jirani na hoteli hiyo vinaweza kugeuka kuwa kambi ya askari walioasi kutoka kwenye jeshi linalomtii gbagbo.

  My take:Hali hii itaendelea hadi lini huu ung'ang'aniaji wa madaraka kwa marais wa afrika.
   
 2. a

  asagulaga Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  He! Gbagbo anang'ang'ania madaraka kwa kuwa anajua atasaidiwa na viongozi wapendao suluhu nyepesi kwa kuunda serkali ya umoja wa kitaifa. Demokrasia ya namna hii Afrika haitufai. Kina Gbagbo wakubali matokeo, waheshimu maamuzi ya wapiga kura.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hapo Gbagbo kutoka madarakani hadi aondolewe kwa mtutu vinginevyo sioni akiaachia madaraka kirahisi pia kiburi alichonacho Gbagbo ni uswahiba alio nao na mmoja wa washauri wake wa karibu anayeongoza Baraza la Katiba aliyepindua matokeo jimbo aliloongoza Quttara na kumtangaza Gbagbo na kumpa ushindi rafiki yake, amekataa wito wa kung'oka madarakani kutoka kwa marafiki zake wa karibu, wanasiasa maarafu na akaenda mbali zaidi kukataa kupokea simu aliyopigiwa na Rais wa Marekani Barack Obama
   
 4. Avocado

  Avocado Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hii ni laana kwa waafrika au ni tamaa tu ya madaraka,kumbe hakuna haja ya kupoteza pesa na muda mwingi kwa ajili ya uchaguzi.Tena hawa ndugu wamefanya uchaguzi mara mbili,hiyo pesa si ingefanya kazi nyingine za kuinua maisha ya wana Ivory coast
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Viongozi wataanza kuwafikiria wananchi saa ngapi wakati wanataka kuneemesha matumbo yao kwanza si ajabu ukasikia serikali ya mseto maana ndio imeishakuwa dili siku hizi Afrika yaani kwa sasa Ivory Coast inaongozwa na marais wawili madaraka matamu sana na muda wako ukiishia unaachia huku roho inakuuma
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwingine tunaye hapa hapa kwetu ....
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  there is always a simple solutions kwa mtu kama Gbagbo - one bullet in his head or poisoning him (sorry)
   
 8. JS

  JS JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Watu wanangángánia madaraka utadhani watazikwa nayo.....selfish personalities....aaarggghhhhhh:redfaces::redfaces::redfaces:
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hilo linaweza kutokea kwa nchi kama Ivory Coast hasa pale majeshi yanayokutii ghafla yanakugeuka
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  JS madaraka matamu asikwambie mtu zile escort za magari unapishwa barabarani watu mnasimamishwa masaa matatu kusubiri rais apite vile vile Gbagbo anaweka ngumu kuachia madaraka maana kuna makubwa mengi yanaweza kumkumba na kama akiachia madaraka sidhani kama ataendelea kukaa Ivory Coast
   
 11. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Afrika tamu jamani, akitoka ikulu hajui pa kwenda!
   
 12. L

  Leornado JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndo maana namsifu Dk Slaa kwa busara zake, alishinda wakamchakachua amekubali yaishe for the sake of amani. Imagine na yeye angekuwa kapiga kambi kwenye hotel flani na jinsi alivyo na wafuasi si ingekuwa balaa?? shame on you African presidents especially in East Africa. Tumeona Kenya 2007 na TZ 2010 mnavyon'gan'gania ushindi.
   
 13. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Du nimeona ikulu ya Ivory Coast ina ukuta gereza la Ukonga linasingiziwa,si ikulu ila ni gereza,tofauti na ikulu yetu ambayo unaweza hata mkulu akinywa chai sebuleni
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ha ha ha ha lol!!!!!!!!!!!!!
   
