Pwani: Wawili mbaroni kwa kukutwa na nyara za Serikali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
JESHI la Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji ,linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kukutwa na nyara za serikali, zinazodaiwa ni meno ya tembo , uzito wa kilo 25.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Rufiji ACP Protas Mutayoba alisema ,tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jana huko maeneo ya Utunge-Kisemvule wilayani Mkuranga.

Mutayoba alieleza kuwa, waliwakamata watuhumiwa hao wawili mmoja ni mwanaume mwenye umri wa miaka 40 na mwengine ni mwanamke mwenye umri wa miaka 21 ,wakiwa na nyara za serikali zidhaniwazo kuwa ni meno ya tembo vipande 16 vyenye uzito wa kilo 25 ambapo thamani yake haijajulikana.

Aidha Kamanda Mutayoba alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Katika hatua nyingine ,Kamanda Mutayoba alieleza, huko kitongoji cha Matope-Kimanzichana wilayani Mkuranga jeshi la polisi limemkamata mtuhumiwa mmoja mwanaume,akiwa na kilogram 150 za bangi ambapo mtuhumiwa huyo ameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kupatikana na bangi.

Aidha jeshi la polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kuwaasa wananchi kuacha tabia ya kufanya biashara haramu.



 
kamanda Mutayoba sio nyara za serikali ni nyara mungu,Kila mwanadamu amepewa talanta yake ya kujiingizia kipato
 
Dah! Hali ngumu watu wanataka kutusua kwa njia haramu huko nako wanakutana na mikosi na kizaa zaa...
 
Back
Top Bottom