Q Chief ana uhusiano gani na wezi wa magari?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,059
4,053
Jana nimeibiwa laptop, power window, head rest, redio na mkoba uliokuwa na makabrasha na nyaraka mbalimbali nilipokuwa Mlimani City mida ya usiku. Walinzi wa Mlimani City wanasema kuwa wao hawahusiki na ulinzi wa magari. Basi kwenye kudadisi kwangu mlinzi mmoja akaniambia wanaovunja vioo na kuiba vitu kwenye magari hapo Mlimani City ni kundi la Q Chief.

Nikaenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Mwenge ambako nilipewa Rb. Polisi nao wakaniambia kuwa hilo kundi ni la Q Chief.
Polisi wakanielekeza niende mitaa ya gerezani huko ntaweza kupata vifaa vya gari yangu.

Sasa natokea gerezani, nimepata vitu vyangu na kuhusu laptop wameniambia niende Azam kuna bwana anaitwa Salehe nimuone.
Cha kushangaza ni hiki, Polisi wanajua kuwa Q Chief ni mwizi na anamtandao wake, kwa nini hawamkamati na kumfungulia mashtaka?

Kweli jeshi letu la Polisi linanuka rushwa.

Na wewe ni MWIZI! Huyo aliyekuelekeza Gerezani ni MWIZI! Huyo aliyekurudishia vitu vyako ni MWIZI

Taifa la WEZI! very sad indeed!

Q chief huyu huyu msanii au mwingine? hata hivyo Polisi na majambazi lao moja..wanampaka namba za simu za wezi..kama hayajakukuta unaweza usiamini.

Q chief huyu huyu msanii au mwingine? hata hivyo Polisi na majambazi lao moja..wanampaka namba za simu za wezi..kama hayajakukuta unaweza usiamini.
Muziki ulimshinda alidai eti TID anamroga. Naona sasa amejiajiri kwenye sekta rasmi ya wizi. Nikija kumuona ntamkamata, natembea na RB yake, nina machungu sana

Kiranja Mkuu hayo madai yako yanaweza kuwa na ukweli fulani ndani yake maana kuna sehemu moja inaitwa kontena maarufu kwa kitimoto iko mikocheni barabara ambayo ndipo ilipo hosptali ya AAR . Hiyo sehemu wateja waliokuwa wanaenda kuburudika pale walipokuwa wanapaki magari yao ikifika muda wa kuondoka wanakuta power window na vitu vingine havipo na baada ya uchunguzi ilikuja kugundulika ni huyo Q-Chief na kundi lake.

Baada ya kupigwa mkwara nafikiri alihamisha makazi na wizi haupo eneo hilo, hata wahudumu wa pale ukiwauliza watakwambia ni Q-Chief na kundi lake sasa sielewi dili hili wanacheza na mapolisi au vipi

Nawewe pia ni mwizi, polisi nao ni wezi, walinzi wa mlimani city ni wezi, na huyo aliyekupa vitu vyako pia ni mwizi. Wewe umeshaonana na wezi wako, badala uwakamate unataka umkamate Q chief.

Ukweli ni kuwa kila siku pale MC watu wanalizwa hivyo uongozi kama ungekuwa na nia ungekomesha wizi huo. Siku moja jamaa aliibiwa kwa kuvunja kioo cha nyuma. Nilipomuuliza mmoja wa wafanyakazi wa mighahawa iliyokua nje alidai ilo ni tukio la nne kwa siku ile na alidai kuwa kuwa ana uhakika kuwa hadi mwisho wa siku lazima wengine kama wanne walizwe.

"Hii mbona ilishakuwa kawaida alisema huyo dada...". Vile vile siku hizi wakupa kadi wakidai kuwa hawatausika ukiibiwa gari ama vitu ndani ya GARI. Jamaa alinisistiza kabisa MZEE hakikisha unasoma....

na nyie mmezidi kwa nini msikae bar za mabibo au kiluvya mnajitanua tanua tu mlimani city..hebu tupisheni hapa bana

na nyie mmezidi kwa nini msikae bar za mabibo au kiluvya mnajitanua tanua tu mlimani city..hebu tupisheni hapa bana

mi binafsi natamani kuifadhili hiko kikundi cha wana jf nimeona ma bronzo wengi wanaenda pale alafu majumban mwao wanacha familia inateseka na ugali maharage wao wanakula chips kuku ..ni wajinga sana sana nimeona wengi wanapendakuwa showoff..sio hilo tu walitakiwa wakuibe na wewe kabisa unless kama ulienda supermarket ambayo imefungwa

muziki ulimshinda alidai eti tid anamroga. Naona sasa amejiajiri kwenye sekta rasmi ya wizi. Nikija kumuona ntamkamata, natembea na rb yake, nina machungu sana

sidhan kama ni huyo dear's kijana anapiga kazi mmoja kali sana ya risk ambayo akienda safari akirudi ni hatamaniki na doller sio huyo kuna mr blue,...na wengi tu wakifika airport wanapoklewa na polisi wanaingiza ndani mpaka kwenye mlango wa emirates ...wakirudi utawakoma mzigo mingi wanaihamishia kwa madiba kazi kwako

Na wewe ni MWIZI! Huyo aliyekuelekeza Gerezani ni MWIZI! Huyo aliyekurudishia vitu vyako ni MWIZI

Taifa la WEZI! very sad indeed!

sasa mkuu, wizi wa kiranja mkuu uko wapi.yeye si amefuatilia mali zake alizoibiwa.. kama haunamchango sio lazima kucomment.

Ebana nilikuwa sijui kama Qchillah ni jambazi,.asante kwa kunijuza..chifu kiumbe kamtema nini!

na nyie mmezidi kwa nini msikae bar za mabibo au kiluvya mnajitanua tanua tu mlimani city..hebu tupisheni hapa bana

KHAAAAA YAMEKUWA HAYA KILA MT AKIJAA KILUVYA NA KINA QCHILA WANAHAMIA HUKOHUKO

Nasikia wameiba sana sana...power window siku ya jumamosi miss tanzania mitaa ya mlimani city

Jaman hebu nyoosheni habari msichafue watu kwa majina ya kupachikana kulingana na matukio

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom