Q-NET Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?

Wezi wakubwa hao. Walimchuna jamaa yangu vibaya sana. Nilipomshitua ilikuwa tayari kaliwa! Hovyo sana hawa.
 
me wanlinishawish sesion ya kwanza nikawasikilizaa nikaambiwa nirudi ya pili cjui mikipata sikurudi tena matapeli wakubwa yani wanataja 1500USD kama mia200 lol kama vile ukienda toilet ukirudi unazikuta hapo mezani poleni mliolizwa
 
QNet ni matapeli. Acha kutetea ujinga. Tangazo gazetini si linalipiwa tu. Na tapeli siku zote anacheza vizuri na sheria ukimfuatilia unakuta hakuna sheria aliyovunja.

Hawa QNet waliingia Tanzania toka 2004 enzi hizo wanaitwa Quest Net wakiwa wanauza biodisc (kipande cha glass wanachodai eti kina manufaa kibao ya kiafya).

Ni utapeli tu wa network marketing na pyramid scheme zenye product geresha ndani yake. Ila Watanzania wengi hawajui haya mambo na wanakuwa impressed na ndoto za kumiliki magari na kwenda nje ya nchi.

Nimesikitika kuona manetwork marketing mengi sasa hivi yanatarget watoto waliomaliza form six wakiingia chuo yanawakomba vibumu vyao.

Hawa ni watoto kibiashara maana hawajui lolote kuhusu biashara ndo wanakuja kudanganywa na hizi pyramid scheme zenye bidhaa-geresha ndani yake (aka network marketing companies).

QNet ni wabaya zaidi kutokana na pesa wanayotoza. Ila wako pia Forever Living Products (FLP), Oriflame, GNLD, Tianshi, D9 na Universal Plan B.
Kama watu wananufaika wewe unawaita matapeli ww siwatakuita shetani?
 
Raha yake utapeli wenu huwa haudumu ni suala la muda tu utalia mkishapewa semina mnakuwa kama machizi wa kuota utajiri baadae akiri itakurudi ukiwa ushachelewa.
Q net wana miaka 15 ya biashara ww kalia ushamba
 
Kwakua wameandikwa kwenye gazeti (THE CITIZEN) ndio kimekua kigezo cha kutuaminisha? Hovyo kabisa
Sasa unadhani gazeti kama la The citizen linaweza kuandika taarifa zisizojiridhisha Nazo. Kweli ujinga ni kaburi
 
Sasa unadhani gazeti kama la The citizen linaweza kuandika taarifa zisizojiridhisha Nazo. Kweli ujinga ni kaburi

Labda nikushauri, ili kuficha upumbavu wako jifunze kusoma comment na kuelewa context then kama hauna uwezo wa kuelewa ni bora ukae kimya
 
Labda nikushauri, ili kuficha upumbavu wako jifunze kusoma comment na kuelewa context then kama hauna uwezo wa kuelewa ni bora ukae kimya
Mpumbavu ni mjinga kama wewe ambaye una msimamo. Kwanza si Gazeti la The Citizen, VP michezo kama ya formula 1 iliyowahi kusponsiwa na Qnet?
 
Sasa kwa akili yako hisa ni utapeli? Hivi nani aliwaroga wabantu?
Hisa ni km kamari. Haina tofauti na utapeli sbb mambo yakiharibika hautarudishiwa hisa zako. Hauna sehemu ya kushitaki.
Weka hisa lkn uwe tayari kwa lolote. Vipi kuhusu hisa za vodacom? Jiongeze, ni sawa unacheza tatu mzuka au biko
 
Hisa ni km kamari. Haina tofauti na utapeli sbb mambo yakiharibika hautarudishiwa hisa zako. Hauna sehemu ya kushitaki.
Weka hisa lkn uwe tayari kwa lolote. Vipi kuhusu hisa za vodacom? Jiongeze, ni sawa unacheza tatu mzuka au biko
Basi kwa tafsiri yako hata kuoa ni utapeli na kamali
 
utapeli ni utapeli hata uwe namiaka 100

Fungua basi network marketing ya kwako isiyo yakitapeli ili tupate pa kukimbilia. Siyo kutujaza roho mbaya ya uliyorithi kwenu bila misingi ya kisayansi na sheria za uchumi. Wewe jamaa yangu lzm ww ni fukara kwa akili hii
 
Nyote mnaolalamika mnataja watu wengine kuwa walitapeliwa au wanakaribia kutapeliwa.

Huu ni ujuha usiokifani.

Nyinyi si lolote Bali wakosa fursa. Kwanini msiende polisi?
 
hivi watu hawajifunzagi tu ivi mtu anakupa pesa kirahisi hivyo ushtukitu dunia hii hakuna cha pesa yakupata kieahisi hivyo

Imeandikwa wajinga ndio waliwao.

Ngoja waliwe ili akili ziwakae sawa.
 
Hao jamaa ni matapeli wa kutupwa...ni zaidi ya DECI. Naomba TCRA iingilie kati utapeli huu wa kimtandao.


TCRA haina msaada ktk ujinga wenu wa kujitakia.


Hivi ununue saa 5M halafu utegemee kupata 10m kila mwezi.


Kabla ya TCRA kukupa inakupasa upelekwe kwanza Mirembe ukapatiwe tiba.
 
Back
Top Bottom