Qatar yaomba kununua asilimia 10 ya shirika la ndege la American Airlines

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,764
2,000
Shirika la ndege la American Airlines limepata ombi kutoka shirika la Qatar Airlines ambalo linataka kununua asilimia 10 ya shirika hilo la Marekani. American Airlines ilisema kuwa Qatar ina nia ya kununua dola milioni 808 ya hisa zake.

Hisa kwenye shirika la American Airlines ambalo ndilo kubwa zaidi duniani zilipanda kwa asilimia 3.5 mwanzo wa mauzo. Mwaka 2015 Qatar Airways ilinunua asilimia 10 katika kampuni ya International Airlines Group (IAG) ambayo ni mmiliki wa British Airways na Iberia.

Baadaye mwaka 2015 iliongeza hisa zake hadi asilimia 20 na kuwa mmiliki wa hisa nyingi zaidi huko IAG.
Mapema mwezi huu Saudi Arabia, Misri, Bahrain na milki ya nchi za kiarabu, Libya, Yemen na Maldive, walikata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar.

Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri zote zilisema kuwa zitasitisha safari za ndege kutoka Qatar na kufunga anga zake kutoka kwa ndege za nchi hiyo.

bbc swahili
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,133
2,000
Let them be very careful! Hawa waarabu wana sera rasmi ya kutowabeba raia wa Israel kwenye ndege zao. Na walivyo wajinga soon, wataanza kuwekeana hadi vikwazo vya ushia, usuni, na vigezo vingine wanavyovijua wao.
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
3,976
2,000
Waarabu wa Qatar wana akili sana wanachokifanya ni watakaponunua hisa ndege za Qatar airways itatumia nembo za America Airlines kwahiyo itaruka kwenda na kutumia anga za Saud Arabia bila taabu kwahiyo vikwazo dhidi ya nchi hiyo iliyowekewa na Saud Arabia na washirika wake zitakuwa zimeshindwa upande wa usafiri wa Anga
 
ipo siku utakufa

Senior Member
Dec 8, 2016
146
1,000
Waarabu wa Qatar wana akili sana wanachokifanya ni watakaponunua hisa ndege za Qatar airways itatumia nembo za America Airlines kwahiyo itaruka kwenda na kutumia anga za Saud Arabia bila taabu kwahiyo vikwazo dhidi ya nchi hiyo iliyowekewa na Saud Arabia na washirika wake zitakuwa zimeshindwa upande wa usafiri wa Anga
Saudia na USA ni mabwana wawili wanaosikilizana sana ,saudia anaweza kuweka ngumu na hao Qatar wakanyimwa hisa
 
fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
8,066
2,000
Let them be very careful! Hawa waarabu wana sera rasmi ya kutowabeba raia wa Israel kwenye ndege zao. Na walivyo wajinga soon, wataanza kuwekeana hadi vikwazo vya ushia, usuni, na vigezo vingine wanavyovijua wao.
Unawashauri una hisa huko utakuwa kada wa ccm!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom