QUANTUM IMMOTALITY: Nadharia ya kukwepa kifo. Je, ni kweli raisi wa urusi PUTIN anaishi milele?

daVinci XV

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
1,827
2,000
QUANTUM IMMOTALITY

Wasaalam

kuna mtaalamu alipata kusema
"UBONGO WA MWANADAMU HAUJAWAHI KUWAZA KITU AMBACHO HAKIPO AU HAKIJAWAHI kuwahi KUWEZEKANA AU KUJA KUWEZEKANA"

kama hujanielewa kwenye nukuu hiyo utakuja na maswali mengi kwenye baadhi ya vipengele huko chini.

Tumejifunza vingi sana kuhusu maisha na vilivyo nyuma ya maisha ya kawaida

Na WAKATI MWINGINE inatakiwa tukubali kuwa kuna NGUVU nyingine inayoendesha na kutawala hii dunia yetu tofauti na ubidamu

Wazungu wamekuwa na michezo ya kutuchezea bongo zetu ,,,,kwa namna mbalimbali na kwa mambo ambayo hatukuwahi hata kuyafikiria

Dan Brown mwandishi nguli wa Vitabu vya fiction alipata kusema fiction nyingi huwa zinapenyeza ujumbe ulojificha

Sasa hapa utaongeza mwenyewe kama utaona kama fiction movies mfano wa movie za marvel nazo ziko kwa njia ya kufurahisha au kuleta na ujumbe pia

Ni wewe na imani zako, kwa sababu imenenwa imani huponya


Vladmir Putin, Raisi wa urusi ni kati ya watu wanaodhaniwa kuwa ni "immortal people" watu wasiokufa

Screenshot_20210119-082608.png

RAISI WA URUSI VLADMIR PUTIN


Ushawahi kusikia nadharia ya QUANTUM IMMORTALITY basi huyu bwana hio nadharia amehusishwa nayo sana

Quantum immortality ni uwezo wa kukwepa kifo hii inahusu uzoefu na uwezo binafsi wa kujua hatari za kifo na kukwepa ni kama inaelezwa pia ni kama kujiua kwa kiasi.

Wazo hili wakati mwingine linafikiriwa kuwa linatumika kwa sababu za ulimwengu ambao sio halisi (huu tuliopo sisi)

Wataalam wengi wanakazia kuwa jaribio au wazo linalohusiana na kukwepa kutokufa halitafanya kazi katika ulimwengu huu wa kweli tuliopo sisi.

Ni vyema ukaenda kwa mtandao kujifunza zaidi kuhusu hio nadharia. (wameelezea hadi namna inavyofanyika)

Watalamu wanoelezea nadharia hii wanasema kuwa watu wa mtindo huu wanauwezo wakutumia asilimia 50% ya ubongo.

ikumbukwe wataalamu wengine pia wana nadharia nyingine isemeyo binadamu wakawaida (yaani mimi na wewe ) tunatumia asilimia 2-1% tu ya uwezo wa bongo zetu

watu ambao wamefanya maajabu makubwa katika ulimwengu kwa gunduzi mbalimbali ,, mfano Albert Eistein, Isaac newton, Hawking na Nikola Tesla inaelezwa ndiyo baadhi waliojaribu kutumia japo aslimia 10%-15% ya bongo zao.

Screenshot_20210119-082401.png

NIKOLA TESLA

Screenshot_20210119-082439.png

SIR ISAAC NEWTON

Nadharia hiyo ilienezwa na mwandishi LOWELL THOMAS ,na kuna movie kadhaa zinaelezea nadharia hii...na zimejaribu kuonesha kama binadamu atatumia asilimia 100% ya ubongo wake mambo yatakuwa vipi

Lakini nadharia hio imepingwa na wanasayansi wengi wakiamin kila mtu ubongo wake unafanya kazi kwa asilimia 100%

Putin anahusishwa na nadharia hii kutokana na matendo mbalimbali ya ajabu ambayo anahusishwa nayo

Hata hivyo picha kadhaa zinamuonyesha na kudhaniwa alikuwepo toka mwaka 1920 na alipigana vita ya pili kama mwanajeshi

Screenshot_20210119-082210.png


Na hili baadhi ya watu ulimwenguni huliamini kutokana na Putin kuwa mwanajeshi kabla.

Screenshot_20210119-082137.png


Hatujui chochote kuhusu hii michezo ya wazungu kama ni ukweli au ni drama

TUNAHITAJI DONDOO ZAIDI ....

karibuni

DA'VINCI XV
 

The Infinity

JF-Expert Member
Sep 21, 2019
495
1,000
"Kila nafsi itaonja mauti, na bila
shaka mtapewa ujira wenu sawasawa
siku ya Kiyama. Na aliyewekwa mbali
na Moto na kuingizwa Peponi, basi
amefaulu; na maisha ya dunia hii si kitu
ila ni starehe idanganyayo"

Qur'an Surah Al-Imraan; Aya ya 185
 

daVinci XV

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
1,827
2,000
"Kila nafsi itaonja mauti, na bila
shaka mtapewa ujira wenu sawasawa
siku ya Kiyama. Na aliyewekwa mbali
na Moto na kuingizwa Peponi, basi
amefaulu; na maisha ya dunia hii si kitu
ila ni starehe idanganyayo"

Qur'an Surah Al-Imraan; Aya ya 185
sahihii kabisa ,

Malaika jibril ambaye tangu adamu mpaka sasa yupo hai

Nabii issah (yesu) mpake leo hii yuko hai mpaka siku atakayorudi tena kutokomeza ufisadi wa massih dajjal

Ibilisi (shetani) mpaka leo hii yuko hai, akiendelea kupotosha watu mpaka siku ya mwisho

Na je uliwahi kuskia pia habari za khizrii

Basi hao wote watakufa hamna cha kusalia

Na kuna vitu huwa vinaitwa nadharia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom