Pwani: Waziri Ummy amsimamisha kazi mganga mfawidhi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Waziri Mhe.Ummy Mwalimu aagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Mlandizi mkoani Pwani.
f43b2737d785cef39a9182f7090959d0.jpg

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu, amemsimamisha kazi Mganga Mkuu Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mlandizi, Stanley Tamambele ya kwa kushindwa kuwasimamia wauguzi na madaktari wa kituo hicho.

Tamambele amesimamishwa leo Julai 25, baada ya kubainika wauguzi na madaktari wa kituo hicho wamemtoza fedha kiasi cha Sh,180,000 mjamzito Salma Halfan kwa ajili ya kununulia vifaa ya upasuaji wakati vifaa hivyo vinapatikana kituoni hapo.

Mwalimu, ambaye alikuwa katika ziara yake ya kukabidhi magari matatu ya wagonjwa yakiwemo magari mawili yaliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa (CCM) na Rais John Magufuli aliyetoa gari moja na vitanda vitano vya kujifungulia.


Awali, kabla ya Mwalimu kukabidhi magari hayo alitembelea kituo hicho ambapo alikutana na Salma ambaye alikuwa amejifungua kwa upasuaji huku akidai ametozwa kiasi hicho cha fedha hali iliyomshangaza waziri na hivyo kutaka daktari na muuguzi aliyetoza fedha hizo kurudisha haraka.

Katika mazungumzo yake na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini Mwalimu alisema kuwa Serikali imewasamehe wajawazito na hivyo wanapaswa kutibiwa bure bila kulipa fedha yoyote hivyo jambo walilofanya kituoni hapo nilakushangaza na kwamba lazima wahusika wachukuliwe hatua.

Chanzo: Mtanzania
 
Hehe huyu naye hajajifunza kwa makamba tu!? Kawasimamisha kazi wale Wa NEMC, Alafu jamaa wanaendelea kuchapa kazi kama kawa

from Katesh using Siemens C55
 
Aliviona hivyo vifaa lakini? (Ili kujiridhisha kama kweli vipo.......)


Ila pole yake huyo alotozwa
 
Waziri Ummy, amesema mnamchezea kinyume.

Naomba mwache jamani. Yeye anasema dawa zimeongezeka, ila nyie mnamchezea kinyume.

Sio haki.

Source ni ITV habari. Saa 8:15 tarehe 25 mwezi Julai 2017.
 
Ukiona Mtu Anapiga Kelele Sana Ujue Kameza Kitu Toka Kwa Mafusadi
Ninapoyatumbua Mafisadi Watu Wananuna Sana Wanaweka Midomo Kwa Kununa Kama Vyura
By Jpm
 
Back
Top Bottom