Q-NET naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu

Hili wazo lako nadhani uwape ndugu zako, kuanzia wazazi mpaka mke, dada, kaka, nk. Ili mpate hizo faida unazoahidi.
mkuu najua uli fail kiswahili. nime maanisha ni biashara kama biashara nyingine ila inahitaji nguvu kubwa sana na hupati faida kwa kukaa nyummbani lazima utoe uongoo na ukweli kwa mtu ili wewe ulie jiunga uweze pata commission. bila hivyo ni bila bila
 
Hahaaa hao jamaa waliacha nikatemana na demu wangu, demu kaingzwa mjini wakamla 1.8M akaanza kunishawish na mimi, kdg tu "sasa vip kuhusu kujiunga qnet?", nguva ya ushawish ikazidi akafanikiwa kunipeleka mbishi mimi kwenye semina ila nishapanga kichwan kama naenda tu kumridhsha, aisee nilishushiwa sumuuu, they left no space for question, nilihisi nimeelewa kila kitu nikaanza kujuta kwenda mana nilishaona nati za msimamo niliotoka nao home zmeshaanza kulegezwa moyo ukaanza kufunguka taratibu, wakaniuliza mara tatu "umeelewa kaka?" mzee mzima kwa upole wa mawazo km 2M nilizotafta kwa shda soon zitanitoka nikajibu NDIO, kwa bahat mbaya kwao nzuri kwangu, akaja jamaa mwingne mpya wakaanza kumpa semina wakaniweka pending kdg kwaio nikawa nimesogea mbali kdgo kuna shm nikakaa, pale ndo nikaona faida ya kulazmisha ubongo na moyo kufanya kazi katika halmashaur mbili tofauti, akili ilichelewa ku login haraka wakat natemewa sumu moyo nao ukawahi kupenda, sasa ndani ya ile dk moja tu akili ikarud fasta, nikaanza kujiuliza hv kweli nimeelewa sumu ndefu vile hata swali nikose? Fasta yakaanza kuja maswali kama mvua, sikutaka hata kwenda kuuliza nikatoka kimya kimya nikapanda daladala nika block namba zote na za yule ex wangu, kuanzia pale ukawa mwisho wetu. Mpaka leo siamin moyo wangu kbsa.
Dah! Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora wew 5M kuna mama kapigwa 15M hapa mwanza, alidanganywa akawaunga wanae wawili, kuna jamaa mwingine kaingizwa mkenge akakopa leo hii anauza nyumba yake
Mkuu pale Mwanza walinikosa kosa mbaya....tawi lao la kule kona ya Bwiru...Daah hawa watu almanusura wanisafishe
 
Mkuu pale Mwanza walinikosa kosa mbaya....tawi lao la kule kona ya Bwiru...Daah hawa watu almanusura wanisafishe
Mkuu hawa watu hawafai, wameharibu kanisa la watu bure, yule jamaa aliekuwa na wadhifa fulani kanisani baada ya kuuza nyumba na mikopo juu ili akatajirike huwezi amini siku hizi jua lake kutwa nzima anafuta wateja
 
kuna mtu namsubiria kwenye kona, nishamwambia sijui hao alliance global ni uhuni haelewi. juzi naona kajaza vifurushi vya hao jamaa chumbani kwake

anajidai mtafutaji kunizidi juzi anahangaika hana hata mia nami nimeweka vikwazo vya kiuchumi ale matunda ya alliance
Hahaha, DAH ni kwanini serekali inaruhusu haya mambo

:Dont folo folo me wizout ene bikoz:
 
Sisi wenye Rasta na Afro hapa Tunachekelea sana


Umeona Mkuu, yaani hata huko mahakamani watakushangaa.. Ununue saa kwa M8 kisha baada ya mwaka upate bilioni..? hata ingekuwa milioni 10 bado ulitakiwa ujiongeze mwenyewe..

Nakubaliana na msemo wa wahenga, kwamba akili ni nywele, kila mtu ana zake..
 
Jana nimepelwkwa na rafiki yangu sehemu hata hajaniambia wapi, nikaanza kuhisi asije akaniua huyu kuitwa tu twende kwenye fursa kimya kimya. Nkkachukua all precautions wakat nimeingia tu kwenye hiyo nyumba nikapewa nje kiti, ikabidi nishee na mke wangu last location kwa njia ya whasap alafu nikawasha location iwe active.

Mara naingia ndani watu tunasimama kama duara hivi tunaweka mikono nyuma alafu tunaambiana Goodmorning wakati ni jioni, nikajiuliza these people are jokin or what is this, kwakweli mpk muda huyo nilikuwa na mixed feeling na ya mwisho kuja kichwani ilikiwa nimeletwa freemason

Mara nikaanza kupigwa somo la Qnet. Yani muda wote wananijenga kisaikolojia kichwani im like "mpigie gitaa mbuzi akitikisika unahsi anacheza" nimetoka pale kwakweli roho iliniuma sana kwaajili ya mshikaji alienipeleka maana kaliwa kichwa mwezi uliopita.

Mie haya ma bussines nilianzaga kupelekwa tangu enzi izo 2007 forever living, nayajua vema, ma Qnet nilishayasoma humu Jf.

Nmeishi na kuona watu wengi miaka na miaka waliojiunga na pyramid schemes lakini sijawahi ona successful hata mmoja physically, zaidi ya picha wanazobandikaga kwenye kuta na majarida ili kushika vilaza wengine.

Nimewapa moyo narudi jumanne. Sasa nawaza tu. Hapa mwana namtoaje maana sasa anaenda kufilisika na hatafanya deal zake za maana akisubiria utajiri wa millions of money per week kama wanavyoaminishana na salam zao za good morning, na majina ya kijinga eti business partner

Dumelang
 
Back
Top Bottom