Q-NET Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?

Good point, Jana kuna rafiki mmoja yuko Qnet kanifuata na BMW nakiajiuliza amenunua lini Gari hii? Oh Mimi Nina pesa sana lakini kichwa kama changu kashindwa kwasababu nawajua wapigaji wale.

Pia wamewafanya vijana wengi kuacha kazi zao nzuri masikini

Mkuu ilikuwaje tena ukaingia King?
 
mimi kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kuna fursa kesho twende ukasikilize, ila kwa vile mjini shule nikang'amua kuwa itakuwa ni moja ya hizi pyramids scheme maana mtu hawezi tu kuanza kukualika kwenye fursa yenye hela kizembe tu.

basi nikaenda mikocheni pale nafika nashangaa watu wanasalimiana good morning mchana, wakanieleza pale mambo meengi kweli kweli wakati naondoka nikawaahidi nitarudi :D:D:D:D

wakajua wamepata kichwa kumbe michezo hiyo naijua kitambo
 
Bongo bana mambo ya ajabu kabisa DECI ililiza watu , lakini wahusika wakawa wanaiangalia tuu mpaka ilipotaka kufilisi Taifa ndio watu wanashtuka too late, mbona hii inaonekana wazi kabisa ni PYRAMID SCHEME? kwanini wahusika wasikamatwe mara moja?

1. Haya kuna wale wengine wa ndani wanaoitwa ' SANITARIUM" wengi ni waumini wa kanisa moja linalosali jumamosi, wanashikisha watu kacomputa eti kanaangalia magojwa mwili mzima,, wizara ya afya hamuwaoni hawa matapeli?
 
Wanaoingia huko wanakuwa na ma hope ya hatari, yaani unakuta wanasema soon nitanunua nyumba ya milioni 100. Kwa ujumla hope ni kubwa. Nimesoma wikipedia yao, nchi nyingi wamekuwa wakifungiwa, they don't last longer, na sasa wamevamia Tanzania

Katika maisha principle ni moja "No easy Money in life"
ilikuwa hivyo kwa jamaa yangu alikuwa D 9 sasa analia ajabu
 
Tafuta muda ufanye biashara. TANGU LINI UFUNGUE DUKA UWEKE BIDHAA HUMO NDANI alafu kila siku uwe hulifungui utegemee HILO DUKA LITAKUPA PESA. Eti umeibiwa?! Mwizi gani akuibie alafu akeambie njoo? UNATAKA URUDISHIWE BIDHAA? Nenda wakakupe namna ya kurudisha hiyo bidhaa upewe pesa yako nacho jua hilo linawezekana kabisa. Ila linamuda wake. USICHELEWE. Nenda wewe unaitwa ubapoteza muda nenda ukaelimishwe namna ya kufanya biashara au kurudishiwa pesa.. humu JF hutosaidiwa kitu. Meet them before it is too late. Hakuna PESA ZA BURE. Do sone thing find time for some thing. That is all.
Kuna mahali alisema ule ni mchango wako wa mwisho,kumbe unaendelea?.
Good morning business partner.
 
Hao jamaa ni matapeli wa kutupwa...ni zaidi ya DECI. Naomba TCRA iingilie kati utapeli huu wa kimtandao.
 
Wanaoingia huko wanakuwa na ma hope ya hatari, yaani unakuta wanasema soon nitanunua nyumba ya milioni 100. Kwa ujumla hope ni kubwa. Nimesoma wikipedia yao, nchi nyingi wamekuwa wakifungiwa, they don't last longer, na sasa wamevamia Tanzania

Katika maisha principle ni moja "No easy Money in life"
Bora tuendelee kuliwa kwa kubet jero jero,au tatu mzuka au biko
 
Nami nilikuwa mpumbavu kama nyinyi mwanzoni. Mungu aliponipa nafasi ya kufanya utafiti hasa baada ya mwenzangu kujiunga Leo najuta kwanini sikujiunga mapema!!?

Siku IPO Mungu awatoe mawingu meusi yaliyozingira bongo zenu
 
Back
Top Bottom