Q-NET naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu

Kimsingi hawa jamaa sio wezi. Ukifuata vile wanavyotaka pesa unapata. Swali ni kwamba kuna watanzania wangapi ambao wanaweza kuwa na chain ya watu labda kumi ambao watakua tayari kutoa mil 4.5/5 kila mmoja ili uweze kupata pesa?

Iko hivi... Hii ni biashara ya mtandao kama inavyojieleza. Unatengeneza mtandao wako na pesa inaingia kutokana na ukubwa wa mtandao unaoutengeneza. Ukishindwa kutengeneza mtandao huwezi pata pesa.
Kwa muktadha huo huwezi kuwashitaki kwa sbb baada ya kutoa pesa kazi inabaki kwako sasa ulete watu mtandao wako ukue nawe upate pesa. Na jamaa wako wazi kabisa tangu mwanzo.
Tatizo ninaloliona na ukurupukaji na tamaa ya pesa nyingi.
Kwa maoni yangu ni kwamba hii sio biashara haifai kwa nchi masikini kwa sbb watu wengi wanaingia kichwa kichwa na mwisho wa siku wanalalamika kuwa wamepigwa.
Hao jamaa ni wezi, watu kumi mjiunge Kwa 5mill hyo tayar ni 50 mil, in return Kwa watu hao kumi haifiki hata 2mill, ko 48 mill imepigwa hapo, wakata in real sense hyo 50 mill Kwa watu kumi mkijichanga mwaweza kufanya kitu kikubwa Sana ,
 
Hajaielewa hiyo biashara, na saa ni miongoni mwa bidhaa zinazouzwa kupitia Qnet.

yy awe mpole biashara hiyo mm nilisha someshwa darasa Mara 2 nikaingia pia mtandaoni kuona biashara hiyo ikoje?

Nikaona biashara hiyo ni uporaji wa fedha toka kwa rafiki zako au majamaa zako. Pia biashara hiyo ni ya watu wenye UWEZO KIFEDHA.

mfano umevaa saa nzuri ya 5m , unakatisha nayo Mbagala kwa Mpalange Nani? Atakayethaminisha au kutofautisha na zile za Machinga za tshs 5,000/=?

Saa hiyo hiyo ukiivaa na kukutana na rafiki, jamaa au kampani kubwakubwa za walionazo ambao wametembea na kufanya shopping dunia nzima, anapoona hiyo saa kwako wakati alishawahi kuiona kwenye Mall huko PANAMA. na akaingia baridi.

atakuuliza vp hichi kidonda mwanangu umekipata wapi? Hapo ndo soma linapoingia unampa mchongo na kumuingiza kwenye Qnet ww kwa kuwa tayari una code anaingia kupitia kwako hivyo ww unapata bonus ya usd 200.
 
Hivi kwanini watu huwa hawasikii ? Kuna thread nyingi sana humu huwa tunawaambia hao jamaa wote wa pyramid schemes na hao qnet ni MATAPELI WA KUTUPWA ...lakin hua hamsikii kabisa ...usawa huu wa huyu jamaa madarakani unampa mtu milioni 5 tena hao jamaa nduguze na gnld na wengineo , si bora mngetukopesha sisi wahitaji jamani kila siku tunaandika thread za kuomba mkopo humu lakin mtu yuko radhi akawape forever living products na jamii ya hao qnet ...yani wote hao wezi tu...sjui forever, sjui gnld, sjui qnet, sjui bitcoin, sjui forex...
Mimi hao wakinijia naishia kuwatukanaga tu.
Forex sio wezi...FOREIGN EXCHANGE MARKET ni biashara ambayo kama upo smart kichwani unaweza jifungia ndani na ukajifunza wewe mwenyewe na practise nyingi then ukaanza na kuweka ela yako bila kumpa mtumwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forex mentor hapa..........Njoo pm ......Kuungwa group la mafunzo ni tsh 25,000/=……Muda wote jumlisha na signal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mpuuzi mmoja ananisumbua kweli kuhusu hawa jamaa wa Q NET natamani nimchane lakini ngoja apigwe akili imkae sawa.
 
Nimepigwa na hawa wezi wa Qnet wamenishawishi nikaingia nikanunua SAA mil 5 nitapata Mara mbili zaidi ya hapo.

Naomba mnipe pesa zangu tutauwana Mwaka huu mil 5 hivi hivi, then mpaka sasa bila bila nitakuja ofisini kwenu na polisi mambo ya utapeli iwe mwisho kabisa.
Pole sana,ila nineamini kweli wajinga ndio waliwao.Mimi walinijia nikawastukia kutokana na maelezo yao.Maelezo yao yanaonyesha wazi kwamba ni Pyramid Scheme,kama ile DECI iliyokuwa contravercial sana hapa nchini miaka ile na ikaliza watu wengi sana.Wajinga sana,eti wakishakujia wewe wanakuambia usimwambie mtu,kama ni kitu genuine,kwa nini watu wasijue,mnaficha nini?

Then nikaingia kwenye mtandao na kuwasaka.Nikakuta walishapigwa marufuku kwenye nchi fulani fulani kama Rwanda,India na kadhalika.Nikatoka nduki.

Nadhani kuna haja ya serikali kuingilia kati na kuwasambatisha once and for all.Haya ndiyo majukumu ya serikali,kulinda wananchi na mali zao.Police mko wapi?
 
Ole Sabaya ameshaliamsha dude kuhusu Hawa QNET
 
Back
Top Bottom