 15. m

  mpweke Member

  #15
  Dec 14, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Anataka Serikali ya Umoja wa Kitaifa, maana hii ndiyo demokrasia inayokua kwa kasi Afrika. Siku zote Afrika itaendelea kubaki nyuma mpaka pale wanasiasa wa aina hii watakapoondolewa madarakani.
  Heri nionekane muongo kwa kusema ukweli, kuliko kuwa mkweli kwa kusema uongo
   
 16. b

  bob giza JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we jamaa una akili sana...hapa afrika bila ya kuanza kuua hawa watu hii kirusi ya kung'ang'ania madaraka mpaka mseto itatumaliza...ukiua wawili watatu wenyewe wataogopa na kuanza kuheshimu demokrasia..ua tuu iwe kiutaratibu unaoeleweka au kimafia..i hate these people and am convinced that we now need some lethal kind of action to silence these muther****ers of gbabo type...
   
 17. j

  j4marunda Member

  #17
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kusema ukweli Africa tuna safari ndefu sana ya kuelekea demokrasia ya kweli.Pale uchaguzi uliporudiwa tarehe 28 Nov wengi hatukuwa na wasiwasi kwamba kuna mambo yatatokea baada ya kupiga kura.Kwa mawazo yangu ni bora kianzishwe chuo cha kufundishia viongozi wa Africa kuhusu demokrasia! maana hata professor wa chuo kikuu kama Gbagbo anafanya mambo haya!
   
 18. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naogopa sana... mara nyingi tunachukua muda mwingi kujadili habari zilizopotoshwa. Nimezungumza na jamaa wawili kutoka Ivory Cost, wanasema kuwa media inatumiwa na west countries kuuhadaa ulimwengu. Quattara hajashinda hata kidogo, bali kilichofanyika pale ni attempt ya kupindua serikali katika mchakato wa uchaguzi.

  Mwenyekiti wa Electoral Commision alitekwa na kulazimishwa kumtangaza Quattara kama mshindi. Sasa hivi huyo jamaa Chaiman of the Ivory Cost Electoral Committee na familia yake hajulikani alipo. Inakisiwa yupo kwenye hiyo hotel ambayo Quattara yupo, UN nao wapo hapo, waasi wanakaa kwenye hotel hiyo ya ki-Faransa.

  Amenipa maelezo mengi na ya kutisha sana kiasi sina muda kuya post yote. Anasema France ndio wanaovuruga nchi hiyo. Wamejaribu kumpiga risasi kama unavyopendekeza lakini mara zote walishindwa. Jamaa ni mcha Mungu ile mbaya, na anafunga mwezi mzima akiomba ulinzi kutoka kwa Mungu. Ndege za Wafaransa zilikuja kupiga mabomu kwenye makazi yake lakini hawakuona nyumba yake bali waliona watu wenye nguo nyeupe wengi sana. Hivyo wakashindwa kupata target ya nyumba yake.

  Sasa hivi ECOWAS, AU, UN wamemlaani Gbagbo kama ameng'ang'ania madaraka kinyume cha matakwa ya wa Ivory, lakini wana Ivory Cost wameandamana huko France kupinga kile kinachofanywa na huyo colonial master kupindua ukweli wa mambo. Bunge la France limegawanyika juu ya tukio hilo. Huko nyumbani Ivory Cost karibu nchi nzima, machief wa makabila yote wameweka msimamo wao kwamba wakimchagua Gbagbo kuwa rais na sio Quattara.

  Kwahiyo jamani, tufanye uchunguzi ili tuusemee ukweli na siyo uzushi, no research no right to speak... sio kweli kuwa mara zote incumbent leader ndiye anaye rig election kwani this time round Quattara (the opposition leader) ndiye amefanya mchezo mchafu na akisaidiwa na mafia!
   
 19. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  :amen: quraan + voodoo= mcha mungu! :A S thumbs_down:

  mkuu hapa umeongea pumba jaribu tena.
   
 20. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Lakini safari hii Gbabgo imekula kwake. Zuria chekundu anajiwekea mwenyewe. Hakuna anayemtambua kama ndiye Rais. Hata akikataa kuondoka itamsaidia nini
   
Loading...