Qnet naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu..

wanaojulikana

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
577
1,000
Nimepigwa na hawa wezi wa Qnet wamenishawishi nikaingia nikanunua SAA mil 5 nitapata Mara mbili zaidi ya hapo.

Naomba mnipe pesa zangu tutauwana Mwaka huu mil 5 hivi hivi, then mpaka sasa bila bila nitakuja ofisini kwenu na polisi mambo ya utapeli iwe mwisho kabisa.

Qnet naomba muwe waungwana mlimshawishi mke wangu na shemeji watoe milioni 8 ambayo walinunua saa mkasema baada ya miezi 13 watapata bilioni 3.3, mbaya zaidi mkamwambia don't share the information. Yaani mnafanya siri mazungumzo, hela mke katoa lakini mnamzungusha sijui mnasema apeleke mtu mwingine tena ndo alipwe, nyie ni matapeli wakubwa na kesi iko police.

Nawapa onyo mkinishinda mahakamani naenda Gamboshi kuwaroga, nyie watu wa ajabu mlianza kwangu baada ya kunipiga porojo zenu nikawashitukia mkamdanganya mke na shemeji na hii njia yenu kutusalimia good morning hata jioni nahisi ndo njia ya kuwapumbaza watu, nawaambia io hela mtaitoa, mama yangu msukuma.
 

ngajone

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
532
500
Dah..... Dah yaani unafanya unafanya manunuzi ya bidhaa kwa Bei Mara 10 zaidi ya thamani Yake Sokoni ambayo haipungui 5m ndiyo unaingia....kisha utafute watu wengine 2 wafanye manunuzi ya 10m ndiyo upewe laki 4.... Yaani Chini ya 3% ya biashara uliyofanikisha
Me wameniita mara 2 nikaenda na semina yao nimesikiliza lakini zote nimewatosa
 

General Stalin

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
627
500
QNET na D9 ni hao hao tu. Wanatafuta mpumbavu mmoja ili awasaidie kupata wapumbavu wengine.
Hawatafuti wajinga bali wapumbavu. Mjinga akielewa atachomoka, lakini mpumbavu hana tiba.
Sorry for the strong words. Wakati mwingine inabidi tu!
ukweli unao umma ukiwakosoa tu matusi utakayokula utatamani kuwapeleka polisi
 

Mtemikwila

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
1,374
2,000
Nikiwaambia njooni mpitimbi tulime hamtaki sasa ngoja mkomeshwe hivyo hivyo, wanaume wa Dar ni watu wa hovyo sana aiseee.
 

xxxxx5

Member
May 3, 2017
43
125
hawa jamaa sio kidogo waninase na kamtego kao ila kupitia jamii forum ilinielimisha na kunuokoa kutoka ktk hilo li Qnet
 

shylock

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
604
1,000
kuna jamaa yangu mmoja alikuja akanismbue akanipa huu mchongo kisha akaniunganisha na dada mmoja yupo Denmark. kuba vitu vingi tu wanauza kama simu,saa,gar ba etc. cha bei nafuu ni saa ndo hiyo inaenda kama 5m.
wanakwambia endapo utampeleja Mteja juna % flan Unapata.
niliwaza nikaona ni ujinga. nikapibga chini mchongo Huo hadi leo.
 

patano

Senior Member
Mar 25, 2017
102
225
Hawa Qnet wanasalamu yao Good morning iwe asubuhi , mchana hata usiku ...walitaka niingiza mkenge wakashindwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom