Qatar kuchezesha Africa Cup 2015 ?

mzenjiboy

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
907
382
Radio DW imesema ya kuwa Morocco imegoma kuwa mwenyeji wa Africa Cup of Nations 2015 kwa kisingizio cha kuogopa raia wao kuja kuambukizwa na magonjwa ya Ebola.

Kutokana na sababu hiyo nchi ya Qatar imesema wako tayari kuwa wenyeji wa dimba hilo ikiwa shirikisho la soka la Africa, CAF, wataiomba rasmi nchi hiyo.

Pia na timu ya Taifa ya Morocco imefurushwa kwenye dimba hilo.
 
Sifa moja ya kuwa mwenyeji wa African Cup of Nations, ni lazima nchi hiyo iwe barani Africa.

Sasa inawezekanaje nchi ya Qatar, ambayo haipo barani Africa, iombe kuwa mwenyeji wa AFCON?!

Inawezekana Qatar inataka kujifariji, baada ya uandaaji wake wa World Cup mwaka 2022, kuwa katika hatihati, kutokana na tuhuma nzito ya rushwa, ambayo inawakabili akina Blatter, kuwa walijazwa 'mapesa' ili waipendelee Qatar kuwa mwenyeji wa kombe hilo.

Sasa kila wakifikiria maviwanja ya 'kufamtu' waliyoyajenga nchini mwao kwa mabiloni ya US dollars, sasa wanaona bora viwanja hivyo viwe somehow busy, badala ya kuwa completely idle kwa kuiandaa hiyo AFCON!
 
issue ya rushwa haipo tena,leo wamesafishwa,hakukuwa na rushwa
 
Hivi si nasikia hao wajumbe wa FIFA nao walihongwa saa za Rolex, the same type, kama 'aliyozawadiwa' mkulu?

Lakini mbona nilisikia pia kuwa akina Blatter, walikataa kata kata kuzirejesha saa hizo za Rolex, kama ambavyo wale jamaa zao wa Bongo, ambao wao waliporejesha yale mabilioni ya EPA na 'soo' ikaisha abruptly?!
 
Sifa moja ya kuwa mwenyeji wa African Cup of Nations, ni lazima nchi hiyo iwe barani Africa.

Sasa inawezekanaje nchi ya Qatar, ambayo haipo barani Africa, iombe kuwa mwenyeji wa AFCON?!

Inawezekana Qatar inataka kujifariji, baada ya uandaaji wake wa World Cup mwaka 2022, kuwa katika hatihati, kutokana na tuhuma nzito ya rushwa, ambayo inawakabili akina Blatter, kuwa walijazwa 'mapesa' ili waipendelee Qatar kuwa mwenyeji wa kombe hilo.

Sasa kila wakifikiria maviwanja ya 'kufamtu' waliyoyajenga nchini mwao kwa mabiloni ya US dollars, sasa wanaona bora viwanja hivyo viwe somehow busy, badala ya kuwa completely idle kwa kuiandaa hiyo AFCON!

Hujui unachoongea...
 
Pia Morocco bora wangepigwa burn ya milele kushiriki michuano ya AFCON. Wana tabia ya unyanyapaa hawa waarabu koko
 
Kwani sisi Tz hatuna sifa zakuchezesha mashindano hayo??
Sifa moja kubwa ni kuwa nchi mwenyeji wa AFCON inatakiwa angalau minimum iwe na viwanja kama kile cha Taifa kilichopo Temeke, muwe navyo angalau 10 hivi.

Pia mahoteli ya hadhi ya nyota 5 kama Serena Dar na Kilimanjaro Hyatt, muwe nazo kama 10 vile vile.

Hapo ndipo utakapoona kuwa kumbe zile 'mbwembwe' ambazo huwa zinatolewa na watawala wetu wa CCM kuwa baada ya miaka 50 ya uhuru, tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele, kumbe hicho ni 'kibwagizo' tu cha kuburudisha 'vijiweni'
 
Sifa moja kubwa ni kuwa nchi mwenyeji wa AFCON inatakiwa angalau minimum iwe na viwanja kama kile cha Taifa kilichopo Temeke, muwe navyo angalau 10 hivi.

Pia mahoteli ya standard ya kama Serena Dar na Kilimanjaro Hyatt, muwe nazo kama 10 vile vile.

Hapo ndipo utakapoona kuwa kumbe zile 'mbwembwe' ambazo huwa zinatolewa na watawala wetu wa CCM kuwa baada ya miaka 50 ya uhuru, tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele, kumbe hicho ni 'kibwagizo' tu!

Mkuu acha kujidharau namna hiyo, kwanza viwanja vinavyotakiwa ni vinne tu sio 10, world cup ndio inatakiwa viwanja vingi
 
Sasa mkuu Ngongoseke umesema siyo vyema tukaonyesha unyonge wetu.

Hata hivyo umeeleza pia kuwa viwanja vinavyotakiwa vya standard ya kile cha Taifa kilichoko Temeke, vinatakiwa angalau to the minimum, tuwe navyo vinne.

Sasa swali, je hapa TZ tunavyo hivyo viwanja vinne, ili tuqualify kuwa wenyeji wa hiyo AFCON hapo January mwakani?
 
Back
Top Bottom