Mupirocin
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,739
- 744
Ninatatizo la maumivu kwenye loin yaani chin zinamoishia mbavu na maumivu yanaradiate kwenda kiunoni na sometimes kiuno kinauma sana kiasi kwamba siwezi kukaa normally afu pia napata burning sensation kwenye miguu hata nikilala na nikikaa kwa muda mrefu. Maumivu yote yanapungua nikitembea na kurudia nikiwa nimekaa. Nimefanya urinalysis iko normal, abdominal uss nimeambiwa ninamoderate pyelonephritis, nimefanya urine culture no growth in 24hrs. Nimetumia dawa zifuatazo: ceftriaxone 1g od 5/7 then nikaendelea na ciprofloxacin tabs 500mg bd 5/7 maumivu yalitulia kidogo kama 2wks hivi. Yakaanza tena nikatumia gentamycin iv 160mg od 5/7 na ampicillin iv 1g tds 5/7, yalitulia maumivu kwa wiki moja tu na sasa napata maumivu makali sana. Nimefanya createnine iko normal ila uric acid ipo elevated kidogo. Sasa sijui nifanye nini maumivu makali sana Madr naomba msaada wenu. Natarajia majibu mazuri.