Qatar Airways kuchukua asilimia 60 ya hisa za uwanja wa ndege Rwanda

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Rwanda na Shirika la Ndege la Qatar zimeingia makubaliano ya TZS 3trilioni, ambapo Qatar itajenga, itamiliki (60%) na kuendesha uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Rwanda.

Uwanja huo utaweza kuhudumia watu milioni 7 kwa mwaka, na awamu ya pili itaongeza idadi hadi milioni 14.

IMG_20191210_195324.jpeg
 
Qatar Airways kuchukua asilimia 60 ya hisa za uwanja wa ndege wa Rwanda

Shirika la Ndege la Qatar Airways limeafiki kuchukua asilimia 60 ya hisa katika uwanja mpya wa kimataifa wa ndege nchini Rwanda ambao unatazamiwa kugharimu dola bilioni 1.3.

Kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa baina ya pande mbili, sehemu ya kwanza ya uwanja huo wa ndege itakuwa na jengo lenye uwezo wa kuhudumia wasafiri milioni saba kwa mwaka.

Uwanja huo wa ndege utajengwa katika wilaya ya Bugesera, yapata kilimota 25 kusini magharibi mwa mji mkuu, Kigali.

Sehemu ya pili ya uwanja huo inatazamiwa kumalizika mwaka 2032 ambapo uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumua wasafiri milioni 14 kwa mwaka.

Serikali ya Rwanda imesema mapatano hayo yataliwezesha shirika la ndege la Qatar Airways kujenga, kumiliki na kusimamia uwanja huo wa ndege wa kisasa.

[https://media]Picha ya kompyuta ya uwanja wa ndege unaopangwa kujengwa na Qatar Airways nchini Rwanda

Waziri wa Miundo Msingi wa Rwanda Claver Gatete amewaambia waandishi habari kuwa bado wanatafuta shirika ambalo litajenga uwanja huo.

Jumatatu Mfalme wa Qatar Sheikh Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani alitembelea Rwanda kushiriki katika kikao cha kimatiafa cha kupambana na ufisadi ACE.

Hii ni safari ya pili ya mfalme wa Qatar nchini Rwanda baada ya safari yake ya siku tatu nchini humo mwezi Aprili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila kuna wasiwasi mm naona kwenye haya makubaliano ,unless ni build operate and transfer ,sasa kama ni 99 years au whatever ? Naona usalama wa nchi uko matatani. Kingine kama wageni ndio majority holder maanake wana final say ,wanaweza wakamkata na raisi kuutumia kama wanamdai .Anyway this is Africa
 
Ukiona hivyo ujue uporaji wa madini na maliasili za DRC ni mgumu siku hizi! Siku za nyuma uchumi wa Rwanda ulipaa juu kwa sababu ya kuiba maliasili za jirani.
Wkt kipindi hiki PK na Tshisekedi ndio marafiki balaa na wanapiga Joint OP's huko porini fresh kabisaa.

Tena kama kuna kipindi mambo ni smooth/mswano kwa PK basi ni sasa hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila kuna wasiwasi mm naona kwenye haya makubaliano ,unless ni build operate and transfer ,sasa kama ni 99 years au whatever ? Naona usalama wa nchi uko matatani. Kingine kama wageni ndio majority holder maanake wana final say ,wanaweza wakamkata na raisi kuutumia kama wanamdai .Anyway this is Africa
Kwa hio kuna uwezekano wewe ukaona usalama wa nchi uko matatani kuliko PK na baraza lake zima sio mzee baba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ndege za mizigo zitakuwa zinatua Rwanda kwenye uwanja unaomilikiwa na wageni. Na hatutoweza kujua zinaleta nini au kubeba nini, na kuna DRC pembeni hapo

Sent from my PBCM30 using Tapatalk
 
Kwahiyo ndege za mizigo zitakuwa zinatua Rwanda kwenye uwanja unaomilikiwa na wageni. Na hatutoweza kujua zinaleta nini au kubeba nini, na kuna DRC pembeni hapo

Sent from my PBCM30 using Tapatalk

Kwa Rwanda ya Kagame au ipi hio?

Rwanda security ni kipaumbele chao cha kwanza kuliko hata chakula,hio ndege itakayotua bila kujulikana imeleta nini ngoja tusubiri tuione.

Halafu hayo mambo ya nchi/mtu kumiliki airport kwenye nchi nyingine mbona ni mambo ya kawaida sana tu?

Kuna mnigeria anaitwa Adebayo Ogunles yeye anamiliki uwanja wa ndege unaoitwa London Gatwick Airport aliununua kwa £1.5bil,je hio ina maana kwamba mizigo itakua inatua kwenye hio Airport bila kukaguliwa sababu Airport haimilikiwi na serikali?
 
Sio Rwanda kutojua, namaanisha sisi majirani kutojua. Kwani unataka kusema zile Tupolev zillizokuwa zinashuka Mwanza kuchukua samaki serikali ya Mkapa ilikuwa haijui zinaleta nini. Mbona Rwanda hiyo inashutumiwa kusaidia wapiganaji uko Congo na kuiba maliasili. Hapa ndo maana yangu

Huo mstari wa mwishi nimekuelewa vzr.
 
Kwa hio kuna uwezekano wewe ukaona usalama wa nchi uko matatani kuliko PK na baraza lake zima sio mzee baba?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wa Tzn ni watu wakutafutiza hofu zisizo za msingi na kuzikumbatia nadhani unakumbuka ishu ya bagamoyo port hii inasababishwa na mentality za kijamaa ambazo zinakujengea hofu ya kushindwa badala ya kuwa risk taker ufanikiwe si ajabu nchi yetu imejaa rasilimali lakini kutokana na huu utumwa wa kijamaa tunaogelea kwenye umaskini badala ya kuwa risk taker eti tunasubili serikali
Leo hii private sector ya Tzn ni kama inakufa kwanza kwa crackdown za serikali kupitia regulatory authorities na pia hakuna juhudi za serikali kuinua private sector mwisho wa siku unakuta serikali inafanya biashara mara inajenga masoko mara inaendesha mwendokasi mara sijui inajenga viwanda wakati mwisho wa siku poor service delivery na zitakufa sijui kwa nini hatujifunzi kwenye historia
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom