Pwani: Polisi inamshikilia Salehe Masokola kwa tuhuma za kuwapa wanawake sumu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Pwani: Polisi inamshikilia Salehe Masokola kwa tuhuma za kuwapa wanawake sumu na kuwasababishia vifo.

Salehe Masokola (22), ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kunwe wilayani Mvomero mkoani Morogoro, anadaiwa kufanya unyama kutokana na ugomvi kati yake na mzazi mwenzake na watoto wao.

====

JESHI la polisi mkoani Pwani ,limethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto watatu akiwemo wa miezi kumi ,waliouawa kwa kunyweshwa sumu na baba yao mzazi.

Chanzo cha kutenda kitendo hicho cha kikatili kinadaiwa ni kutokana na ugomvi mkubwa kati ya wazazi wa watoto hao.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa alieleza tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huko kata ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

Aliwataja watoto hao kuwa ni pamoja na Shaila Salehe miaka sita ,Nurdin Salehe (4)na Sabrat Salehe mwenye miezi kumi waliouawa kwa kunyweshwa sumu ambayo ni dawa ya kuulia magugu iitwayo Twiga Amine na baba yao mzazi Salehe Masokola (22),mkazi wa kijiji cha Kunwe ,Mvomero mkoa wa Morogoro .

Wankyo alibainisha,baba wa watoto hao alikuwa na mgogoro na mkewe ambae ndiye mama wa watoto .

“Mtuhumiwa alipowafuata watoto kutoka kwa mama mkwe wake kwa madai kwamba anakwenda kucheza nao na angewarudisha baadae ” alifafanua Wankyo.

Alielezea,mtuhumiwa aliwapakia marehemu kwenye baiskeli kutoka Kunke hadi kitongoji cha Ditele ,Kibindu ambapo aliwanywesha dawa hiyo kwa kuwachanganyia na juisi hivyo kupelekea vifo vya watoto hao.

Kamanda huyo alisema ,katika eneo la tukio kumeokotwa chupa mbili za juisi zilizotumika ,chupa ya dawa na matapishi ambavyo vilichukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

“Mara baada ya tukio mtuhumiwa alikunywa sumu kwa lengo la kutaka kujiua lakini aliokolewa na watu kisha kukimbizwa katika hospital ya mission Bwagala wilaya ya Mvomero kwa matibabu” Wankyo aliweka bayana.

Mpaka sasa hali yake sio nzuri kwani yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa chini ya uangalizi wa polisi .

Katika hatua nyingine ,Wankyo alisema jeshi hilo limekamata viroba saba vya bangi vilivyokuwa vikisafirishwa kwenye gari yenye chesesi namba V75w – aina ya mitsubishi station wagon huko Kijiji cha Mwatemo kata ya Kiwangwa Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
 
watoao hawa wanaooa wakiwa wadogo ndio tatizo lao. Mtoto wa miaka 22 ana watoto wenzake watatu. Inamaana alioa akiwa na takribani miaka 14. Huu ni mtindio wa ubongo katika ndoa
 
watoao hawa wanaooa wakiwa wadogo ndio tatizo lao. Mtoto wa miaka 22 ana watoto wenzake watatu. Inamaana alioa akiwa na takribani miaka 14. Huu ni mtindio wa ubongo katika ndoa
Miaka 22 mbona mtu mzima,nyie ndo mkifikisha umri wa miaka 45 bado mnajiona vijana
 
huyu bwana salehe kwa ukuajia wetu wa ubongo na uelewa wa mambo bado ni mtoto, nchi za dunia ya kwanza na pili 18yrs ndo mtu mzima huku kwetu na ulaji wa ugali 25yrs ndo yafaa tuwe watu wazima.

Akili gani mbovu hii ya kuua watoto bila ya hatia eti kisa ugomvi wa familia.
 
m
Miaka 22 mbona mtu mzima,nyie ndo mkifikisha umri wa miaka 45 bado mnajiona vijana
mtu mzima nchi za dunia ya kwanza na pili izi zetu tunakula mashudu kama ng'ombe uwezo wa ubongo uko chini sana iyo 22 ni miaka tu ila uwezo wa ubongo wake ni mtoto wa 14yrs
 
Tatizo yeye mwenyewe bado mtoto ndio maana haya yametokea mtu wa miaka 22 ana watoto 3 usishangae mama watoto akawa ana miaka 20.

Wanaume wa mikoani acheni ukatili
 
Kamanda wa Mkoa wa Pwani anaripoti taarifa ya Mkoa wa Pwani.Wajuvi nijulisheni kama kuna uwezekano kamanda wa Mkoa fulani akakaimu ukamanda Mkoa mwingine.
 
Kamanda wa polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa alieleza tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huko kata ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo

Mara baada ya tukio mtuhumiwa alikunywa sumu kwa lengo la kutaka kujiua lakini aliokolewa na watu kisha kukimbizwa katika hospital ya mission Bwagala wilaya ya Mvomero kwa matibabu” Wankyo aliweka bayana.

Mpaka sasa hali yake sio nzuri kwani yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa chini ya uangalizi wa polisi .

Pwani - Chalinze wilaya ya Bagamoyo, then ghafla Mvomero - Morogoro, naomba ufafanuzi hapa mtuhumiwa alikwendaje Chalinze na Mvomero ndani ya muda mfupi namna hiyo. Je huko Chalinze hakuna hospitali?
 
Pwani: Polisi inamshikilia Salehe Masokola kwa tuhuma za kuwapa wanawake sumu

Pwani: Polisi inamshikilia Salehe Masokola kwa tuhuma za kuwapa wanawake sumu na kuwasababishia vifo.

Heading inataja wanawake, ndani habari inaelezea watoto, hapa uandishi haujakaa sawa kabisa
 
Pwani - Chalinze wilaya ya Bagamoyo, then ghafla Mvomero - Morogoro, naomba ufafanuzi hapa mtuhumiwa alikwendaje Chalinze na Mvomero ndani ya muda mfupi namna hiyo. Je huko Chalinze hakuna hospitali?
Mkuu nimerudia kuisoma habari , mwandishi yupo sahihi.Itakuwa hivyo vijiji vipo mpakani mwa Mikoa ya Pwani na Morogoro
 
Mwanzoni mwa wiki hii kuliripotiwa habari kama hii pia huko Mvomero

Screenshot_2018-12-01-10-28-50.png

https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjAKegQIAhAB&usg=AOvVaw0HIRvRKYvepcH9qwUIB3Zl
 
Mkuu nimerudia kuisoma habari , mwandishi yupo sahihi.Itakuwa hivyo vijiji vipo mpakani mwa Mikoa ya Pwani na Morogoro

Sawa Mkuu, hapo nimekuelewa, ningekuwa mwandishi ningechombezea "kijiji kilichopo umbali wa kilomita kadhaa toka Chalinze mjini..." kutia ladha na kuondoa maswali kama yangu kwenye habari
 
Back
Top Bottom