Q-NET naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu

Mm kuna bro nilisoma nae chuo alikuwa ananisumbua kila siku kuna business ya pesa ndefu tuifanye nikimuuliza IPI mbona unipi intro anasema mpk tuonane baada km miezi miwili nikaona nionane.

Akaniambia tuonane makumbusho ule mtaa wa Mesuma hotel akanipeleka ofisi zao nashangaa kila MTU good morning wakati jioni kunipeleka ndani ndio anaanza kuniambia huo upuuzi wao.

Kwa heshima yake nikavumilia mpk walipomaliza nikawaambia nitakuja tena, nilivyoondoka pale mpk Leo sijarudi na simu sipokei tena.
 
sipendaga izo vitu cha makert networking juzi rafiki yangu akanidanganya kuna issue anataka tufanye tukapanga tukutane kwenda kumbe ndo ananikutanisha na hao watu wanaongea uwiii nikabaki natoa macho tu walivyo wahongo eti wote wameacha kazi nzuri za mishahara ya 1m and above coz hii inalipa sana nilivyotoka hapo nikasema sirudi tena simu zinavyopigwa kila saa niende kumalizia course hujui session iliyobaki , yani maisha ya biashara yangekuwa kama wanavyoongea life ingekuwa simple sana
 
Kweli kabisa, wanajua wakisema ukweli watakukosa na biashara yao itafeli. Ila wanaushawishi wa hatari aisee, mie walining'ang'ani kwa miezi mi3 mpaka wakaamua kuniacha tu
wakishakupiga semina zao zile mbili lazima wakulazimishe maana wanajua umefahamu 75% ya mambo yao ila ki ukweli ni waongo wana maisha ya kimovie tu ukiaa nao utaona wanaanza kujipisha story ooh kuna dokta ameacha kaona aimlipi kaja qnet amelalamika saana kwamba amechelewa mara kuna rubani kaacha kazi juzi tunae humu ndani yaan usanii mtupu
 
Hivi kwanini watu huwa hawasikii ? Kuna thread nyingi sana humu huwa tunawaambia hao jamaa wote wa pyramid schemes na hao qnet ni MATAPELI WA KUTUPWA ...lakin hua hamsikii kabisa ...usawa huu wa huyu jamaa madarakani unampa mtu milioni 5 tena hao jamaa nduguze na gnld na wengineo , si bora mngetukopesha sisi wahitaji jamani kila siku tunaandika thread za kuomba mkopo humu lakin mtu yuko radhi akawape forever living products na jamii ya hao qnet ...yani wote hao wezi tu...sjui forever, sjui gnld, sjui qnet, sjui bitcoin, sjui forex...
Mimi hao wakinijia naishia kuwatukanaga tu.
Daaah....kumbe wako wengi hivyo !
 
Back
Top Bottom