Qantas Airlines, shirika salama zaidi la ndege duniani

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,783
Shirika la Ndege la Qantas Australia lenye miaka 100 kazini limeshika namba moja kwenye orodha ya 2021 ya Ndege salama zaidi kusafiri nazo duniani iliyotolewa na airlineratings.com ambapo namba 2. Qatar, 3. Air New Zealand, 4. Singapore Airlines, 5. Emirates, 6. Eva, 7. Etihad 8. Alaska 9. Cathay 10. British Airways.

11. Virgin Australia, 12. Hawaiian 13. Southwest Airlines, 14. Delta Air Lines 15. American Airlines, 16. SAS 17. Finnair 18. Lufthansa 19. KLM 20. United Airlines.

Utafiti uliofanywa na Airline Ratings ulihusisha Mashirika 385 ya Ndege kote duniani na kutazama vigezo mbalimbali ikiwemo rekodi za ajali pamoja na ‘umri’ wa Ndege zenyewe.

Wamesema moja ya vilivyoipa namba moja Qantas ni kujali usalama wa abiria kwa kuhakikisha Marubani wote waliokua likizo kutokana na covid19 wanaingia darasani kwa mafunzo ya siku 6 kabla ya kuanza kuruka.

26229542_1919675288042775_8357914480278119156_n.jpg

189558_10150111057462686_8165147_n.jpg
 
Nakumbuka Air Tanzania ilishawahi kutoboka kioo angani.

Na tena ilishawahi kupasua tairi wakati inatua Mwanza.

Juzi Kati hapa ndege ilikuwa inaenda Mwanza, ikarudia njiani eti mafuta hayatoshi.

Hatuko makini kabisa kwenye kutoa huduma bora
 
Nakumbuka Air Tanzania ilishawahi kutoboka kioo angani.
Na tena ilishawahi kupasua tairi wakati inatua Mwanza.
Juzi Kati hapa ndege ilikuwa inaenda Mwanza, ikarudia njiani eti mafuta hayatoshi.
Hatuko makini kabisa kwenye kutoa huduma bora
Aisee hawa aviation inspectors wetu wanafanya kazi kweli? Hiyo ya kioo kutoboka angani haikusababisha ajari kweli?

Kweli hatupo makini katika huduma zetu. Kwasababu serikali ya awamu hii inajipambanua kuboresha shirika letu la ndani inabidi iwe na mikakati mirefu na mifupi kuhakikisha matatizo kama haya hayajirudii. Ni Jambo la ajabu sana ndege kurudi kwenye run way kisa haina mafuta ya kutosha!
 
Iteni basata waje huku wafungie watu, uvaaji gani huo wa watoto wa kike...
 
Back
Top Bottom